Tariffs za TANESCO zipoje?

Tariffs za TANESCO zipoje?

Kama matumizi yako kwa mwezi yanazidi unit 75 unatakiwa kuwa tariff 1, unit ambazo zinazodi unalipia Tsh 350 kwa unit.

Andika barua ufike ofisi ya TANESCO uliyokaribu nayo ukiomba kubadilishiwa Tariff.

Unaweza kujieidhisha kwa kuangalia kwenye risiti yako ya kununulia umeme inaonesha tariff uliyopo.

Pia unapounganishiwa umeme automatic unakuwa Tariff 1, Tariff 4 unaenda baada ya kuwa umeomba ndio unapelekwa.

Nafikiri ulishawahi kuomba kubadilishiwa Tariff? Kama bado angalia upo Tariff gani kwanza.

Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako unaoutoa hapa jukwaani. Lakini ukitaka kubadilisha kutoka T1 kwenda T4 kwa wale tunaonunua umeme kupitia mitandao ya simu unaambiwa uende na risti ya miezi sita nyuma ndo ushughulikiwe. Wakati umbali wa kwenda ofisi ya tanesco ni sawa na kulipia service charge miezi miwili. Ukitaka haraka utaombwa pesa hii imekaaje mkuu.
 
Nataka kuweka kipima umeme. kitakachopima umeme wangu ktk apartment yangu, Nipo nyumba ya kupanga, inamatumizi makubwa zaidi ya unit 800 kwa mwezi, naomba ufahamu, naambiwa vipima umeme hiv vinapatikana kariakoo, je nikikinunua je Fundi wa mtaani wanafaa kunifungia?
 
Mita ikiwa mpya pale wanapokufungia wanakukopesha units kadhaa ili uanzie. Sasa unapoenda kununua mara ya kwanza unalipa deni na kuendelea kununua umeme kama kawaida. Nahisi hiyo hela ni kwa ajili ya kulipia zile unit za mwanzo na wewe kupata umeme, baada ya hapo utanunua tu utakavyo

Namaanisha kwamba; mimi na wewe tumefungiwa mita mpya,halafu tumekopeshwa 50 units kila mmoja maana hawatoi zaidi au chini ya hapo.Lakini units zikiisha,tunalipa gharama tofauti.Hii inatokana na nini mkuu wakati tumekopeshwa units sawa?
 
Hiyo hutokea ikiwa mita yako ya zamani ilikuwa Deni tu na sio vinhinevyo
 
Namaanisha kwamba; mimi na wewe tumefungiwa mita mpya,halafu tumekopeshwa 50 units kila mmoja maana hawatoi zaidi au chini ya hapo.Lakini units zikiisha,tunalipa gharama tofauti.Hii inatokana na nini mkuu wakati tumekopeshwa units sawa?

Mtu yeyote akifungiwa meter hukopeshwa unit 50 na siku ukienda Tanesco hutakiwa kuzilipia sh 18,178 hii in gharana ya 363.56 kwa kila unit na service charge ya 6,734.40 .
Jumla ya gharama za kulipia unit 50 na service charge ni 24,912.40. Kwa mtu aliyefungiwa mfano mwezi wa 11 na kwenda kulipia mwezi wa 12, lakini mtu aliyefungiwa mwezi wa 11 akaenda kulipa mwezi huo huo halipi service charge na gharama zake ni 18178 tuu
 
Baada ya kupitia michango ya wadau hasa ufafanuzi wa hawa ndugu zetu wa ofisi ya uhusiano Tanesco nimegundua kwamba kumbe ni rahisi sana kujua kiasi cha units za umeme utakazopata kwa fedha uliyonayo. Kwamba unatakiwa kujua vitu vitatu ambavyo ni: (1) Kiasi cha pesa utakachotumia kununua umeme, (2) service charges kwa mwezi pamoja na 22% (yaani 18% VAT, 1%EWURA, 3%REA) (3) bei ya unit pamoja na 22% (kwa mchanganuo niliouonyesha hapo katika namba 2. Mfano kama wewe uko katika Tariff 1 ukitaka kununua umeme formula yake ni hivi: Fedha uliyonayo toa service charge kwa mwezi na 22% yake ambayo ni 5,520+1,114.4=6,734.4. Kiasi kinachobakia gawa kwa bei ya unit ukiongeza na 22% yake ambayo ni 298+65.56=363.56. Kwa hiyo kama una shs. 100,000 utatoa 6,734.4 ambayo ni jumla ya service charge kwa mwezi na kubakiwa na 93,265.6. Hicho kiasi kilichobaki utagawa kwa bei ya unit 363.56 na hivyo utapata unit 256.53. Kama nimechemsha basi wadau mtanisahihisha.
 
