TANZIA: Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe afariki dunia nchini Singapore alikokuwa anapatiwa matibabu

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,344
2,000
Jinga kabisa Wewe. Rudi darasani ujifunze maana ya "Mzalendo." "The Butcher of the Zimbabweans" unamwita "Mzalendo!!!?" Tena Kama Rais wetu atahudhuria mazishi yake na kumwita "Comrade" nitajua lao moja!!!

Mkuu nisome vizuri utanielewa, Mimi ni katika wale wasiomkubali huyu jamaa..

Hapo nilipo sema Mzaleno nimeweka alama ya mshangao nikishangaa Mzalendo aliyewahi kuwa Rais wa zimbabwe akaenda kuugulia na kufia Singapore wakati alikuwa ananafasi ya kujenga hospitali bora Zimbabwe na kusomesha madaktari ilihuduma hizo nzuri alizofuata Singapore angezipata hapohapo Zimbabwe..
 
Inferior Complex

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
3,637
2,000
Nimeshtuka na kifo chake..
Huyu jamaa nilikuwa namkubali sanaaa..kifo chake kimeniuma mnoooo
Habari za hivi Punde zikiripotiwa na Shirika la habari la Uingereza BBC, ni Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefariki Dunia akiwa na miaka 95.

Habari zaidi zinakuja.

President Emmerson Mnangagwa

"It is with the utmost sadness that I announce the passing on of Zimbabwe's founding father and former President, Cde Robert Mugabe.

Cde Mugabe was an icon of liberation, a pan-Africanist who dedicated his life to the emancipation and empowerment of his people. His contribution to the history of our nation and continent will never be forgotten. May his soul rest in eternal peace."
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,429
2,000
R.I.P Comred Mugabe. Aliwahi kusema yeye ni simba anayeongoza jeshi la kondoo barani africa. Kwa maana kwamba viongozi wengi wa africa ni waoga haswa kwa nchi za magharibi.

Pumzika kwa amani.
 
Inferior Complex

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
3,637
2,000
Leo umemsahau unforgettable??

Anyway kifo cha Mugabe
Tutaona unafkki wa watu
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amefariki dunia akiwa na miaka 95 nchini Singapore.

Tangu aondoshwe madarakani na makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa mnamo November 2016 imekuwa nadra sana kuonekana hadharani.

Amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu mwaka wa 1980.

Alikuwa Waziri Mkuu hadi 1987 alipochukua usukani kama rais wa nchi hiyo. Utawala wake umeshutumiwa kwa ukandamizaji wa upinzani, ukiukaji wa sheria za uchaguzi, na kusababisha uchumi wa nchi kuanguka.

Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa unayajua kumhusu kiongozi huyu.

1. Hapendi kushindwa.

Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tenisi, kulingana na aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.

Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.

Yeye ni shabiki wa klabu za Chelsea na Barce

2. Kufufuka.

Kuhusu afya yake, Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,” Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo nimemshinda Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimiza miaka 88.

Ingawa alilelewa katika familia ya Kikatoliki, alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.

3. Shabiki mkubwa sana wa kriketi.

Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni mlezi wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe na nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare

“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”

4. Mazoezi na vyakula vya kienyeji.

Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viungo vya mwili,” Bw Mugabe alisema miaka sita iliyopita. Huwa anaamka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri. Siri nyingine ya maisha yake marefu ni kuwa anapenda sana ‘sadza’ – chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe, na ambacho kina virutubisho vingi muhimu. Vilevile havuti sigara, ingawa hunywa pombe kidogo anapokula chakula cha jioni.

5. Alipata mtoto akiwa miaka 73.

Ana watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.

Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa na umri wa miaka mitatu Mugabe alipokuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.

6. Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley.

Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Mugabe hakumtaka mwimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Mwimbaji, Jim Reeves.

7. Mvaaji wa nguo maridadi.

Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake sawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Huwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake.

8. Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake.

Bw Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.

Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri.

Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru; Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.

9. Ni mtu mwenye shahada nyingi.

Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini. Alisomea shahada zake nyingine kupitia mtandao akiwa gerezani.

Shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
 
goggles

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,421

10. Alimwambia balack Obama kuwa kama anataka nchi ya zimbabwe ikubaliane na ndoa ya jinsia moja basi yeye amuoe Balack Obama.

R.I.P Robert Mugabe
 
Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
719
1,000
Leo September 6, 2019 rais wa zamani Robert Mugabe amefariki dunia. Mmoja wa wana familia amethibitisha kuwa mzee baba amefariki akiwa na umri wa miaka 95. Sisi na wa mwenyezimungu na kwake tutarejea. Kila nafsi itaonja umauti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom