Tarime na Rorya, Mara: Watu 18 mbaroni kwa tuhuma za mauaji kwa kutumia mishale yenye sumu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara, linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia kisha kumchoma mishale yenye sumu mkazi mmoja wa kitongoji cha Mwara bw.Magige Mesenda na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya tarime na rorya kamishina msaidizi,Mwandamizi SACP Henry Mwaibambe,amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikijihusisha na mauaji ya watu mbalimbali kimekamatwa kikiwa na silaha za jadi ambazo zimekuwa zikitumika kufanya vitendo hivyo vya mauaji.

CHANZO: ITV
 
Weka picha
Picha sina mkuu.

''Uhungu" ndio jina la sumu kwa kabila letu, kwa sasa haya mambo yamepungua sana yanakaribia kutoweka kabisa.

Hiyo sumu hutengenezwa halafu hupakwa kwenye ncha ya mshale, ukimshoot mnyama hiyo sumu ikiingia mwili na mshale inaua.

Watu waliitumia kuwinda wanyama wakubwa pamoja na swala kwa ajili ya kitoweo
 
anhaa vipi na athari ya hiyo sumu kwa huyo mnyama uliyemuua...?? sumu inasambaa mwili mzima au
 
Back
Top Bottom