johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,135
Wasamehe bure, wengine walikuwa hawajazaliwa bado.Alifurumushwa na makomandoo?
Tanzania kila mwanajeshi ni komandoo kwani?
Baadhi ya watu mnau-overrate sana huo ukomandoo.
Usilolijua ni usiku wa giza waganda wenyewe walikua upande wa watanzani kuwapa plot nzima ya kumuondoa dikteta uchwara Nduli.
Hata Yoweri Museveni alikua akipigana kwa upande wa Tanzania ndio ujue ni jinsi gani vita ile tulisaidiwa na wananchi waliochoka utawala wa mabavu.
Usemayo ni kweli tupu mkuu...pia iddi amini alipata msaada wa silaha na askari toka Libya, na Palestina [ PLO].
..vikundi vya waasi kama Museveni vilituhitaji zaidi Watz, kuliko sisi tulivyowahitaji wao.
..ila ni ukweli kwamba wananchi wa kawaida wa Uganda walikuwa wamemchoka Iddi Amini, na waliwapokea askari wetu kwa furaha na shangwe na kuwaita " WAKOMBOZI. "
Usemayo ni kweli tupu mkuu.
Historia halisi ya Tanzania nilichokuja kugundua ina mazonge sana uhalisia umefichwa.
Leo hii mtu kama John Okello hana cha kukumbukwa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.
Najaribu kuwaza kama lile somo uchwara la historia lilokuwa mbioni kuanza na vitabu viwe vya kumsifia chifu wa chato sijui watoto wetu wangekuwa na mentality ipi huko vizazi vijavyo.
👍....Lakini pia Watz. wengi (including Wanajeshi) walikuwa wameudhika vya kutosha na maneno ya kejeli/dharau na ya Ufidhuli kutoka kwa Iddi Amin kwa Watz. na kingozi wao "Musa" kiasi kwamba waTz wakajiuliza hivi huyu jamaa Nyerere ana nini mbona anamwogopa Nduli? ? Kwa hiyo WaTz walijawa na usongo mkubwa kumwadhibu Nduli na kuombea... ngoja ije siku tu Waambiwe "Haya Piga" .......pia iddi amini alipata msaada wa silaha na askari toka Libya, na Palestina [ PLO].
..vikundi vya waasi kama Museveni vilituhitaji zaidi Watz, kuliko sisi tulivyowahitaji wao.
..ila ni ukweli kwamba wananchi wa kawaida wa Uganda walikuwa wamemchoka Iddi Amini, na waliwapokea askari wetu kwa furaha na shangwe na kuwaita " WAKOMBOZI. "