SoC04 Tanzania yenye mabadiliko na maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
29
11
Tanzania tuitakayo yenye wakazi wenye maisha na maendeleo makubwa ni Tanzania yenye mambo yafuatayo tena yakiwa katika ubora wake.

1. Mfumo bora wa uchaguzi na wenye kuzingatia haki na maendeleo katika jamii ya watu husika, kuwe na mfumo utakaohakikisha kiongozi anatimiza yale aliyoahidi wakati wa kampeni na jamii ionyeshe kujivunia kuwa na kiongozi huyo, sio miaka ya utawala inatimia halafu kiongozi anakuwa amejinufaisha mwenyewe tu na wala hawajibishwi mbaya zaidi anagombea tena.

Screenshot_20240511-091959.png


2. Serikali ihakikishe ina vyombo imara vya kutetea haki za watu nakuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu bila kujari pesa, umaarufu wala cheo. Yeyote aliye na hatia sheria izingatiwe. Hiyo hali ya mtu kupeleke kesi katika vyombo vya sheria anaanza kuzungushwa nakupigwa tarehe ikomeshwe maana watanzania wanaumia.

Screenshot_20240511-092254.png


3. Kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinasimamiwa nakutekelezwa, ili kulinda maisha ya watu. Kasumba ya rushwa huko barabarani ikomeshwe maana kuna traffic wanajari faini na vijipesa badara yakuangalia usalama wa abiria.

Screenshot_20240511-090044.png


4. Serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa katika hali nzuri ya kimazingira na kila Mtanzania anaelimishwa juu ya hilo ili kuondokana na ukataji miti kiholela, magonjwa ya mlipuko na utupaji taka hovyo. Kwa kuipa nguvu sekta husika katika kuhamasisha upandaji miti, usafi wa mazingira na pia kuna sehemu moja ya machimboni huwa inasahaurika sana nawakati tunaona watu wakipoteza maisha kwa kufunikwa na vifusi serikali ilitizame hili pia.

Screenshot_20240507-153602.png


5. Sekta mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama elimu na afya na nyinginezo ziwe na wafanyakazi tosherevu ili kuzifanya ziwe bora nakuleta manufaa makubwa kwa watanzania wote tuondokane na hali yakuwa na uhaba wa wafanyakazi jambo ambalo linaturudisha nyuma kimaendeleo.

Screenshot_20240511-090649.png


6. Wafanya kazi waboreshewe mishahara pale panapostahili ili waweze kuendesha maisha yao vizuri. Mfano kuna walimu wengi kutokana na mishahara yao kuwa haikidhi mahitaji tumekuwa tukiwaona wakitumbukia kwenye shida ya mikopo kausha damu n.k. serikali ilitizame hilo pia wakati wanafunzi wanaongezewa boom wakufunzi wao pia wawe nafuraha ili wafanye kazi kwa bidii bila stress.

Screenshot_20240511-092404.png


7. Kahakikisha bei za bidhaa mbalimbali ikiwemo umeme, gesi, mafuta ya petroli, sukari, dizeli na nyinginezo zinakuwa na utaratibu mzuri ili pale zinapopanda Watanzania wawe wanafahamu sababu nasio ghafla tu mara vitu vinapanda bei katika hali ya sintofahamu.

Screenshot_20240511-091818.png


8. Kuna fursa za ajira za mda mchache hizi wangekuwa wanapewa wale ambao bdo hawajaajiriwa na wana sifa ikiwa ni njia moja wapo itayoweza kuwafanya kupata mitaji yakuwawezesha kujiajiri huko mitaani tena bila hongo eti ndo wapate nafasi TAKUKURU ifanye kazi yake.

Screenshot_20240511-091706.png


9. Kuenderea Kuboresha na kudumisha amani kwa kila mtanzania pamoja na mali zake, kwa kujenga vituo vya polisi maeneo yasiyokuwa na vituo hivyo pia doria ziwe za siku zote sio wakati wa matukio tu na sikukuu, hii itafanya kupungua kwa vitendo vya ukatiri nchini.

MWISHO NAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KWA HATUA KUBWA ZINAZODHIDI KUCHUKULIWA KWAAJILI YA KUHAKIKISHA MAENDELEO YANAPATIKANA NA KUIJENGA NCHI MPYA "HAPO KAZI IENDELEE"
 
u na wala hawajibishwi mbaya zaidi anagombea tena.
Mwananchi kwa kumnyima kura ilipaswa ndio iwe kumuwajibisha kwa kuikosa nafasi. Lakini nibkwa nini anampigia tena anashinda? Hapo ni mbwa kala mbwa: kiongozi hajawajibika ipasavyo na mwananchi naye hajawajibika (Chini ya dhana ya uchaguzi huru na wa haki lakini)

Yeyote aliye na hatia sheria izingatiwe. Hiyo hali ya mtu kupeleke kesi katika vyombo vya sheria anaanza kuzungushwa nakupigwa tarehe ikomeshwe maana watanzania wanaumia.
Sawa sawia chief, wote tunachotaka ni HAKI itendeke. Ndio maana hilo ni lazima liende tu sambamba na kumhukumu mtu kwa kuzingatia ushahidi kamili na nafasi ya kujitetea. Haki.
 
Back
Top Bottom