Tanzia: Mzee Rochus Matipa wa RTD afariki dunia

baba koku

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
345
225
Nimepata taarifa za uhakika kabisa kuwa mtangazaji na mwandishi wa habari mkongwe wa RTD tangu miaka ya 1970 na baadae Radio One na ITV kwenye miaka ya 1990 Mzee Rochus Matipa amefariki dunia jana saa tano asubuhi huko mjini Mpanda, mkoani Katavi. Mipango ya mazishi inafanyika huko huko Mpanda.

R.I.P Mzee Matipa tutakukumbuka kwa sauti yako nzuri hususani wakati wa kusoma news bulletin ya kingereza.
 

baba koku

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
345
225
Wakongwe wa News Room ya TBC kwa maana ya Tanganyika Broadcasting Corporation na baadae RTD waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Mzee Matipa, Kimwaga, Agoro Andulu,Ben Kiko,John Mndolwa, Shida Msangeni,Vicky Khatib,Ernest Zullu,Marco Mutaya, Mudimu na wengineo. Wote tunawakumbuka daima mlitekeleza wajibu wenu kwa jamii.
 

baba koku

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
345
225
Pia na mzee Christopher Magola aliyefariki mapema mwaka huu. Yeye alikuwa bado kazini ITV. RIP mzee Magolla
 

moudgulf

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
83,239
2,000
Rip mzee matipa. tunaikumbuka sauti yako nzito kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom