Waliokuwa wanapigana wanasifia. Wewe ni nani hata ukosoe mambo mema?
Mambo mema unayozungumzia wewe ni yepi hayo? kuhamishwa kwa masawe ndio jambo jema pekee kwa wanatarime /rorya.
Mara zote wanaoalikwa kwenye sherehe kama hizo huwa ni watu ambao ni wa muandaji wa tukio, na huwa wanasema yale ambayo muandaaji angependa ayasikie.
Tukio la kuandaliwa hili! Hakuna reality hapo
wakuu mmesema ukweli wenyewe, hii ilikuwa ni mipango ya police na mkuu wa wilaya ndo wameandaa watu wao na wakaelekezwa nini cha kuzungumza. Hakuna mzee yeyote wa tarime anaweza kuthubutu kusimama na kumpongeza masawe kwa kazi mbaya ya kutesa na kuuwa wanatarime aliyokuwa akiisimamia.
Mwita Maranya nakubaliana nawe .Kumekuwa an uharamia na hata sasa uko mkubwa .Wame make up story hakika ila hakuna kitu kama wazee wa Kimila kukaa na na Mwema na watu hao watakuwa watu au wazee aina ya Nape wachumia Tumbo but wazee hasa walio ona mauajia ya watoto wao hawawezi kukaa na kusema asante .
Mkuu Lunyungu ni jambo la ajabu lakini ndio ukweli wenyewe kwamba polisi kanda maalum ya tarime/rorya imeongeza machungu kwa wananchi.
Polisi hhao kazi yao ni kuvamia wananchi, kuwapora, kuwapiga, kuwatesa na hadi kuwaua na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Kwa wanatarime kanda maalum ni janga, na kama wakiambiwa wachague kuwepo ama kutokuwepo kanda maalum, watachagua kutokuwepo.
Wizi wa mifugo haujakwisha, mapigano ya koo hayajakwisha, biashara za magendo hazijakwisha na mauaji ya raia katika eneo la nyamongo ndio yanaongezeka. Sasa wananchi wanashangaa hii kanda maalum ilianzishw aili kuwaua na kuwadhalilisha ama kulinda usalama wao na mali zao. Nadhani utakumbuka tukio la polisi hao kuwakamata wananchi na kuwadhalilisha vibaya sana kwa kuwalazimisha kunyonyana nsehemu za siri. Hilo ni jambo ambalo haliwezoi kuvumilika kwa viwango vyovyote vile.
Anyway, tunasubiri kuona utendaji wa kamanda deus kato, kwani masawe alikuwa anafahamika tangu siku nyingi kwamba uwezo wake ni mdogo na haieleweki aliwezaje kupandishwa kuwa RPC, ingawa kuna tetesi kwamba igp mwema alicheza ki-homeboy.