Tanzania yatinga Fainali...

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,421
2,271
Timu ya Bongo FC ya Finland jana iliweza kuingia fainali ya kombe la Prevention ilipoweza kuifunga Guinea kwa mabao 2-1. Sasa Bongo FC itakutana na Nigeria katika fainali itakayochezwa siku ya Jumamosi katika jiji la Helsinki.

Katika mzunguko wa kwanza wa makundi Bongo FC iliweza kuifunga Nigeria kwa mabao 3-2. Wachezaji wa Bongo FC wamenukuliwa wakisema kuwa wana uhakika wa kuifunga tena timu ya Nigeria.

Mmoja wa washabiki wa Bongo FC akifurahia ushindi


Wachezaji wa Bongo FC wakipasha misuli moto kabla ya mpambano


Wadau wa Bongo FC wakitafakali ushindi dhidi ya Guinea na kupanga mikakati ya mpambano wa Fainali...
 
Last edited:

Hongera kwa ushindi. Lakini Zanzibar ni NCHI.
 
ni nchi ya baba yako? nyie mnataka muachwe peke yenu ili muendeleze ugaidi na dini yenu ya kigaidi hiyo....lol
 
Ndani ya Bongo FC kuna Wazenj wawili, wanawakilisha Nchi...
 
huyo jamaa kwenye picha namfahamu anaitwa bernard kakaengiyupo Finland
 
ni nchi ya baba yako? nyie mnataka muachwe peke yenu ili muendeleze ugaidi na dini yenu ya kigaidi hiyo....lol

umekosa sera kijana dini na ugaidi ni vitu viwili ambayo hafifanani kata kidogo maana ya dini ni mfumo wa maisha yako katika kila kitu kwa hivyo kunataratibu na misingi yake ambayo imewekwa na hakuna mtu anaweza kuirekebisha na watu wanaofanya ugaidi ni watu ambao wana person interest zao kama ungekuwa na hekima ungeelezea maana ya ugaidi na maana ya dini ndiyo utajua kijana things before u do everything...
 
Final: Prevention Cup

Leo saa kumi na nusu kwa saa za Afrika Mashariki, Bongo FC itajitupa dimbani kuwavaa Nigeria..
Yote yakayojili katika mpambano huo yatawekwa wazi hapa JF kama kawa......
 
Hatimae Tanzania(Bongo FC) imetwaa kombe la Prevention baada ya kuiadhibu Nigeria kwa bao 2-1. Nigeria ambao leo walikuwa na matumaini ya kuibuka washindi, walijikuta wakotolew nje na Bongo FC ambao walicheza vizuri sana katika kipindi cha pili
Bongo FC wenye jezi za njano wakishangilia bao la pili na la ushindi dhidi ya Nigeria.

Hadi kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza Nigeria ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0. Kipindi cha pili Bongo FC waliingia kwa nguvu mpya na kucheza mpira wa hali ya juu, na kufanikiwa kuzawazisha bao na mfupi kujipatia bao la ushindi.


Wachezaji wa Bongo FC katika picha ya pamoja na kombe la Prevention, wakishangilia ubingwa.

Wa pili toka kushoto ni kocha wa Bongo FC akiwa amezungukwa na wachezaji na washabiki mara baada ya mpira kwisha





Mh. Paul Sozigwa mwenye kombe alikuwepo kushuhudia Bongo FC wakichukua ubingwa.
 
Moja ya kash kash za bongo FC langoni mwa Nigeria.....

Wakenya walijitokeza pia kutoa shavu kwa Bongo FC....
 
Dennis Londo na Wasomali hao umewatoa wapi? wewe si umeoa mfini? Mkeo akikuona na hizo totozz utamweleza nini?
 
sasa na wao basi walete kombe Bungeni kwani tumeshazoe hata kama ni kakombe mbuzi (I.E Coca cola) as longer as tumetwaa bungeni watu wanletwa Bungeni.Noomba niwepo kwenye kamati ya maandazlizi ya kuwapeleka Bungeni.
 
ni nchi ya baba yako? nyie mnataka muachwe peke yenu ili muendeleze ugaidi na dini yenu ya kigaidi hiyo....lol

Unajua mamake ni nani ? Ivyo wewe nae si mama mmoja sasa kiherehere cha mama yako kukubali kolewa na gaidi wa dini nyengine. Bi mkubwa kashindwa kuzuia hamu yake na hivyo akajitosa,
 
Kati ya wachezaji 4 wa Bongo FC, 1 picha inatoa ugumu wa utaifa wake. Lkn wapinzani 6 picha inatoa maelezo yasio na maulizo sana. Kulikoni? au mambo ya mamluki?
 
Well done Kibz and co. Hizo jezi za "Bongoland" nitazipataje mkuu?
Shukrani, Jezi za Bongoland zilikuwa ni toleo la mwanzo wakati timu inaanzishwa, sina hakika kama bado zipo, ila nitawasiliana na utalawa, then nitakutaarifu
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…