Tanzia: Diwani afariki dunia Igunga

Tanzia: Diwani afariki dunia Igunga

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
344
Reaction score
306
Diwani wa kata ya Nanga wilaya ya Igunga, Ramoti Mapalala amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Noah,

Taarifa za kuaminika zilizomfikia mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu kutoka kwa Ocd wa Igunga Maige zinaeleza kuwa diwani huyo akiwa na piki piki yake aliingia barabarani ghafla akiwa anatoka Nanga kuelekea barabara kuu ya Igunga Nzega pasipo kuchukua tahadhari na kwa bahati mbaya gari hilo likamgonga na kufariki papo hapo

Kwa sasa askari wa jeshi la Polisi wanashughulikia utaratibu wa kuuondoa mwili barabarani
 
Diwani wa chama gani nijiandae kutuma rambi rambi
 
Diwani wa chama gani nijiandae kutuma rambi rambi

Wewe tuma tu hiyo rambirambi, huyo ni mtanzania mwenzako aliyejitolea kuwatumikia watanzania. Tuma kwa mkuu wa wilaya yake ama kwa mbunge wake zitafika tu. RIP Diwani Mapalala
 
Wewe tuma tu hiyo rambirambi, huyo ni mtanzania mwenzako aliyejitolea kuwatumikia watanzania. Tuma kwa mkuu wa wilaya yake ama kwa mbunge wake zitafika tu. RIP Diwani Mapalala

Mkuu Lyimo rambi rambi sio pesa tu hata maneno ya kufariji pia yanafaa kwa wakati huu
 
Kama ana mtoto mkubwa basi ajiandae kurithi udiwani wa babaye! ccm ni chama chenye huruma,kitamfuta machozi kwa kumpa huo udiwani!!
 
ha ha ha nimecheka sana hii ni sera mpya wa CCM. Vigogo wakae chonjo watoto wao watawamaliza ili wachukue nafasi zao.

Hakina kwa utaratibu waliouanzisha ccm wataujutia,
rip diwani.
 
ina maana rambirambi za ssmu ni kupitisha jina la mtoto au mjukuu kugombea kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom