Golden Age
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 203
- 45
TANZANIA YETU
IMMORTAL TECHNIQUE
(THE 3 rd WORLD)
Ukitazama kwa undani utagundua Tanzania ni nchi ambayo haijapiga hatua kubwa za kimaendeleo katika siasa ,demokrasia,uchumi,teknolojia,elimu,miundombinu pamoja na nyanja nyingine nyingi.
Mchungaji Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya chama chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) aliwahi kusikika bungeni akisema" ukienda kwenye elimu ni matatizo,ukienda kwenye kilimo ni matatizo,ukienda kwenye afya ni matatizo ,mwaka baada ya mwaka ni matatizo yaleyale why can't we think a little bit more.....".
Pia siasa za Tanzania kidogo zipo tofauti,katika kampeni za uraisi,udiwani na ubunge wagombea wa hizi nafasi Mara nyingi sana huwa wanapanda jukwaani ambapo jukwaa linaweza kuwa kwenye uwanja wa Mpira au sokoni au sehemu yeyote ya wazi na baada ya hapo wagombea wetu huwa wanatoa sera zao baada ya hapo uchaguzi unafanyika na mchezo unakua umekwisha.
Kwa nchi zilizopiga hatua kubwa za kimaendeleo katika siasa wao nao wana utaratibu tofauti,wao huwa wanafanya midahalo na kupitia midahalo hiyo huwa tunashuhudia wagombea wanavyoshindana kwa hoja zenye mashiko tofauti kabisa na hapa Tanzania.
Pia mchungaji Msigwa aliwahi kuzungumzia bungeni kuhusu uwezo wa baadhi ya wabunge katika kujenga hoja na kutoa mawazo ambayo yatalisaidia taifa kusonga mbele ambapo alinukuliwa akisema" akichangia profesa hapa hana tofauti na mtu wa darasa la pili,huwezi kutofautisha mtu kwenye masters na mtu wa darasa la pili where are we taking this nation.... ".
Pia mchungaji Msigwa akaenda mbali zaidi kwa kusema bunge ni sehemu ya kutatua matatizo na sio kutengeneza matatizo kwa hiyo kunahitajika kuwe na mchango wa mawazo mazuri kutoka kwa wabunge ili kuokoa taifa.
Pia mchungaji Msigwa anaamini maendeleo yanakuja baada ya watu kupingana mawazo ili kupata mawazo mapya na kwamba katika jamii ambayo watu wote wanafikiri kwa namna moja basi jamii hiyo itakua imekufa ambapo aliwahi kunukuliwa bungeni akisema" maendeleo duniani yamekuja kwa kua na mawazo tofauti yanayopingana,badala ya kutuzomea mtusikilize huu ndio wajibu wetu...."
Pia mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kupitia tiketi ya chama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Joseph Mbilinyi nae pia anaamini demokrasia na maendeleo ni vitu ambavyo vinatembea katika njia moja na kwamba bila demokrasia ni vigumu Tanzania kupata maendeleo, aliwahi kunukuliwa bungeni akisema "hatuwezi kupata maendeleo bila demokrasia hatuwezi kujadili maendeleo bila demokrasia, bila utulivu wa kisiasa kwenye nchi......hatuwezi kujadili maendeleo bila uhuru wa vyombo vya habari,wanafungia magazeti kiholela tu,wanazuia wananchi wasiangalie bunge kwenye TV.......".
Pia Raisi wa awamu ya tano Mheshimiwa Dk.John Pombe Magufuli aliwahi kunukuliwa akisema " Tanzania hii ilikua shamba la bibi,watu walikua wanafanya ya hovyo,ninaposema ya hovyo ni ya hovyo kweli,mimi nipo serikalini,lakini nimekua serikalini kwa miaka ishirini....mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama, ukikosa madawa hospitalini,hata ukiwa chadema utakosa,hata ukiwa ccm unaimba kila siku ccm oyeee utakosa tu madawa...".
Watu wengi wamekua wakitoa malalamiko kwa uongozi,hata mkuu wetu wa kaya nae tunaona katika nukuu hapo juu amesema kwamba mambo ya hovyo yalifanyika serikalini kwelikweeli yaani sio kitoto.
