Tanzania yawakamata 'askari wa Congo' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yawakamata 'askari wa Congo'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maswi, Nov 7, 2011.

 1. Maswi

  Maswi JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 898
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zaidi ya askari 20 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametiwa kizuizini nchini Tanzania kwa kuingia kaskazini -magharibi mwa nchi hiyo kinyume cha sheria, jeshi la Tanzania limesema.

  Walisema walikuwa wakiwafuata waasi kutoka Congo wanaopata matibabu Tanzania, alisema Lt Kanali Emmanuel Mcheri.

  Watu hao wenye silaha kali walikamatwa baada ya kutia nanga karibu na boti ya polisi katika bandari ya Kigoma kwenye ziwa Tanganyika.
  Eneo la mashariki mwa Congo lenye utajiri mkubwa wa madini limegubikwa na makundi ya waasi.
  Lt Kanali Mcheri alisema askari hao, ambao bado wanahojiwa, walikuwa na bunduki, maguruneti, bastola na risasi nyingi.
  Aliiambia BBC Swahili, " Wamevunja usalama wa nchi yetu kwa kuingia nchini kwetu na silaha nzito. Nimeshatoa taarifa kwa viongozi waandamizi serikalini na nasubiri maagizo zaidi."
  Maafisa wa eneo hilo wamekataa kuzungumzia suala hilo.
  Licha ya kuwepo makubaliano ya amani huko Congo mwaka 2002, uliomaliza mapigano mabaya ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka mitano, bado kuna vurugu mashariki mwa nchi hiyo.
  Majeshi ya kutunza amani ya umoja wa mataifa yamekuwa yakiunga mkono juhudi za kupambana na baadhi ya wapiganaji mashariki mwa Congo na kuwahusisha wengine kwenye jeshi la nchi hiyo.
  Takriban wakimbizi 42,000 wa Congo wako Tanzania, wakiwa wamekimbia mapigano mashariki mwa Congo, kulingana na shirika linalowatunza wakimbizi la umoja wa mataifa.
  source BBC BBC Swahili - Habari - Tanzania yawakamata askari wa Congo
   
 2. Maswi

  Maswi JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 898
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jeshi la kongo limesema ni wanajeshi waasi
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  TPDF/JWTZ hawana navy force yaani weupeeeee...watu wameingia mpaka chumbani eti mnadai mmewakamata! pia tuliona hata kuokoa wahanga wa mv spice ilikuwa mtihani sasa wanakula mshahara tu na kupiga magwaride kwenye sherehe
   
 4. N

  Natsima New Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani hapo ndo umefikiria hadi mwisho? We umelisaidia nini ili lifanye kazi kama unavyotaka
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  hii ni hatari jamani JWTZ wapulizeni hao wakongo mpaka wanyooshe maelezo. Nalog off
   
Loading...