"Kwa hiyo viongozi wa mkoa walipaswa kuleta mapendekezo yao Makao Makuu ya Chama cha Albino Tanzania, maelekezo ambayo walipewa wafanye hivyo na Katibu Mkuu na kila jambo linalofanyika katika chama lina hatua zake za kupitia hadi kufikia kuwa tamko la chama," ilieleza taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa matamko ya mikoani yanaweza kutolewa na Mwenyekiti wa Mkoa kwa kupata baraka kutoka Makao Makuu na kusema kuwa Chama kinaiomba serikali kuelewa na kwamba kipo nayo bega kwa bega kushirikiana kwa masuala mbalimbali kwa manufaa ya Albino wa Tanzania.
kauli hiyo imekuja baada ya Chama cha Walemavu wa Ngozi Albino (TAS) Mkoa wa Shinyanga kusema kuwa baada ya kupokea mafuta aina ya ENAT Natural vitamin E cream kutoka nchini Australia, wamebaini kwamba yana madhara makubwa kwao na hayafai kutumiwa na albino hapa nchini.