Tanzia: Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Tambuka Reli, afariki Dunia

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Tambuka reli,kata ya Kalangalala mjini Geita kamanda AMOS MASANJA amefariki Dunia kwa kugongwa na gari juzi na mazishi yamefanyika jana jioni.

Bwana AMOSI MASANJA atakumbukwa kwa mambo mengi na mazuri aliyoyafanya ndani ya chama kiwa ni pamoja na kuendesha kampeni za nguvu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwezesha CHADEMA kushinda udiwani wa kata ya Kalangalala chini ya PETER DONARLD N'GWENESHO ambaye aliwaongoza makamanda kwenye mazishi akiwemo Mbunge kivuli CHADEMA na katibu wa wilaya ya Geita Kamanda Rogers Ruhega,mjumbe wa kanda ya ziwa magharibi kamanda DAUD NTINONU na wengineo.

RIP Kamanda.
 
Badilisha heading hiyo usiwe kama magazeti ya udaku eti kumbe nyerere alishawahi kumpapasa amina chifupa kumbe ndani ukisoma wanamaanisha alimshika kichwani
 
Mkuu mpaka mmezika ndio unaleta uzi? any way Poleni wafiwa,
R.I.P Kamanda!!
 
Du lsije ikawa lile gari lililosababisha ajari liliendeshwa na Mwigulu. RIP kamanda
 
Badilisha heading hiyo usiwe kama magazeti ya udaku eti kumbe nyerere alishawahi kumpapasa amina chifupa kumbe ndani ukisoma wanamaanisha alimshika kichwani

Sijakuelewa mkuu...hebu funguka zaidi...kwangu naona heading na kilichomo ndani ya habari havipishani
 
nilifungua hapa nikafikiri ni yule jamaa BILLCANAS
Kwa sababu ndicho unachokiombea kitokee. MUNGU ni mkubwa atamlinda na mabaya yote hasa katika kipindi hiki ambacho yeye na wale wapambanaji na wenzake kule Dodoma tunawahitaji sana.
 
Naona wewe ndo mwenye ukoma...kama uko sawa unge sajesti heading iwe vipi

Mwenyekiti wa Chadema ni Mbowe. Bora ungesema Chadema yapata pigo au mwenyekiti wa tawi CDM afariki. Ukisahihishwa usifoke.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Title yako inasumbua vichwa vya watu sawa na title ifuatayo: Rais atachia ngazi baada ya uchaguzi wa Oktoba. Title hii ilitakiwa iwe:Rais wa TFF ataachia ngazi baada ya uchaguzi wa Oktoba.
 
Mwenyekiti wa cdm tawi la Tambuka reli,kata ya Kalangalala mjini Geita kamanda AMOS MASANJA...amefariki Dunia kwa kugongwa na gari juzi na mazishi yamefanyika jana jioni...kamanda AMOSI MASANJA atakumbukwa kwa mambo mengi na mazuri aliyoyafanya ndani ya chama...ikiwa nipamoja na kuendesha kampeni za nguvu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwezesha cdm kushinda udiwani wa kata ya Kalangalala chini ya kamanda PETER DONARLD N'GWENESHO...ambaye aliwaongoza makamanda kwenye mazishi...akiwemo Mbunge kivuli na katibu wa cdm wilaya ya Geita Kamanda Rogers Ruhega,mjumbe wa kanda ya ziwa magharibi kamanda DAUD NTINONU na wengineo.RIP Kamanda.

Poleni sana wana Geita kwa msiba huo, tumwombee apokelewe kwa amani huko aliko nasi aliotuacha tuendeleze mapambano mpaka Magamba yasahaulike
 
Back
Top Bottom