Tarehe 27/01/1971 Jenerali Idd Amin alijitwalia madaraka ya kuiongoza Uganda kabla ya kufurushwa na Makomandoo wa Tanzania 1978/79!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,561
Nichukue fursa hii kulipongeza jeshi letu tukufu la JWTZ kwa kazi njema waliyoifanya mwaka 1978/79 na kuwarejeshea Wananchi wa Uganda uhuru wao.

Jenerali Iddi Amini alipindua serikali na kuingia madarakani kihuni.

Maendeleo hayana vyama!

cc: Mmawia
 
Usilolijua ni usiku wa giza waganda wenyewe walikua upande wa watanzania kuwapa plot nzima ya kumuondoa dikteta uchwara Nduli.

Hata Yoweri Museveni alikua akipigana kwa upande wa Tanzania ndio ujue ni jinsi gani vita ile tulisaidiwa na wananchi waliochoka utawala wa mabavu.
 
Usilolijua ni usiku wa giza waganda wenyewe walikua upande wa watanzani kuwapa plot nzima ya kumuondoa dikteta uchwara Nduli.

Hata Yoweri Museveni alikua akipigana kwa upande wa Tanzania ndio ujue ni jinsi gani vita ile tulisaidiwa na wananchi waliochoka utawala wa mabavu.

..pia iddi amini alipata msaada wa silaha na askari toka Libya, na Palestina [ PLO].

..vikundi vya waasi kama Museveni vilituhitaji zaidi Watz, kuliko sisi tulivyowahitaji wao.

..ila ni ukweli kwamba wananchi wa kawaida wa Uganda walikuwa wamemchoka Iddi Amini, na waliwapokea askari wetu kwa furaha na shangwe na kuwaita " WAKOMBOZI. "
 
Usemayo ni kweli tupu mkuu.

Historia halisi ya Tanzania nilichokuja kugundua ina mazonge sana uhalisia umefichwa.

Leo hii mtu kama John Okello hana cha kukumbukwa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Najaribu kuwaza kama lile somo uchwara la historia lilokuwa mbioni kuanza na vitabu viwe vya kumsifia chifu wa chato sijui watoto wetu wangekuwa na mentality ipi huko vizazi vijavyo.
 
..kwa maoni yangu wanaotia mazonge na kupotosha historia ya vita vya kagera ni vijana wa miaka hii na sio wazee au watu wazima waliokuwa na akili zao wakati vita inapiganwa.

..pia kuna vitabu na maandiko ya kutosha ya kumuwezesha mfuatiliaji kuujua UKWELI. Upotoshaji kuhusu vita vya Kagera / Uganda umejaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

..lakini pia Watanzania wakati mwingine ni kama wanaamini zaidi habari za uongo kuliko za ukweli. Tuna bahati mbaya sana kwamba waongo-waongo ndio wanaoaminika zaidi ktk jamii yetu kuliko wanaosema ukweli.
 
Makomandoo wale sio hawa akina Urio Bwire Adamoo na Linjenje..wasingeweza
 
..pia iddi amini alipata msaada wa silaha na askari toka Libya, na Palestina [ PLO].

..vikundi vya waasi kama Museveni vilituhitaji zaidi Watz, kuliko sisi tulivyowahitaji wao.

..ila ni ukweli kwamba wananchi wa kawaida wa Uganda walikuwa wamemchoka Iddi Amini, na waliwapokea askari wetu kwa furaha na shangwe na kuwaita " WAKOMBOZI. "
👍....Lakini pia Watz. wengi (including Wanajeshi) walikuwa wameudhika vya kutosha na maneno ya kejeli/dharau na ya Ufidhuli kutoka kwa Iddi Amin kwa Watz. na kingozi wao "Musa" kiasi kwamba waTz wakajiuliza hivi huyu jamaa Nyerere ana nini mbona anamwogopa Nduli? ? Kwa hiyo WaTz walijawa na usongo mkubwa kumwadhibu Nduli na kuombea... ngoja ije siku tu Waambiwe "Haya Piga" .....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom