Yule mshairi maarufu wa CCM, Salum Tambalizeni, amefariki. Alimnadi Mkapa mwaka.95. Chama wametoa taarifa hii. RIP...
Aisee wewe wacha kamba bana, Tambalizeni nyumbani kwake ni Kiwalani minazi mirefu.
Taarifa za kifo chake bila shaka ni habari njema sana kwa JK maana mwaka 2005 huyu Tambalizeni alifuatwa na Kikwete akimuomba amfanyie kampeni kwenye kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea Urais upande wa CCM lakini Tamba alimjibu Kikwete hapa Rais ni Salim Ahmed Salim tu.
Kikwete alikasirika sana na kumuuliza hata wewe wa ukae unanifanyia hivi? Subiri tutaonana Kikwete akimuahidi Tamba kwa uhakika huku akijuwa Rostam na Lowasa yatosha kuuvusha mtandao.
Hatimaye JK akaingia katika ufalme na kuhakikisha vile vitenda vya kuimba mashairi kwenye kampeni wanapewa Bongo fleva na Tot tu.
Na Jk alihakikisha Tamba hakuna uchaguzi wowote ndani ya chama atakaoshinda na hatimaye akapoteza Unec na dili zote za kukatisha korido za Lumumba zikaishia hapo na ndio likawa kaburi lake la kisiasa na mbaya zaidi hana elimu sina hakika hata kama alifanikiwa kumaliza darasa la saba na hii ndio sababu iliyomfanya Mkapa akiwa madarakani ashindwe kumpa japo Udc.
Tegemeo la mwisho la Tamba ikawa ni Malumbo Secondary school mali ya Philiph Mangula na wajanja wenzake ambapo Tamba kwa heshima ya Mkapa akapewa share na kuwa mmoja wa wakurugenzi lakini tatizo la Mzaramo huyu anapenda ngono utadhani kachanjiwa.
Ndipo akashindwa kulipa masuprier wa chakula shuleni wakambuluza Mahakamani na nyumba yake kutangazwa mnada, ashukuliwe Mkapa ndiye aliyemchangia million 25 na Mangula sina hakika alimchangia ngapi na Salim alimchangia million 10 ndipo nyumba ikasalimika.
Ilibidi aishi kama digidigi ila baada ya mieza kadhaa Tamba aliibuka kutoka mafichoni na kununuwa daladala mbili kwa mpigo huku nyuma akiziandika kwa Mungu madogo na akanunuwa na usafiri wake binafsi Mark 2 Grand na kukata vilimilimi waswahili wote wa Kiwalani.
Kwakweli inasikitisha na nazidi kuona umuhimu wa shule, huyu jamaa angekuwa na shule japo kidogo tu basi angekuwa mtu mzito sana serikalini maana Tamba na Mzee Jongo ndio yalikuwa majembe ya Mkapa. Hawa wote wametokea Jumuiya ya wazazi.
Bila shaka Benjamini Mkaoa atahudhuria haya mazishi ambayo possibly lazima yafanyike kijijini kwao Marumbo.
Pole sana Kingwendu kwa kumpoteza home boy ambaye kwenye ufalme wake alikuoa sana shavu kwenye mikutano ya Maccm.
Cc😡Ritz chama faiza Fox hiyo ndio Ccm yenu Tamba hakuoaswa to die in vain. Hapa bila kukufuru huyu mtu kifo chake kimeharakishwam mshaurini Jk asikanyage kwenye mazishi licha ya siasa Tamba pia alikuwa ni mganga wa kienyeji kimyakimya. Huwezi ameacha majini mangspi maana hata driver wake alikuwa analalamika asubuhi hawawezi kutoka nyumbani hila kumpigia ramli driver wake ili ajuwe kama hana nuksi kwa siku hiyo.
Huyo ndio Tambam