Nafikiri ulisoma pia hii Mkuu

1 inakuwa hivi.
1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi

Mfano

Una shilingi 10,000

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh
 
Nilisoma na kuelewa vizuri kaka. Ndipo nikaona nielezee kwa jinsi nilivyoelewa. Na hii ni baada ya kupitia pia moja ya bill niliyowahi kulipa 100,000 na kukuta mahesabu yamekwenda kama nilivyoonyesha kwenye maelezo yangu ya awali. Baada ya kuwa umeshatoa service charge na kubakiwa na 3,266/= naona hapo kwenye kukokotoa 22%VAT ndugu Kolebo utakuwa umekosea kidogo. Kwa sababu hiyo amount iliyobaki kimahesabu inahesabika kama 122% (yaani 1.22). Kwa maana ya kwamba hiyo amount inatakiwa itosheleze manunuzi ya umeme (100%) na pia itosheleze 22%VAT. Kwa hiyo 100% kabla ya hiyo amount ya 3,266 (ambayo kama nilivyosema kwa sasa ni 122%) itakuwa ni 2,677.05 na 22% ya 2,677.05 (siyo ya 3,266!) itakuwa 588.95. Total 2,677.05 + 588.95=3,266. Kwa maana hiyo 2, 677.05 gawia bei ya unit moja 298 (isiyo na 22%VAT) utapata units 8.98. Au kirahisi kabisa kama nilivyokuwa nimefafanua katika maelezo yangu ya awali chukua tu amount iliyobaki 3,266/= baada ya kutoa total service charges per month kisha gawia bei ya unit iliyokwisha meza kabisa 22%VAT (yaani 363.56) utapata unit zilezile 8.98.
 
Kwa hiyo kama una shs. 100,000 utatoa 6,734.4 ambayo ni jumla ya service charge kwa mwezi na kubakiwa na 93,265.6. Hicho kiasi kilichobaki utagawa kwa bei ya unit 363.56 na hivyo utapata unit 256.53. Kama nimechemsha basi wadau mtanisahihisha.
kumbuka unit apte hizo hutamaliza nazo mwezi
mwezi ynaofuata ujue una Deni la Service charge ya 6.734/=
sijui km na gharama nyingine watazipiga
ukweli Tanesco wanatuumiza kwani Eanzania haikutakiwa iwe na umeme wa juu hivyo
 
Ndiyo Mkuu. Hiyo kwa vile inajieleza kabisa kwamba ni monthly service charges inabidi kuzilipa tu hata kama unit zako utakuwa haujazimaliza ndani ya mwezi ulionunua hizo unit. Na hizo gharama zingine za 22%VAT ni wazi zitakatwa kwenye unit utakazonunua. Hivyo ndivyo mimi nilivyoelewa na ninaamini hivyo.
 
Mtu yeyote akifungiwa meter hukopeshwa unit 50 na siku ukienda Tanesco hutakiwa kuzilipia sh 18,178 hii in gharana ya 363.56 kwa kila unit na service charge ya 6,734.40 .
Jumla ya gharama za kulipia unit 50 na service charge ni 24,912.40. Kwa mtu aliyefungiwa mfano mwezi wa 11 na kwenda kulipia mwezi wa 12, lakini mtu aliyefungiwa mwezi wa 11 akaenda kulipa mwezi huo huo halipi service charge na gharama zake ni 18178 tuu

Duuuh! nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu
 
Naomba kukuuliza swali la mwisho.Mfano nimelipa 24,912.40 naruhusiwa kununua umeme wa hela ninayotaka,au inakuaje?
 
Mkuu KOLEBA shukrani nyingi zikufikie hapo ulipo, HapaKaziTu.

Nakuomba unielimishe kuhusu swala la Voltage ndogo kwenye Cutout.
Kwenye Cutout umeme ukipimwa unasoma Volt 170 hadi 180 tu, badala ya kusoma Volt 220 hadi 240 ambazo ndiyo voltage za kawaida kwa mfumo wa umeme wa kiTanzania.

Hata kwenye sockets za ndani ya nyumba umeme ni mdogo, yaani hauzidi Volt 180. Tatizo hili linasababisha hata Friji isifanye kazi vizuri.

