Nelly
JF-Expert Member
- Jan 25, 2020
- 5,666
- 11,123
Huu ndio ulikua mtihani mkubwa.. Kama ulikua huna "backup ya maana" ilikua ni msiba ule paleeUlifanikiwa vipi kurudi nyumbani
Huu ndio ulikua mtihani mkubwa.. Kama ulikua huna "backup ya maana" ilikua ni msiba ule paleeUlifanikiwa vipi kurudi nyumbani
Kuna mwamba alikuana vidole viwili vyenye wino.. NilistaajabuKinacho furahisha ni kwamba Ile challenge ya kuonesha kidole baada ya kupiga kura ilikufa rasmi
Lingine Cha kufurahisha baadhi ya halmashauri kuliko tokea sekeseke huwezi kukutana na upuuzi wa mabango ya green
Kwa Dar kweli watu waliopiga kura ni wachache sana. Nilipita kwenye vituo vinne nikielekea Goba sikuona watu zaidi ya wasimamizi, ilikuwa ni saa3 hivi. Hata kama kusingekuwa na maandamano, bado serikali na wahuni wangejisikia vibaya sana maana hakukuwa na wapiga kura.Yaani nyie wote mliotoa ushuhuda hapa hakuna hata mmoja alie ianza hiyo siku na kupiga kura?
Ni maajabu
Yaan km mie tyuuh, kila nikikumbuka napatwa na kiwehu wehu.Kwa mkasa ulionikuta nikisimulia tena nitapata depression upya. Bado siamini kama ni kweli aisee
Nilirudi lakini kiutata sana,Ulifanikiwa vipi kurudi nyumbani
Kumbe polis walikuwa wamejipanga kabisa kuua,yaan ndo pamenuka tu wakaanza na kurusha risasi za moto!Ilinikuta geita hakukua na dalili yoyote ya maandamano rkn ilipofika saa8 tulipata taarifa huko kwa majirani zetu katoro yakua kimenuka sisi mda huo tunafanya biashara kama kawa amani ya kutosha
ilipofika saa kumi kama na nusu tukasikia et mitaa ya nyakumbu geita kimenuka mimi hata sikushituka kwasababu nilijua amani ipo baada ya nusu saa niliona kwa kasi watu wanakimbia wengne wanafunga maduka chapu, naami nikaanza kurusharusha bidhaa zilizokua nnje kwa kasi ile namaliza tu mabomu ya machozi
sija kaa sawa ile njia ya kwenda home kila nnapokimbilia polisi wapo nikajikuta nipo kati kati lile eneo nililokuepo na tulikua wengi ili ukatishe barabara ni kujitoa mhanga mda huo tumejibana kwenye mjumba ya watu vichochoroni na maafsa nao wengine wanashuka kwenye gari kutoka kwenye njia kuu lami kuja vichochoroni ALOOOOOH nilijua nakufa kilichosaidia kalikuja kamvua ka kasi kidogo ndipo nikakatisha barabara na kundi jingne lilinifata pale kati ya barabara tunakimbia alikuepo jamaa kapigwa risasi ya kifuani anatuita tumusaidie
yaani dah jamaa ameshakatalia machoni pangu jamaa bonge hivi sijui alipona Amani ni nzuri tusiombee maandamano isingekua mvua mimi ningekua nmekufa
EXALIOTH
JF--GEITA
Kuna mwamba alikuana vidole viwili vyenye wino.. Nilistaajabu
NB:Havikua vya kwake/sehemu ya mwili wake
Mpaka sasa nikiwaona polis siamin kama kwel waliweza kufanya huo unyamaSikua Kwenye maandamano ila kuna mtoto mmoja hivi aliniita baba nisaidie, kabla sijafanikisha lengo la kumuokoa wakaniwahi wao😢😢😢 Imagine a child between 13-17yrs unamfumua kichwa bila huruma.
Hii kitu sitokuja kuisahau kwa kweli.
Tukisema huyo maza ni shetani mnywa damu sikosei, huyu maza anatakiwa tumtoe madarakan na kumnyonga hadharaniSikua Kwenye maandamano ila kuna mtoto mmoja hivi aliniita baba nisaidie, kabla sijafanikisha lengo la kumuokoa wakaniwahi waoImagine a child between 13-17yrs unamfumua kichwa bila huruma.
Hii kitu sitokuja kuisahau kwa kweli.
OkTarehe 29, me nliamua kubaki ndani kama taadhari incase maandamo yatatokea, mpaka saa saba mchana huku mtaani kwetu palikua shwari kabisa hapakua na dalili za maandamano, nkaamua nimuite demu mmoja aje kunipa kampani home, alikuja fresh... ilivofika mida ya saa tisa tukaanza kuskia milio ya risasi huko nje, kumbe tayar palishaanza kuchangamka, plan ilikua mtoto wa watu arudi kwao by saa 12 jioni lakini kwa hali ilivyokua hatari ikabidi alale tuu home,
Kesho yake tarehe 30 ndo alirudi kwao, nashukuru Mungu alifika salama
Watu walimiminiwa risasi bila huruma nchi ina laana hiiMi nilikuwa Ubungo Maziwa saa nne kasoro nikavuka fresh kale kadaraja ka watembea kwa miguu kuingia EALC ,Ile nafika yard ya mwendokasi chuma zinalia nyuma ilibidi nilaze mshale mpaka Emmaus Center kituo Cha Wakarismatiki Wakatoliki nikajisemea bora waniulie kanisani.
