TANZIA: Aliyekuwa mpiga picha wa magazeti ya Nipashe na Standard News Papers Limited, Athuman Hamis afariki

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mpiga picha Mwandamizi ambaye aliwahi kufanya kazi katika magazeti ya Nipashe na Tanzania Standard News Papers Limited, Athumani Hamisi amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.


26229624_2235234946490911_5476783752590814276_n.jpg


Chanzo: EATV
 
Wanabodi,

Nimepokea taarifa hii ya msiba kwa mshtuko na masikitiko, Mwandishi wa habari, na mpiga picha Athumani Hamisi, Amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili.

Taarifa Zaidi zitafuatia.

RIP Athumani Hamisi.
Rejea
Mpiganaji Athumani Hamisi Apata Mapokezi ya Kishujaa.
Msaada kwa Athuman Hamis | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua ...
Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua ...

Nilimtembelea akiwa hospitalini Afrika ya Kusini
athumani hamisi na paschal mayala mambo mswano
mpiganaji athumani hamisi akila tizi kwenye kituo cha Medcare jijini Johannesburg iliyo karibu na makao makuu ya shirika la utangazaji la sauzi SABC
Athumani+Hamisi+na+Pascal+Mayalla..jpg


wapiganaji athumani hamisi na paschal mayala wakiwa hospitali ya medcare leo. wote wapo hapo kwa matibabu kufuatia ajali walizopata nyakati tofauti Mpigapicha wa Magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi aliyelazwa Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini kwa takriban miezi mitatu, ameishatoka katika hospitali hiyo kufuatia afya yake kuendelea vizuri ambapo sasa hapo amehamishiwa hospitali nyingine ya Medcare mahsusi kwa mazoezi ya viungo. Mwandishi wa PPR aliyemtembelea Athumani Hamisi hospitalini hapo, alimshuhudia akifanya mazoezi ya viungo ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kusimama kwa kwa msaada wa mashine maalum. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Athumani Hamisi amesema anaendelea vizuri ila amewaomba Watanzania wazidi kumuombea. Ametoa shukrani za dhati kwa Rais Kikwete aliyemtembelea mara mbili, pia anaishukuru serikali na mwajiri wake kwa huduma zote anazopata ukiwemo ujumbe mahsusi toka Deily News ambao humtembelea kila mwezi. Pia anaishukuru sana familia yake akiwemo mchumba wake aliyeko Nchini Marekani kwa jitihada zao kwake katika kipindi chote tangu kuugua kwake.
 
IMG_20180104_180746.jpg

Nyumbani kwa Athumani Hamisi Sinza Madukani,
Kutoka kulia, Muhidin Michuzi, alifanya kazi na Athumani Hamisi Daily News, Tuma Abdalah News Editor, Daily News, Dr. Jimmy Yonazi, Managing Editor, Daily News, Dr. Msengi, Kaka wa marehemu, Isaac Mruma, alikuwa ME Daily News.
Picha na Pasco Mayalla
Paskali
 
IMG_20180104_184749.jpg
IMG_0360-2.jpg

Kama kawaida yake Mtu wa Watu, Mzee wa Msoga, rais Mstaafu, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwepo.

Paskali
 
Mpiganaji Athumani Hamisi, aliyefariki jana asubuhi, amepumzishwa leo katika makao yake ya milele, kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Rais Mtaafu, mtu wa watu, Dr. Mrisho Kikwete, ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi hayo ambapo serikali iliwakilishwa na Waziri wa Habari, Dr. Harison Mwakyembe, na kundi mkubwa kabisa la wanahabari wapiga picha za magazeti, kuwahi kutokea.
Mwili wa Athumani Hamisi Msengi kumaliza ukiwa nyumbani kwake mara baada kuswaliwa Sinza Madukani.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.Jim James Yonas akizungumza jambo mara baada ya mwili wa Athumani Hamisi Msengi kumaliza kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadj Mussa Salum akizungumza jambo nyumbani kwa marehemu leo jijini Dar es Salaam

Kaka mkubwa wa marehemu Dkt Ibrahim Msengi akizungumza jambo mara baada ya mwili wa mdogo wake Athumani Hamisi Msengi kumaliza kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.

Mwili wa Athumani Hamisi Msengi kumaliza ukipandishwa kwenye gari kuelekea kwenye makaburi ya Kisutu mara baada ya kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.






RIP Athumani Hamisi, pumzika kwa amani, Amen.

Paskali
 
Back
Top Bottom