Tarehe isiyosahaulika na Wamarekani

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
Wengi huita siku ya MaShambulio ya al-Qaida dhidi ya Marekani, Mashambulio ambayo yalichukua takribani uhai wa watu zaidi ya 3000.

Kulitokea mashambulio Manne ambayo yalitumia ndege Nne, Inasemekana watekanyara wa al-Qaida ambao walikuwa 19 walipata mafunzo kwanza ya Kuongoza ndege ili kutimiza shambulio hilo, Baada ya Hapo wakajigawa katika makundi manne, Makundi matatu yakiwa na watu Watano watano na kundi moja likiwa na Wanne.

Ndege ya kwanza Kuiteka ilikuwa ni American Airlines Flight 11, iliyotumiwa kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la mjini New York kama saa mbili asubuhi, Ndege hii iliua abiria 87 na Magaidi 5.

Baada kama ya saa moja mbele Ndege ya Pili iliyoitwa United Airlines Flight 175, ikagonga mnara wa Jengo lile lile la Biashara la Kimataifa upande wa Kusini mnamo saa tatu asubuhi.

Watu wengi waliona tukio hili la pili kwasababu habari zilikuwa tayari zimeshika vichwa katika mji na kila kamera za televisheni zilikuwa zikielekezea macho yao huko katika eneo la tukio, na wakati huo huo ndege ya pili ikagonga tena mnara wa Kusini mwa Jengo hilo, Hivyo tukio hili si lakusimuliwa kabisa kwa wakazi wa marekani, Ndege hii ya pili iliua abiria 60 na magaidi 5.

Baada kama ya Nusu saa mbele, Ndege iliyoitwa American Airlines Flight 77, ikagonga jengo la The Pentagon la mjini Arlington, Virginia (karibu kidogo na Washington DC) ambalo ni makao makuu ya Idara ya Ulinzi ya Marekani, Pia dege hili likawa limeenda na Abiria 59 na magaidi 5.

Baada ya Nusu saa nyingine ndege ya United Airlines Flight 93 ilianguka chini mjini Shanksville, Pennsylvania bila kugonga jengo lolote, Ina aminika Abiria walipambana kuiongoza ndege hii kutoka kwa magaidi bila mafanikio na kuanguka chini, Target ya Magaidi ilikuwa ni Kugonga Jengo la US Capitol au Ikulu ya White House na Ikashindika hivyo kuua abiria 40 na magaidi 4.

Hivyo Ilikuwa ni siku ya Huzuni sana kwa Wamarekani, Kwa Maana Siku hii ilichukua uhai wa watu wengi wasio na Hatia Kabisa, Ndege zote Nne abiria wake jumla 246 walipoteza Maisha, Magaidi 19 nao wakapoteza Maisha, Katika Jengo la Biashara la Kimataifa watu 2,602 walipoteza maisha, Pia Jengo la The Pentagon watu 125 walipoteza maisha katika vifo hivyo kulikuwa na Zimamoto 343, Polisi wa New York 23, Polisi wa Bandari 37 na wengine wasiojulikana wengi sana.

Marekani ilikiri Haikudhaniwa kuna tukio kama hili lingekuja kutokea, Tena litekelezwe na Watu wanaotoka nje ya Marekani, Marekani mara ya mwisho kutokea shambulio kama hilo ilikua mwaka 1941 pale Wajapani waliposhambulia kituo cha jeshi la maji kilichopo katika Bandari ya Pearl, Hawaii.

Baada ya Shambulio hili, Osama Bin Laden akakimbilia Zake huko Afganistan na Kuhifadhiwa na Taliban, Serikali ya Marekani iliwaomba Afghanistan kumsalimisha Osama Mikononi kwa marekani lakini kiongozi wa Taliban Mullah Muhammad Omar alisema anahitaji uthibitisho kama Osama anahusika na shambulio, Raisi wa marekani wakati huo George W. Bush akasema ahitaji kuthibitisha hilo, Ndipo Marekani ilipoanza vita na Afganistani maarufu kama War on Terror (WoT) ambayo ilianza 11 September 2001 na inadumu mpaka leo dunia nzima si Afganistan tu japo tarehe 23 May 2013 Raisi Barack Obama aliwahi sema haitakuwa Global, Bali italenga makundi kadhaa tu.

MASWALI YA KITAALAMU......

Majengo Pacha (Twins Tower's) ambayo ni Majengo ya Biashara ya Kimataifa (World Trade Center) huwa yana majina kila moja, La Kaskazini Linaitwa WTC1 na la Kusini Huitwa WTC2.

