TANZIA: Mwanamuziki Mkongwe Shaban Dede amefariki dunia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Hizi ni habari mbaya kwa mashabiki wa Msondo Ngoma Music Band, Mwimbaji na mtunzi tegemeo wa bendi hiyo Shaaban Dede amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

=====

Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo Alhamis Julai 6,2017 saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha.

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi maiti yamemkuta.


Chanzo-Michuzi blog
 
Mwanamuziki mkongwe, Shaaban Dede amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar alikokuwa akipatiwa matibabu.

DECCVP9W0AAv8Me.jpg
 
duuh,kizazi chao ndio kinapukutika,A.M.P.P(alale mahali pema peponi)
 
Back
Top Bottom