Nimekaa hapo mpaka saa kumi na Moja anga limetulia njia zote zimefungwa .
Ninaamini watu wengi wemeuwawa wakati wakitafuta namna ya kurudi nyumbani kutoka mafichoni.
NA siyo kila polisi alipiga risasiMpaka sasa nikiwaona polis siamin kama kwel waliweza kufanya huo unyama
Yaan mim simlaumu samia ila nabaki kuwashangaa tu hawa polis wana roho gani
Hv karibun nipo road nikawaona yaan ile kuwaona tu nikajaa hasira ila bahati nzur hawakunisimamisha ila kama wangenisimamisha sjui tungejibizana vipi maana mwili ulikuwa umewaka tayar
Sahihi mkuuTukisema huyo maza ni shetani mnywa damu sikosei, huyu maza anatakiwa tumtoe madarakan na kumnyonga hadharani
Msingi wa kuandamana ulikua Nini..Leo tupeane ushuhuda wa Tarehe 29 ilikukuta wapi, ilikuaje ulivyoshtuka watu wapo barabarani?Na jee kuna story gani za watu waliouliwa uliziskia ukashtuka au zilizokuhuzunisha?Kipi kilikushangaza?Leo tupeane habari kuhusu tarehe 29
Nianze na mimi binafsi kabla ya tarehe 29 na marafiki zangu wanne tulipanga tutatoka kuandamana....Nakumbuka tulifanya kikao jumamosi ya tarehe 25 tukiwa watano tukijadili mambo ya nchi na jinsi tulivyojiandaa kuandamana
Tupo watu watano ambao tunaaminiana sana na tunashirikishana katika mambo nyeti kama haya.Kwa hali ilivyokua social media zilivyokua za moto tulijua kabisa tarehe 29 uhakika wa kutoka ni mkubwa.
Twende mbele kufupisha mambo,tarehe 28 tulikutana tena tukipiga story kuhusu tumejiandaa vipi nakumbuka jamaa yangu mmoja.alisema what if watu hawatotoka?Nikajisemea liwalo na liwe.
Usiku wa kuamkia tarehe 29 nakumbuka tulikua macho mtandaoni mpaka saa 7 usiku, nikaenda kulala nikiwa na shauku kubwa sana.
TAREHE 29 ASUBUHI...
Tuliamshana tutoke mapema saa 11 ila rafiki yangu akanambia tutoke saa 12 muda wa maandamano kuanza.Niliswali nikamuomba Mungu sana na wife alikua siku zote hataki nikaandamane akihofia nitauwawa japo haipendi serikali ya Samia wala ccm lakini alikua ananisihi nisiamandane, lakini nilimweleza ukweli wote kuwa ishu ya kuandamana inaanza na kila mmoja nikisema sitoki na yule akisema hatoki jee ni nani atatoka?
Kusubiriana tulijikuta tukikutana Goba tulikua jumla wanne tu pamoja na mimi yule mmoja tuliona anatuchelewesha
SAFARI IKAANZA
Tulitoka Goba kiukweli palikua hamna hata dalili ya maandamano, tukaenda hadi mbezi mwisho napo hakukua na dalili za maandamano, yule jamaa yetu ambaye alichelewa kutoka alitufata hadi mbezi mwisho kwa boda boda.Tulikaa mpaka saa tatu na robo hamna dalili ya maandamano kabisa kiasi kwamba tukaanza kukata tamaa na kilichoudhi ni kufungua mitandaoni na kuona barabara zote ni nyeupe na hakuna dalili za maandamano yoyote yale.
Tulikaa mahali hapo mbezi tukaanza kuulizana sasa itakuaje?Kiukweli nilijikatia tamaa na nilikua na hasira balaa nikasema why watanzania tumekua waoga kiasi hichi, tulikaa mbezi mpaka tukawaza turudi tu majumbani mwetu hapo nilikua na hasira balaa nikasema nikifika home siongei na mtu yoyote zaidi nitalala tu.
Nilikua nishakata tamaa kabisa, tukaona tuingie mgahawani tunywe tu chai maana tangu tulipotoka tulikua hatujala chochote.
MAANDAMANO YAKAANZA RASMI
Tumemaliza kunywa chai tunaanza kurudi zetu Goba ile tunavuka njia panda ya Goba ndo naona mtandaoni watu wameanza kujikusanya ubungo Kibo, Aisee hatukua na jinsi kwa haraka tulichukua pikipiki kila mmoja hadi Kibo, nilishuhudia watu kwa mamia wakielekea Kibo wakisogelea eneo ya Kibo nyomi za mbezi kimara zote zilielelekea Kibo!!
ITAENDELEA