TANZIA: Padre Afariki Dunia Zanzibar

semtema

Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
52
Reaction score
13
Padri anaetambulika kwa jina la PETER MINJA amefariki dunia jana kwa matatizo ya presha ya mda mrefu na kupelekea damu kuganda katika mzunguko wake wa ubongo. imeelezwa kua hakuna uhusiano wowote wa tukio la juzi la risasi na kifo cha Padre Peter Minja.

Ibaada ya mazishi itafanyika kesho katika kanisa la parokia ya Mpendae saa nne asubuhi na kuzikwa Kitope.

Bana Ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe. AMEN
 
Unamaanisha Fr. Peter Claver Minja? rip ny dear tutakumiss sana waumini ndugu na jamaa zako.
 
RIP Fr. Minja...Ni msaidizi wa aliyepigwa Risasi Fr. Mkenda...Poleni sana wana Mpendae kwa wakati mgumu mnaokabiliana nao.
 

source ya habari yako ni ipi?! anyways, RIP
 
Mwanga wa milele umwangazie ee bwana.
 
Mwanga wa milele umuangazie eeh bwana apumzike kwa Amani.
Pole waumini wote ,ndugu jamaa na marafiki
 
Mi nilizani yule aliyepigwa risasi au wameua mwingine.Anyway iswe tabu R.I.P father
 
semtema hatuwezi kusema hakuna uhusiano wowote wa tukio la juzi la risasi na kifo cha Peter Minja kwani kwa vyovyote ni lazima alishtuka.

 
Last edited by a moderator:
Mgonjwa wa shinikizo la damu kwa muda mrefu halafu unaambiwa mwenzako kapigwa risasi kwa nini usishtuke mpaka kifo? Kwa hali yoyote hicho kifo kinahusiana na tukio la mwenzie kupigwa risasi. R.I.P Fr. Minja. Poleni waumini.
 
huenda ikawa sababu Kama alikua jirani na eneo la tukio la risasi
 
Immediate cause ni ile risasi he was shocked and thought may be he was the next target. R.I.P Fr. Minja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…