Pia inasemekana kwamba ikitokea kuna kiongozi mzuri ambae anasimamia katika haki na kutimiza majukumu yake ipasavyo,basi huwa anapingwa na kufanyiwa fitina,kwamba anaonekana kama mnoko hivi.
Wana HipHop nao kupitia kazi zao za kisanaa wamekua wakielezea uhalisia kuhusu Tanzania,Nikki mbishi amewahi kusikika akichana " wezi wa rasilimali za serikali wapo free".Pia anaendelea akichana " nchi ambayo falsafa hazina tafsiri/kwenye shule ya kata hakuna mtoto wa waziri".Hizi shule za kata zimekua zikipigiwa kelele sana kwamba hazijakidhi vigezo vya utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi ikiwemo ukosefu wa walimu,vitendea kazi,maabara pamoja na madawati.
One incredible pia katika wimbo wake unaoitwa " kesho yetu" kutoka katika santuri ya soga za mzawa alisikika akichana " watoto watapendaje elimu na shule wanakaa chini".Pia one incredible kwa kutumia lugha ya kificho alituhabarisha kwanba kuna tatizo kwenye uongozi ambapo alisikika akichana" haya maisha ni safari ili hili gari ni bovu/hii hali hatari sirikali na uovu/dereva ni mkali ilihali kipofu...."
Mbunge wa Singida mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu amewahi pia kuongelea suala la elimu ambapo alisikika akisema "siwezi nikapeleka watoto wangu kwenye shule za kata, mtu yeyote ambae anajali elimu hapeleki mtoto kule na wale ambao wamesema hizo shule zijengwe watoto wao hawasomi hizo shule kabisa,zile shule za kata ni majina tu lakini ukweli wa Mungu hizo sio shule, tatizo la maelfu ya hizo shule ni walimu...".
Pia alisisitiza kwamba serikali haipangi vipaumbele vyake ipasavyo ambapo alinukuliwa akisema " hutakaa usikie bunge limeshindwa kukaa kwa sababu hakuna hela,hutakaa usikie Raisi au Waziri ameacha kusafiri nje kwa sababu hakuna hela,lakini ni kauli za kawaida kabisa kusikia madaktari hawajalipwa mshahara,madawa hakuna,umeme hakuna..."
Pia tukija kwenye uchumi bajeti ya Tanzania imekua ikitegemea misaada ya wafadhili kwa kiasi flani na ukizingatia tayari Tanzania ina ardhi kubwa,watu wengi,bandari,mbuga za wanyama,misitu madini pamoja na gesi.Binafsi nakubali kodi zina mchango katika maendeleo ya kiuchumi,lakini pia rasilimali tulizonazo kama zikitumiki vizuri basi zitakuza uchumi Kwa kiasi kikubwa.
Ukisomasoma vitabu vinavyohusu uchumi utakuta vimeandikwa " a society develops economically as its members increase jointly their capacity for dealing with enviroment,this capacity for dealing with enviroment is dependent on the extent to which they understand the laws of nature (science), on the extent to which they put that understanding into practice by devising tools........" .
Pia utakuta vitabu vimeandikwa " taxes do not produce national wealth and development,wealth has to be produced out of nature,from tilling the land or mining minerals or felling trees or turning raw materials into finished products for human consumption...".Kwa hiyo hapo utagundua kwamba kuna maendeleo makubwa sana ya kiuchumi yatapatikana kama rasilimali tulizonazo zikitumika vizuri.Kalapina nae katika ngoma yake ya fasihi amewahi kusikika akichana " Tanzania!! Tanzania!!!! wawekezaji kila sekta wamevamia/kwenye migodi mbuga na ardhi pia/........."Hili suala la wawekezaji wa kigeni .....itaendelea
Je immortal technique anasemaje kuhusu uhalisia wa nchi za ulimwengu wa tatu ikiwemo Tanzania??????? Basi hakikisha unajipatia nakala yako ya kitabu cha HipHop na Maisha ambacho kitatoka hivi karibuni kwa shilingi za kitanzania elfu tano tu.
Asanteni sana
Naomba kuwasilisha
Imeandikwa na Golden Age Technique
0713 560 346