Tarime: Mapolisi watimka

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Tarime: Mapolisi watimka

2008-10-17 22:27:23
Na Emmanuel Lengwa, Jijini


Wiki moja tu, baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime kumalizika, wale askari zaidi ya 400 wa kikosi maalum cha kutuliza ghasia, FFU, iliodaiwa kwamba walipelekwa huko kudhibiti wizi wa mifugo na mapigano ya koo wameshafungasha virago na kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Askari hao waliotumika vema kudhibiti vurugu za wafuasi wa vyama vya siasa, na wakalazimika kutumia nguvu ya ziada ikiwa ni pamoja na kutembeza virungu, kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na maji ya kuwasha, walikuwa chini ya Kamanda wa Operesheni Maalumu nchini, Kamishna Venance Tossi.

Uchunguzi wa Alasiri umebaini kuwa hata Kamishna Toss mwenyewe ameshaondoka mkoani Mara.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow amethibitisha kuwa askari wote wageni waliopelekwa Tarime tayari wamesharejea kwenye vituo vyao.

Akasema huko Tarime hivi sasa wamebaki askari wake tu, ambao ndio wanaendelea na kupambana na matukio ya wizi wa mifugo, mapigano ya koo na kulinda amani kwa ujumla.

``Tarime wapo askari wangu tu, wale wengine tayari wamesharudi kwenye vituo vyao vya kazi, waliondoka mara tu baada ya uchaguzi kumalizika,`` akathibitha Kamanda Barlow.

Alasiri ilipowasiliana na Kamanda Tossi kwa njia ya simu, alisema sio jukumu la mwandishi wa habari hii kujua mahali alipo wala anapofanyia kazi kwa sasa.

``Wewe shida yako ni nini? Sio jukumu lako kujua nilipo, maana wewe sio mwajiri wangu, maswali yako kuhusu operesheni ya Tarime muulize IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema),`` akawaka Kamanda Tossi.

Kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wilayani Tarime, Kamanda Tossi na Barlow kwa nyakati tofauti waliulizwa na Alasiri ikiwa askari hao wa FFU wanapelekwa huko kwa ajili tu ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime au la.

Hata hivyo makamanda hao walipinga vikali madai hayo na kusema kuwa kikosi hicho maalum kilipelekwa huko kwa ajili ya operesheni ya kumaliza wizi wa mifugo na mapigano ya koo yanayoendelea Tarime.

Leo Kamanda Barlow alipokumbushwa kauli yake hiyo, amesema wakati ule walifanya tathimini na kuhisi kwamba wakati wa kampeni na kwenye uchaguzi, kungekuwa na uwezekano wa kukithiri kwa uhalifu na ndio sababu wakapelekwa askari zaidi wa FFU.

``Tathimini yetu wakati ule ilionyesha kuwa huenda matukio ya uhalifu yakaongezeka wakati wa kampeni na kwenye uchaguzi na ndio sababu wakaletwa askari wale, kwa kifupi walikuja kwa ajili ya uchaguzi na sasa wamemaliza kazi na kuondoka,`` akasema Kamanda Barlow.

Kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime zilitawaliwa na vitendo kadhaa vya kihalifu, ambapo ilifikia hatua hata baadhi ya wanasiasa kufanyiwa vurugu ikiwa ni pamoja na kupopolewa mawe.

Miongoni mwa walioonja kadhia hiyo ni Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliyepasuliwa ngeo kwa mawe na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi aliyenusurika kupigwa mawe baada ya polisi kuzima vurugu kwenye mkutano wake.

Uchaguzi mdogo wa Tarime ulifanyika Oktoba 12 mwaka huu ambapo mgombea wa CHADEMA, Bw. Charles Mwela aliibuka kidedea na kutangazwa kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo hilo.

SOURCE: Alasiri
 
ni lazima waondoke, kwa kuwa walimaliza kazi waliotumwa na msekwa, na jk ingawa hawakuweza kushinda. kwa kuwa nguvu ya umma ilkuwa kubwa kushinda magari ya deraya na farasi.
 
Back
Top Bottom