damnz
Member
- Feb 25, 2016
- 15
- 95
Ipatapo jana mida ya saa 9 jioni nilipata meseji ikisema kwamba kuna mwanafunzi kakapotea ni mwaka wa kwanza kozi ya irrigation engineering-SUA,wenzako wanaekaa nae room walisema kwamba mwenzao alikuwa ni mgonjwa hivyo siku hiyo aliondoka tangu asubuhi na laiacha simu yake ndani na wakidhani ameenda sehemu ya karibu,hadi kufikia mida ya jioni alikuwa hajarudi.
Leo mida ya mchana huu nimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa hostel zao Mr.hatibu Kilenga ambae amesema kwamba;
"Kwa masikitiko makubwa napenda kuwajulisha ndugu wana SUA wanafunzi wote ,waafanyakazi na watu wote kwamba leo asubuhi majira ya saa tano asubuhi baada ya heka heka za kumtafuta ndugu yetu YEREMIA MBENDULE,hatimae tumemkuta katika pori la uwanja wa SUA akiwa tayari amefariki dunia,tukiwa na polisi tunampeleka marehemu hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa taratibu nyingine.
Namshukuru Rais wa chuo Mr. Ndunguru,makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mr. Salim na wanafunzi wote kwa ujumla kwa jitihada za kumtafuta mpendwa wetu"
Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!AMEN
Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza kozi ya Bsc.irrigation and resource engineering na Jumatatu alikuwa anajiandaa kuanza mtihani wake wa mwiho wa muhula.