Kwa taarifa za vijiweni, nimeambiwa eti tatizo ni Transformer itakuwa ina uwezo mdogo kuhudumia wateja wote waliopo maeneo kama yangu yanayopata umeme kutoka kwenye Transformer hiyo.

Je, nifanye nini au nichukue hatua gani ili umeme ufikie kiwango cha kawaida cha Volt 220 adi 240 ?????

Asante kwa msaada wako mkuu. Ndiyo maana nimeshakuwa addicted na JF.
 
Kwa maelezo haya Tanesco/Tra mnatuumiza kwa kodi nyingi yaani service charge nayo ina Vat 22% pesa inayobaki baada ya service charge ambayo natakiwa ninunulie umeme nayo ina Vat 22% hizi kodi zinafanya gharama za umeme kuwa juu kila kukicha.Ombi langu muongeze uwanja wa watumiaji umeme kwa kiwango fulani kwa mfano wale wa T4 wawe na "range" kuanzia unit 1-100 na bei ya unit iwe hiyo ya Tsh 100/uniti pia iwe T4(a) iwe unit 100-150 kwa bei fulani labda Tsh 150/uniti n.k .hii itawapa unafuu watumiaji wa umeme wengine ambao labda wanavuka kiwango fulani ila hawatumii zaidi ya uniti 120.
 
Mkuu KOLEBA shukrani nyingi zikufikie hapo ulipo, HapaKaziTu.

Nakuomba unielimishe kuhusu swala la Voltage ndogo kwenye Cutout.
Kwenye Cutout umeme ukipimwa unasoma Volt 170 hadi 180 tu, badala ya kusoma Volt 220 hadi 240 ambazo ndiyo voltage za kawaida kwa mfumo wa umeme wa kiTanzania.

Hata kwenye sockets za ndani ya nyumba umeme ni mdogo, yaani hauzidi Volt 180. Tatizo hili linasababisha hata Friji isifanye kazi vizuri.

Kwa taarifa za vijiweni, nimeambiwa eti tatizo ni Transformer itakuwa ina uwezo mdogo kuhudumia wateja wote waliopo maeneo kama yangu yanayopata umeme kutoka kwenye Transformer hiyo.

Je, nifanye nini au nichukue hatua gani ili umeme ufikie kiwango cha kawaida cha Volt 220 adi 240 ?????

Asante kwa msaada wako mkuu. Ndiyo maana nimeshakuwa addicted na JF.

Kwa kiasi cha umeme jokofu linafanya kazi bila tatizo labda liwe linatumia umeme mwingi kutokana na model yake.
Kama eneo lako umeme unaonekana ni mdogo kwanza unatakiwa utoe taarifa kwenye ofisi ya karibu ya TANESCO, pili unaweza omba ubadilishiwe phase labda unayotumia inawatu wengi.
 
Asante kwa majibu mkuu.

Ndiyo, Jokofu (Friji) langu linatumia umeme mwingi.

Sijakuelewa vizuri kuhusu kubadilishiwa phase una maana gani hasa, naomba ufafanue au uelezee kwa namna iliyo rahisi zaidi.
Nyumba yangu inatumia umeme wa 3 Phase, siyo Single Phase.

Vile vile nina jiko la umeme.

Natanguliza shukrani.
 
je,ukitaka kuangali unit zilizobaki/kuongeza unit halafu CIU ikaandika;"Error-77" tatizo huwa ni nini?
 
WATEJA WENGI WANAOTUMIA UNIT CHINI YA 75 HAWANA UELEWA NA HIZO TARRIF. NI WAKATI SASA WA TANESCO AMA KUAMUA KWA DHATI KUUELIMISHA UMMA KUHUSU HIZO TARRIF AU KWAKUWA SASA NI ZAMA ZA TEKNOHAMA WATAFUTE TU SOFTWARE AMBAYO ITAFANYA KAZI "AUTOMATIC" BADALA YA MAMBO YA KUANZA KUANDIKA BARUA KWA MAMENEJA WA TANESCO. KWA HILI NAMUOMBA WAZIRI MUHONGO AINGILIE KATI KWANI KUNA WATEJA WENGI WANAOTUMIA CHINI YA UNITI 75 LAKINI WANAKAMULIWA NA NDIO HAO WANALALAMIKA KILA SIKU KUWA UMEME BEI GHALI KUMBE KUNA ZOEZI LA KUOMBA KUBADILISHWA TARRIF KWA MAMENEJA.
 
Back
Top Bottom