TANZIA: Katibu wa mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Christopher Mwamsibu afariki dunia

BETTY MSIGWA

Member
Aug 8, 2016
43
36
Mbeya.jpg
Buriani Katibu wa Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Christopher Mwamsibu aliyefariki Leo hospitali ya Ikonda Makete alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kila nafsi itaonja mauti.
=======

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupitia Chadema amepata pigo baada ya katibu wake, Christopher Mwamsiku kufariki dunia alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ikonda Wilayani Makete mkoani Njombe.

Akizungumza kwa njia ya simu Sugu alisema kifo cha katibu wake ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kampeni zake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni pigo kwake na chama kwa ujumla.

‘’Daah!! Kaka (mwandishi), nimepata pigo kubwa sana, nimepoteza moja ya nguzo yangu kubwa na chama kwa ujumla na kwa mara ya mwisho nimeongea kwa njia ya simu jana usiku kwa kirefu, akiniamba kwa sasa anajisikia vizuri, tukaagana vizuri tu. Leo alfajiri nimepigiwa simu naambiwa kwamba ametutoka. inaniuma sana,” alisema Sugu.

CHANZO: Mwananchi
 
BURIANI KATIBU WA MBUNGE JOSEPH MBILINYI
....Buriani Katibu Wa Mbunge Jimbo La Mbeya Mjini Christopher Mwamsibu Aliyefariki Leo Hospitali Ya Ikonda Makete Alikokuwa Akipatiwa Matibabu...... Kila Nafsi Itaonja Mauti.....
Amekufa kwa ugonjwa gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom