TANZIA: Abbas Dilunga afariki dunia, alikuwa mchezaji pekee wa Tanzania kucheza team ya All African Stars

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,682
3,065
Mchezaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars Abbas Dilunga amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake, Chanika, Dar es Salaam.

Maziko ya gwiji huyo ambaye ndiye baba mzazi wa mchezaji wa Ruvu Shooting, Said Dilunga, yanafanyika leo saa 10 jioni Kisarawe mkoani Pwani.

Akitoa taarifa ya msiba huo kwa niaba ya familia, Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema marehemu ameacha wajane wanne na watoto 13.

Inna lillah wa inna ilayh rajiu'n.
 
Huyu itakuwa ana undugu na yule Dilunga mwandishi aliyekufa juzi kwani?

May his soul rest in peace. Eimen.
 
Masau Bwire bwana! aki report issue zake mie hooooiiiii
RIP mzee wetu Dilunga
 
R.I.P Abbas Dilunga? Hivi Wale kina Hassan Dilunga (simba) na Saidi Dilunga ( Ruvu Shooting) in ndugu?
Said Dilunga ndo amefiwa na babake...halafu yule wa Simba anaitwa Hassan saleh Dilunga ...huenda n majina ya ukoo tu ...
 
Msiwe waongo Maulidi Dilunga, Omari Mahadhi ndiyo walichaguliwa timu ya Afrika na kuna mwingine wa tatu nitawajuza!
Mbona watz mnapenda KUDANGANYA??
 
Back
Top Bottom