Tanzia Tanzania: Wakati Watanzania wako hoi kiuchumi chama Tawala kiko bize kuua Upinzani.

VUGU-VUGU

Senior Member
Feb 24, 2017
160
500
Wanabodi,
Wasalaam.

Ikiwa ni miaka miwili tangu kumaliza kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Tanzania hali si shwari kisiacha,kiuchumi,kiutamaduni na kiusalama.Tanzania ya sasa ni tofauti kabisa na ile ya miaka mitatu iliyopita katika nyanja hizi za kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kiusalama.
Watafiti wa masuala ya kisiasa na kiuchumi wamekuwa wakitoa Taarifa zenye kuashiria mwenendo usioridhisha wa Taifa letu katika siasa na uchumi.Nawaomba tutafakari juu ya haya;

Kufilisika kwa Mabenki ya Biashara,Tanzania mpaka kufikia June 2014 kulikuwa na mabenki takribani 53 ya kibiashara, Duniani kote bank ndio kichocheo kikubwa cha Uchumi ,China ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na bank nyingi na kubwa ikifuatiwa na Marekani,Yaani kati ya bank 50 kubwa duniani 11 ziko China huku 6 zikiwa USA huku Ufaransa,Janan & Wingereza wao wakiwa na bank 5 kubwa kila moja.Tazameni hali ya kiuchumi za nchi hizi halafu tafakarini upya swala lenu la kupunguza bank za biashara nchini.

Tangu kuwako kwa serikali ya awamu ya Tano kwa mara ya kwanza katika Taifa hili tumeshuhudia bank zikifungwa au zikidhoofika huku mkuu wa nchi akitamani zifungwe na abaki na bank chache tu kama ilivyo kwa Uganda yenye mabenki 26 huku jumla ya Watu ikiwa 41.9m sawa na ratio ya (1bank: 1,615, citizens), Huku rafiki zetu wa Rwanda wao wanamabenki 11 huku idadi yao ikiwa 11.9m sawa na ratio ya (1bank :1,090,909 citizens), Tanzania idadi ya watu ni 54m mabenki tuliyonayo ni 53 sawa na ratio ya ( 1bank :1,018,867 citizen ), Ukitazama uwiano huu nadhani utajifunza kitu.

Baadhi ya mabenki yenye hali Mbaya.
National Bereau de Change LTD/Twiga Bancorp LTD iliyoanzishwa Tangu mwaka 1992 ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa zaidi ya miaka 25 ila kwa awamu hii imeishiwa pumzi na 28/10/2016 iliwekwa chini ya BOT.

Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprise LTD ( PRIDE) iliyoanzishwa Tangu mwaka 1994 imefanya kazi kwa zaidi ya miaka 23 ila katika awamu hii imeishiwa pumzi na wakati wowote itafungwa huku ikiwaacha wateja wake zaidi ya 100,318 kwenye Matawi yake zaidi 70 yaliyoko nchi nzima.
Mbinga community bank. Hii nayo imeshindwa na imeishiwa pumzi katika awamu hii ya tano,Niwakumbushe kwenye kusajili hizi community bank mtaji lazima uanzie na bill 2 huku zile za biashara mtaji ni 12 bill.

Banki ya Wananchi Mwanga, Hii nayo awamu hii imeishiwa pumzi na sasa iko taabani.
Hii ni baadhi kwani ziko nyingi kwani zinakabila ukuaji mkubwa wa NPL kwani wateja hasa wa mikopo wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.


My take! Nashangaa sana kuwaona vijana,wazee na akina mama wa chama Tawala wako bize na kuua upinzani nchini kitu ambacho naamini si hitaji la watanzania kwa sasa kuona inchi yetu haina upinzani, ili hali hali ya Taifa kiuchumi ni mbaya sana, Huku mkuu wa nchi akituletea kejeli kwamba kama vyuma vimekaza tuweke grice,

CCM nadhani ni wakati wa kutatua matatizo ya watanzania kwani kipaumbele chao sio ninyi kuua upinzani bali wao kuwa na maisha bora.

Marry-xmass and Happy new year 2018.
..........................................................
 

Tanzania ya Watanzania

Senior Member
Apr 9, 2017
145
250
Vugu vugu tatizo lako unapotea sana ila unaakili sana wewe,Umenena kwa mifano kabisa hali ni mbaya sanaaa huku.

Asante sana ,Najua kuna watu watakupuuza ila umeeeleza ukweli mtupu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom