TANZIA: Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe afariki dunia nchini Singapore alikokuwa anapatiwa matibabu

Jinga kabisa Wewe. Rudi darasani ujifunze maana ya "Mzalendo." "The Butcher of the Zimbabweans" unamwita "Mzalendo!!!?" Tena Kama Rais wetu atahudhuria mazishi yake na kumwita "Comrade" nitajua lao moja!!!

Mkuu nisome vizuri utanielewa, Mimi ni katika wale wasiomkubali huyu jamaa..

Hapo nilipo sema Mzaleno nimeweka alama ya mshangao nikishangaa Mzalendo aliyewahi kuwa Rais wa zimbabwe akaenda kuugulia na kufia Singapore wakati alikuwa ananafasi ya kujenga hospitali bora Zimbabwe na kusomesha madaktari ilihuduma hizo nzuri alizofuata Singapore angezipata hapohapo Zimbabwe..
 
Nimeshtuka na kifo chake..
Huyu jamaa nilikuwa namkubali sanaaa..kifo chake kimeniuma mnoooo
 
R.I.P Comred Mugabe. Aliwahi kusema yeye ni simba anayeongoza jeshi la kondoo barani africa. Kwa maana kwamba viongozi wengi wa africa ni waoga haswa kwa nchi za magharibi.

Pumzika kwa amani.
 
Leo umemsahau unforgettable??

Anyway kifo cha Mugabe
Tutaona unafkki wa watu
 
10. Alimwambia balack Obama kuwa kama anataka nchi ya zimbabwe ikubaliane na ndoa ya jinsia moja basi yeye amuoe Balack Obama.

R.I.P Robert Mugabe
 
Leo September 6, 2019 rais wa zamani Robert Mugabe amefariki dunia. Mmoja wa wana familia amethibitisha kuwa mzee baba amefariki akiwa na umri wa miaka 95. Sisi na wa mwenyezimungu na kwake tutarejea. Kila nafsi itaonja umauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…