Tanzanian child prodigies...

epigenetics

JF-Expert Member
May 25, 2008
269
80
Hivi Tanzania kuna 'child prodigies' (watoto/vijana wenye upeo mkubwa kiakili usiolingana na umri wao) ambao wameweza kuwika katika anga mbali mbali ukubwani?

Je, kuna program zozote zilizopo nchini zinazo 'aim' kutunza vipaji vya watoto kama hao?

mf....
Terence Tao

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Terence_Tao[/ame]


Huyu kijana sasa ni Professa wa Hisabati pale UCLA. Dogo alijifundisha hesabu akiwa na umri wa miaka 2, na alianza kuchukua kozi za Hisabati za level ya chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 9.

Una stori za watu kama hawa uliowahi kusoma nao?
 
Mimi binafsi nilisoma na dada fulani jina Eliza, sekondari. Alikuwa haandiki notsi, wala hasomi baada ya vipindi. Yeye ni darasani kusikiliza tu! Muda wote yupo akijisomea Novels. Style yake ilikuwa ni kusubiri pepa na kusoma vitabu vya somo siku moja kabla ya mtihani. Kwa staili hii aligonga point 7 fom foo. Miaka ya tisini mwanzoni. Sijui aliishia wapi.....
 
Back
Top Bottom