Tanzanite ya Arusha, yainufaisha Bahama kupindukia

Wewe kama una takwimu za kuonyesha kwamba nilichoandika si kweli kwa nini usiweke takwimu za kuonyesha kile nilichoandika si kweli!? Naona unabwabwaja bila kujua usemacho. Kutetea maslahi ya nchi yetu hata siku moja haiwezi kuonekana ni uhasidi/wivu kwa mtu mwenye akili timamu.

Kama kutetea maslahi ya nchi ni uhasidi basi hakukuwa na haja katika hiyo inayoitwa "mining act" iliyopitishwa hivi karibuni kuzuia usafirishaji wa Tanzanite ambazo hazijasafishwa ili kuliwewezesha Taifa lisafishe Tanzanite hizo nchini ama kwa kupitia wafanyabiasha ambao watakuwa tayari kusafisha Tanzanite. Hii itasaidia katika kuongeza ajira nchini na pia pato la Taifa kwanza kwa kupata kodi toka kwa watakaojiriwa katika makampuni ya usafishaji wa tanzanite na makampuni hayo pia kulipa kodi na wakati huo huo kuiuza Tanzanite ambayo imeshasafishwa katika nchi mbali mbali duniani kwa bei ya juu ukilinganisha na bei ya tanzanite ambayo haijasafishwa.


Wekeni takwimu hapa sio mazungumzo ya mitaani tu. Pia kumbuka kuna kitu kinaitwa value addition hao wanaopata zaidi wamechukua hii mali ghafi wakaifua vizuri na kuimarket inavyo stahili - kwa hiyo wanastahili faida kulingana na juhudi yao. Tatizo letu ni wivu na uhasidi - hivi ndio vinatufanya tulivyo !!
 
Ni kweli hizo nchi zilitajwa pamoja na afrika kusin canada na australia zinauza tanzanite kwa bei rahis kuliko bei inayouzwa nchini kwetu kwa sisi wadau wa tanzanite soko limeharibika sana kwani watalii kutokaka hizo nchi tayari washafanya manunuzi kwenye nchi zao tena kwa nusu bei. Huku kwetu upatikanaji ni mgumu na bei ni juu sana

Hivi kweli Mkuu MLERAI hii inawezekana? 'Tena kwa nusu bei' vigumu kuamini.
 
Last edited by a moderator:
Nimestaajabia kuona Bahama, ikiwa imejazwa maduka makubwa kwa madogo ya Tanzanite, mengi ya maduka niliyoyashuhudia pale Nasau na hata Free Port yamejazwa madini safi ya Tanzanite katika ukubwa tofauti na kwa wingi, huku yakiuzwa kwa gharama kubwa kupindukia.
Unaweza bisha lakini amini madini yetu yanayochimbwa hapo Arusha ndio yanayoendesha uchumi wa bahama
The Hunter, si kwamba nimeshtuka sana ila tu nimemkumbuka Prof. wangu kutoka Trinidad&Tobago (University of West Indies)aliwahi kunionesha vito hivyo vya thamani kubwa, kama kilogram 6 alizonunua, na kwenda kukata katika carat ndogondogo kama 1-7 na kuviuza huko Trini na St Navis &Kitts...leo hii si yule tena na alikuja nchini kupitia mkutano wa "International Trade Conference" Naamini ni Kweli unayoyasema.
 
Back
Top Bottom