Asante sana brother karibu
KAKA MI MITA YANGU IPO KWENYE TARRIF 4,,ILA MUDA MWINGINE MATUMIZI YANAZIDI UNIT 75_ KWA MWEZI,, JE! TANESCO HAWAWEZI KWELI KUNIONDOA KTK IYO TARRIF 4, YAANI NAHOFIA ILO LABDA,, AU UTARATIBU UPOJE,,maana inatokeaga Mara moja moja Sana matumizi kudhidi, aswa kipindi hiki cha likizo wageni wengi home,,
Kama matumizi yako kwa mwezi yanazidi unit 75 unatakiwa kuwa tariff 1, unit ambazo zinazodi unalipia Tsh 350 kwa unit.
Andika barua ufike ofisi ya TANESCO uliyokaribu nayo ukiomba kubadilishiwa Tariff.
Unaweza kujieidhisha kwa kuangalia kwenye risiti yako ya kununulia umeme inaonesha tariff uliyopo.
Pia unapounganishiwa umeme automatic unakuwa Tariff 1, Tariff 4 unaenda baada ya kuwa umeomba ndio unapelekwa.
Nafikiri ulishawahi kuomba kubadilishiwa Tariff? Kama bado angalia upo Tariff gani kwanza.
boss mimi nimefurahishwa na namna anavyotoa ufafanuzi hapa.
hili shirika ni la uma lakini limejaa ukiritimba sana.
mimi mama yangu nikimnunulia umeme anaweza kukaa miezi 6 unit hazijaisha.
niliomba kubadilishiwa tariff lakini mpaka leo wananizungu.
ninafanya kazi ya kulipa service charge tu.
you can immagine service charge ya miezi 6au 8 inavyokuwa hata unit ntakazopewa ni chache mno
mama yangu anawaza kaa miezi 3ukiangalia salio unaona zimepungua unit 5 labda.
sijui ntasaidikaje?
nahitaji msaada wako.
Naomba uni PM namba yako ili tufuatile kaka
Mkuu Koleba nakushukuru kwa ufafanuzi na hasa huu wa Error 77 umekubali kuzima na kuwaka vizuri
ila nimeshtuka hii ya kujinyima kutumia T1 nikitaka nihamishiwe T4
swali lingine la kifizikia nikizimam Friji kutwa nzima ninapokuja kuiwasha naona inachukua muda mrefu kupata ubarudu na kugandisha nishauri nifanyeje ili isile umeme na ina thermostart 9umeme wa tz umeshakuwa shida )
- kumbe nikiirudisha friji heater na pasi ni lazima nitavuka unit 75 nazo nitatozwa zaidi kwa Tsh 52 yaani kutoka 298/ hadi 350/
- bado Tanesco wanaumiza naona km umeme umepanda kwani matumizi yangu halali kwenye mita ya kizamani yalukuwa hayazidi 40,000/= unit km 120 kwa mwezi
nafanyaje ili kuhamia T4?
Mkuu ile Error 77 imekwisha baada yakufuata maelekezo na kumbe init pia zilikwishaMkuu Nando ni pm namba yako tuongee zaidi utaweza kusaidiwa.
Mkuu ile Error 77 imekwisha baada yakufuata maelekezo na kumbe init pia zilikwisha
asante sana kwa ufafanuzi
lakini bado naomba ushauri wa kuingia T4 kwenye unit 1- 75 @ 100/= (7.500) nikizidisha matimizi ya unit hata 20 bado 7,000/= na 22% nitaokoa vingi kuliko unit 95 kwa T1 X 298/= + 22% ni zaidi ya 28,310/=
bado nipo njia panda niingie T4?
Nashukuru kwa ushauri wako MkuuIla unit 75 kwa sasa ni 9,150 kumbuka kuna makato mengine madogo, zamani kabla Tanesco hawajapandisha bei umeme ilikuwa ni 3,500.
Andika barua kwa meneja ukiomba kubadilishiwa tariff. Ikiwezekana attach risit zako mbili tatu za hivi karibuni kuwekea uzito swala lako. Na wakiona unastahili watakuhamisha tu bila tatizo. Zoezi hilo wala halichukui muda mrefu na ukishabadilishiwa bili yako ya kwanza utaenda kuilipia Tanesco kisha utaendelea na utaratibu wako kama kawaida
Kila la heri mkuu
asante sana mkuu,hii inasaidia maana nimepiga hesabu nimeona kwa siku natumia wastani wa ujnit 3.9,nina friji,taa ,feni na TV,pasi natumia mara chache,vipi kwa utaalamu wako matumizi hayo yanweza kuwa shihi?
Mkuu hapa nyumbani tukiweka umeme Wa laki moja unakaa siku mbili tu na hakuna kabisa vifaa vya kula umeme sana
Wakuu msijichanganye tariff 1 inakuwa hivi.
1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)
Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi
Mfano
Una shilingi 10,000
TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4
Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266
Kila manunuzi yanakuwa na vat
3266 * 22% unapata 718.4
Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.
Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh
Mkuu nilikua natumia meter ya kawaida,wakanibadilishia wakaweka ya luku.Units zimeisha wamesema nipeleke 32,000/= je,ni sawa mkuu?