GE2025 TARIME MJINI: CCM Makao makuu wanapambana kufanya maridhiano mgombea ubunge ACT - Wazalendo ajitoe kumuokoa Esther Matiko asiyekubalika

GE2025 TARIME MJINI: CCM Makao makuu wanapambana kufanya maridhiano mgombea ubunge ACT - Wazalendo ajitoe kumuokoa Esther Matiko asiyekubalika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tarimemjini

Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
71
Reaction score
142
Juhudi kubwa zimefanyika ili wananchi na wana CCM Tarime kumkubali Esther Matiko lakini zimeshindikana.

Vilanza vitisho toka kwa Mkuu wa Wilaya dhidi ya watu walioandamana kupinga uteuzi wa Esther Matiko ambayo sio chaguo la wana CCM Tarime mjini.

Baadae kikaitwa kikao cha maridhiano kati ya baadhi ya waliokuwa wagombea lakini bado maridhiano yakabaki ya usoni lakini watu wakitoka kwenye kikao bado wanakaza.

Kwa sasa kilichobaki ni makao makuu ya CCM kufanya maridhiano na mgombea wa Act-Wazalendo kwa kumuhonga cheo ndani ya serikali au kwa kumpa pesa watazokubaliana.
 
Wamekuwa waoga sana. Kwa hiyo majimbo yote wanataka wachukue wao?

Walifikiri kuizuia Chadema kushiriki uchaguzi itawapa wao ahueni?

Ndio wajue watanzania kwa ujumla hawaitaki CCM.
Pale Mwanga wamemuhonga Henry Kilewo aliyekuwa agombee CHAUMA hakuchukua hata fom
 
Waliofika 100 achukue na kusepa, akikaza fuvu atachezea vitasa siku za mwishomwisho
 
Kama CCM sasa imefikia hadi kuihofia ACT basi imeshakufa inasubiri kuzikwa.

Na huyu kijana Jackson Kangoye akikubali kujitoa atakuwa amesaliti wana Tarime mjini na hatutotaka kumuona tena sura yake
Na akikubali kujitoa atakuwa hana utofauti na bar maid, wana tarime tusichotaka ni kuchaguliwa msaghane ambaye hakuwa kwenye mpango
 
Back
Top Bottom