WTC2 lililogongwa saa (8:46) asubuhi lilitumia dakika 56 tu Likaungua na Kuanguka kuteketea kabisa

Lile lingine la Kaskazini WTC2 lililogongwa Saa (9:02) nalo likatumia dakika 102 tu likaanguka na kuteketea kabisa.

Kuanguka kwa majengo haya marefu kulisababisha majengo ya pembeni nayo kushika moto, hivyo hata jengo lingine la 7WTC lililokuwa pembeni likaanguka pia saa (5:20) ulikua ni uharibifu usiovumilika.

WTC1 ilianza Kujengwa mwaka 1968 na WTC2 ilianza kujengwa mwaka 1969 huku 7WTC ilijengwa mwaka 1984

Swali walilouliza wataalamu wengi wa ujenzi lilikuwa "Ilikuwaje Majengo yale Yaungue na Kuanguka kisha kuteketea kabisa"?

Swali ni muhimu sana hili kwakuwa majengo haya Yalijengwa kwa Nguzo za Chuma kwa Zege, Ilikuwaje yaanguke kwa wastani wa sekunde 9 tu lingine likianguka kwa wastani wa sekunde 11 Pekee.

Manusura mmoja aliyeitwa Bruno Dellinger aliyekuwa akifanya kazi WTC1 Gorofa ya 47 alihojiwa na BBC na kusema "Baada ya sauti kubwa ya kuporomoka kwa jumba lile, kila mahali kulibadilika na kuwa kweusi kutokana na moshi uliokuwa ukifuka na milio kadhaa na sikuweza kupumua"

BBC pia ilimuhoji Professor Eduardo Kausel katika Idara ya Uhandisi wa Kiraia na Mazingira katika Taasisi ya Teknolojia.

Profesa Kauseli anajua wazi wengi wetu tukiulizwa kwanini yale majengo yalianguka tutasema yalianguka kwa sababu ni tukio la kigaidi.....

Lakini yeye Kauseli anasema Jibu la swali hilo litakuwa na mfululizo wa matukio ya kimuundo na kemikali ambayo yalileta janga ambalo hakuna mtu, wakati huo, alikuwa na uwezo wa kufikiria.

Baada ya Tukio, Marekani ilitumia taasisi mbili NIST na MIT kujua kwanini majengo yale yalianguka, NIST na MIT iliingia kazini mwaka 2002 na Mara ya mwisho kutoa tafiti ilikua mwaka 2008

Taasisi zote zilikuja na majibu sawa kuwa:
++Kama kungekuwa hakuna moto, majengo yasingeanguka;

++Na ikiwa kungekuwa na moto tu, bila uharibifu wa majengo, yasingeanguka pia.
++Joto ambalo lilifika 1,000 ° C, lilisababisha glasi kwenye madirisha kupanuka na kuvunjika, ambayo ilileta hewa ambayo ilitumika kama chakula cha moto, Moto ulichochewa na hewa na ndio sababu ulienea.
++Takwimu rasmi zinakadiria kuwa kila ndege ilibeba takribani galoni 10,000 za mafuta (zaidi ya lita 37,850).
Mafuta mengi yalichomwa , lakini pia kulikuwa na mafuta mengi ambayo yalimwagika kwenye ghorofa ya chini ya majengo pacha.

Hivyo Kulingana na Utafiti wa hawa jamaa inaonekana Moto ulivyokiwa mkali, Joto likazidi, Vyuma kama kawaida vikipata joto hupanuka hivyo vikaachia muhimili wa jengo na kuanguka.

Hivyo Hata majengo yalipoanguka hewa bado ilisukumwa zaidi ndio maana kukawa na wingu zito, Kausel anasema ni sawa majengo yalianguka kwa sekunde lakini moto katika vifusi uliendelea kuwaka kwa siku 100.

Hii ni video ikionyesha Mawasiliano ya Airport na marubani wa ndege hizo, Pia baadhi ya Phone records za wahanga walizoachia watoto na wapendwa wao.

#WeRemember911
#NeverForget
#9/11

Polycarp Mdemu
998839bc029be3f2ae376adafba5d1a3.jpg
 
Kuna uwalakini wa kitaalamu ambao umekuwa mgumu kuelezeka jinsi majengo yale yalivyoanguka kiurahisi namna ile. Hata hii leo asubuhi kwenye twitter nimesoma engineer mmoja anauliza inakuwaje mafuta ya ndege yakayeyusha vyuma na kila kitu kwenye majengo marefu kama vile? Imekuwaje kukawa na picha moja tu inayoonyesha shambulio la pentagon? Ina maana kulikuwa na camera moja tu kwenye jengo muhimu kama lile kwa ulinzi?

Mwenyezi Mungu ndiye anayejua ukweli.
 
Back
Top Bottom