..r.i.p Mzee Patrick Sylverius Qorro[koro].
..kama sijakosea aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa vijana TANU, na waziri mdogo ktk serikali ya Mwalimu Nyerere.
..baadaye alipata kutumikia kama Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Breweries, na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kiwanda cha Sigara. wakati huo mashirika hayo yalikuwa mali ya umma.
..alikuwa mtu muadilifu sana, mchapakazi, kiongozi mfuatiliaji na results oriented, aliyeheshimu wakubwa na wadogo.
..aliyaacha mashirika ya breweries na sigara yakiwa ktk afya nzuri, kwa maana ya uzalishaji, mafao na nafasi za kujiendeleza kwa wafanyakazi. moja ya miradi ninayoikumbuka kuachwa na Mzee Qorro pale breweries ni zile nyumba za wafanyakazi pale Buguruni.
..Patrick Qorro alikuwa mtu aliyependa kujiendeleza kielimu. alichukua shahada ya MBA pale udsm akiwa tayari ni mwenyekiti mtendaji wa Tanzania Breweries.
..zaidi ya hayo alikuwa kiongozi mpenda MICHEZO. wakati wa uongozi wake timu za mpira wa miguu za Breweries na Sigara zilipanda daraja na kucheza ktk ligi kuu. kama mtakumbuka enzi za akina Jamhuri Kihwelu, Yassin Abuu Napili, etc etc.
..bungeni alikuwa ni mbunge mwenye msimamo usioyumba ktk kutetea maslahi ya nchi. namkumbuka akiwa mbunge aliandika hoja binafsi kupinga uchafuzi wa mazingira ktk mbuga zetu za wanyama.
..nje ya majukumu yake ya kiserikali na kisiasa, Mzee Qorro alikuwa mtu mwuungana, mnyenyekevu, na mwenye msaada kwa wenzake.
NB:
..kama sijakosea Mzee Patrick Qorro aliwahi kuomba radhi kwa wapiga kura wa Karatu kutokana na kauli tata aliyoitoa ktk mkutano wa kampeni ambao ulihudhuriwa na makamu wa raisi Dr.Omar Ali Juma[r.i.p].