Tanzia: Pole mwanamziki Hashim Dogo kwa kuondokewa na baba yako

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,639
29,512
Yule mwanamziki nguli wa Hip Hop wa miaka ile mwenye jina hapo juu ameondokewa na baba yake profesa rubanza siku ya juzi na amezikwa jana. Mungu ametoa na kwake amerudi jina lake lihimidiwe
 
Hashim dogo, dogo mwendawazimu mzee wa shadow in the darkness pole sana kwa msiba wa pop dee!
"Wanataka kumega deal juu ya bega la msawahili ni vema kuwasitiri? Au tufanye ukatili" by Hashim dogo kwenye track Tunasonga.
 
We kama wewe unamjua ni wewe Heeee we kila mtu hapa bongo unamjua kwendraaa simjui simjui simjui imekuuma, narudia tena simjui mxyuuuu

Hivi vitu viko wazi, kama vazi la kahaba,
Nasambaza maradhi, halafu nakupa Siku 7,
Machozi ni haba, Uokozi ni Njozi baba,
Ulimwengu wa Saba, Jehanam ya aina yake,

Kipe kitu kikupe, kikutupe kupe akikunyonya damu kwa hamu,
Kama hujafaham, DOGO mwanaharam,
Kalam inamwaga damu,

Nakuacha mweupe ka' mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula hongo,

Hivi hii ni Serikali,
Au Sera Kali kwa mbali,
Au sera za mali,

Ni ipi, tafakari, nakufa kiume,
Tunapokwenda pana Zali,
Vichaa wangu walume wananyaka hiyo hali,

Tujitume, Pesa tuchume, kwa mwezi tudake,
Utake usitake, kila mjuba sasa kivyake mifuko itune,
Kama hujipendi njoo nichune, wabongo roho ziume,

Kama hufiki, usijikune,
Hivi inatiki,
Kila siku ya wiki,
Ikipata karatasi, wino hutoka kwa kasi,
Basi nina wasiwasi, kwa haya nawahasi,


Kiu ya Jicho, ulicho nacho ndicho ulicho,
Bongo ni Kama ficho, ya huwezi huchezi na anga,
Tokea '78 wabongo wamefunga mkanda!!
 
Lkn kwa wale real hip hop funs ni ngumu kutomjua though ila poa sio wote lazma tuwe washabiki wa nyimbo hizo
Asiyejulikana na watoto wa dot.com au watu waliotoka Sitimbi miaka us juz juz...... Miongon mwa waanzilishi wa kikosi!! Solo thang anamjua vizuri..
In those days hip hop ilikuwa hip hop sio sasa hivi wamebaki rappers tu
Ni nguli kwa real hip hop wanaofuatilia hip hop toka ktambo ambao n wachache sana. Wanaojiita wanahiphop cku hiz wana mjua joh makin na ney wa mitego tu. Mfano mdogo leo hii unaweza miongon mwa ma emc ninao wakubal n nash mc. Ila kuna watu hawamjui na mtu anaweza kukuuliza ndio msanii gan huyo mbona cmuji. Sasa ikiwa hata mtu km nash hafahamik na baadh ya watu vp kuhusu dogo. Ili uweze kumjua dogo lzma uwe mfuatiliaji wa under ground king emcz
 
Come down shem, hili nguli ndo mwanzilishi haswa wa block 41 na pia alishawai mteka msafiri kondo a.k.a traveller kabla ya kuja kugundua wana kaundugu flani
Nmekuelewa shem msafiri nampata ndio solo Thang, huyo mwingine labda alianza mziki kabla sijazaliwa simjui kabisa hebu tupia kapicha labda ntampata
 
Nmekuelewa shem msafiri nampata ndio solo Thang, huyo mwingine labda alianza mziki kabla sijazaliwa simjui kabisa hebu tupia kapicha labda ntampata
aah kumbe wewe mbichi mbichi mie nilikuwa nadhani ni mdada mkubwa tu basi kuanzia leo sikuogopi
 
Asiyejulikana na watoto wa dot.com au watu waliotoka Sitimbi miaka us juz juz...... Miongon mwa waanzilishi wa kikosi!! Solo thang anamjua vizuri..
In those days hip hop ilikuwa hip hop sio sasa hivi wamebaki rappers tu
Yeah,
Hawa wa siku hizi hata Imam Abas (Muokozi wa Mitaa ya Kati) hawamjui. Ukiwaaambia hata baggzy mallone, kibacha (KBC), Chief Rhymson (zavara), Zomba, D-Rob wote hawa wa KU Crew hawatakuambia hawaajui
 
Back
Top Bottom