"NIKIRIPOTI KUTOKA KANDA YA KATI MKOANI DODOMA,MIMI NI BEN KIKOO WA RTD"...
Itaendelea kubaki sauti tamu zaidi kuwahi kusikiwa na masikio yangu katika Radio za hapa nchini!
Sauti ambayo haikumfanya msikilizaji achoke kuisikiliza..ni sauti yenye Mamlaka na sauti yenye Mvuto.
Sauti ambayo ikisikika tu basi tunafahamu huyu ni Ben Kiko,kinyume na sasa watangazaji wengi wanaigana kila kitu kiasi ni ngumu kumtofautisha yule wa Mawingu Radio na hata ile Radio ya Wakati...swaga zile zile
"ama niniiii"
"aje aje jombaaa"
NI UJINGA....
R.I.P BEN KIKO
Nyuma yako mbele yetu umeacha tasnia ya habari ikizidi kupoteza mvuto kila siku,waandishi makanjanja wanazidi uwingi wa wale wenye weledi.
Umeondoka KIKO ukiacha ma PRESENTER ni wengi zaidi kwasasa kuliko WANAHABARI..
Umeondoka ukiacha watu wanaojiita waandishi wa habari wa sasa hawajui hata bei ya gazeti, hawajaui hata majina ya mawaziri wao, hawajui hata idadi ya mikoa yao...yan hawajui tu!! Hata huo muziki wanaoutaka bado hawaujui.
Kuna wakati natamani ningekuwa MWANAHABARI katika kipindi chenu.
Kapumzike KIKO.!!