#COVID19 Tanzania yapokea Dozi 499,590 za Chanjo ya Pfizer

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Tanzania leo imepokea dozi 499,590 za chanjo ya ugonjwa wa Uviko-19 aina ya Pfizer kutoka serikali ya Marekani ikiwa ni msaada wa mpango wa Covax.

Chanjo hizo zimepokewa wakati tayari baadhi ya Watanzania wamepata chanjo ya Johnson &Johnson na Sinopharm.

Chanjo hizo zimepokewa leo Jumanne Novemba 23, 2021 na Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima, amesema hadi sasa Serikali imepokea dozi ya Johnson &Johnson 1,227,400; 2,578,400 ya Sinopharm na 499,590 za Pfizer.

Dk Gwajima amesema takwimu zinaonesha hadi kufikia Novemba 19 wananchi 1,359,624 wamepata chanjo ambao kati yao hao wananchi 988,293 sawa na asilimia 1.7 wamemaliza chanjo na kupata kinga kamili.

Takwimu hizo ni kwa wale waliopata chanjo ya Johnson ambayo ni dozi moja na Sinopharm ni dozi mbili. Ambapo wananchi 371,331 sawa na asilimia 0.6 ya watanzania wamechanja dozi moja ya Sinopharm wakisubiri kupata dozi ya pili.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya kupokea chanjo Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright amesema serikali yake itaendelea kushirikiana na mataifa ya Afrika katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Amesema serikali yake inatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Uviko 19 na inawasisitiza watanzania kupata chanjo pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari.

Chanzo: Mwananchi

----
HOTUBA YA MHE. DKT. DOROTHY O. GWAJIMA (MB), WAZIRI WA AFYA, WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI WA MAPOKEZI YA CHANJO YA PFIZER-BIONTECH UWANJA WA NDEGE TAREHE 23 NOVEMBA, 2021.



  • Mhe.Ummy Mwalimu (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Mhe.Liberata Mulamula (Mb) Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  • Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (Mb) Waziri wa Afya, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Zanzibar
  • Msemaji wa Serikali,Mr Gerson Msigwa
  • Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milisic
  • Kiongozi wa mabalozi hapa nchini, Balozi Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih
  • Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dr Tigest Ketsela Mengetsu
  • Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Shalini Bahuguna
  • Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto,
  • Balozi Joseph Edward Sokoine, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  • Dkt. Aifello Sichalwe, Mganga Mkuu wa Serikali,
  • Mkurugenzi Idara ya Kinga,
  • Wafanyakazi wa Sekta ya Afya, Mambo ya Nje na Wizara mbalimbali,
  • Wadau mbali mbali wa maendeleo,
  • Wananchi,
  • Mabibi na Mabwana.
Ndugu Wananchi,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo na kuweza kujumuika tena hapa katika tukio hili muhimu la mapokezi ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19

Pili, shukrani za pekee ziwaendee wadau wetu wa Maendeleo hususani katika kujali afya za Watanzania kwa kutupatia Chanjo ambazo zitatusaidia kuwakinga dhidi ya mapambano ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).

Shukrani za pekee ziwaendee mpango wa COVAX Facility ukiongozwa na mashirika ya GAVI, WHO, CEPI na UNICEF kwa kuanzisha mpango huo hususani kwa kuwezesha kupatikana kwa chanjo dhidi ya UVIKO -19 ambazo leo kama nchi tunapokea awamu ya tatu ya chanjo hizi. Leo tunapokea chanjo aina ya Pfizer-Biontech.

Vilevile nachukua fursa hii kuwashukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, na uongozi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kwa kukubali jukumu la kuandaa mapokezi ya chanjo hii. Hongereni sana kwa maandalizi mazuri mliyofanya.

Nawashukuru viongozi wote mliofika mahala hapa leo hii kushuhudia upokeaji wa chanjo hizi za Pfizer-Biontech na huku mkiwawakilisha wengine wengi ambao wangependa kuwepo hapa leo lakini kwa sababu ya majukumu mengi haikuwezekana.

Ndugu Watanzania,

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana afya za Watanzania. Ndiyo maana tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma za kinga nchini. Hadi sasa tumekwisha pokea jumla dozi 1,227,400 za Jenseen ambazo zinakinga watanzania 1,227,400 (dose moja) na Dozi 2,578,400 za Sinopharm ambazo zinakinga watanzania 1,289,200(kwa dose mbili) na leo tonapokea dose 499,590 za Pfizer ambazo zitakinga watanzania 249,795(dose mbili).

Ndugu wananchi hadi kufika kufikia tarehe 19.11.2021, takwimu zinaonyesha kuwa tumeshafikia wananchi 1,359,624 walipata chanjo. Ambapo kati ya hao wananchi 988,293 sawa na asilimia 1.7% ya watanzania wamemaliza chanjo na kupata kinga kamili dhidi ya UVIKO 19 kwa kuchanja dozi moja ya Jensen na wengine Sinopharm dose mbili. Aidha wanchi 371,331 sawa na asilimia 0.6% ya watanzania wamechanja dozi moja ya Sinopharm. Napenda kuwapa pongezi wananchi wote waliojitokeza kupata huduma hii na kukamilisha chanjo ,kwani wamechukua uamuzi sahihi wa kulinda afya zao na wananchi wengine hususani kwa mikoa kumi inayoongoza sasa ambayo ni DaresSalaam,Kilimanjaro,Dodoma,Arusha,Mwanza,Ruvuma,Mbeya,Morogoro, Mtwara na Kagera.

Napenda kusisitiza wale ambao bado hawajapata chanjo, wafanye haraka kupata huduma hii kwani ugonjwa wa UVIKO-19 upo na tumeendelea kuwapoteza ndugu zetu kutokana na ugonjwa huu. Aidha nitoe pongezi zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali Taifa letu na kutuletea huduma hii ya chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Ndugu Watanzania,

Leo tunapokea chanjo dozi 499,590 aina ya Pfizer kutoka COVAX Facility kwa ajili ya kuendelea kuwapatia wananchi aina nyingine ya chanjo dhidi ya UVIKO-19, hii itawapatia wananchi fursa ya kuchagua chanjo anayotaka. Chanjo hizi kama zilivyokuwa za Janssen na Sinopharm zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni bora na salama.

Ndugu Watanzania,

Napenda kuwajulisha watanzania kuwa, Wizara ya Afya itafanya wajibu wake wa kujiridhisha na uhakiki wa ubora wa Chanjo hii kwa kupitia wataalamu wetu na Mamlaka husika kabla ya kuanza kutolewa kwa Watanzania.


Ndugu Watanzania,

Serikali itaendelea kutoa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo hivyo, niwaombe wanaohusika na zoezi hilo kuwajibika kwa kasi kubwa ili kuwawezesha watanzania wengi kupata chanjo mapema iwezekanavyo. Aidha, Wizara ilitoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania.

Ndugu Watanzania,

Mara baada ya kuzihakiki, mpango wa usambazaji upo tayari na mara moja zitapelekwa katika vituo vyetu kwa ajili ya kuwapatia wananchi. Napenda kusisitiza kwamba chanjo zinatolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini kwa hiari na bila malipo. Hii ni pamoja na vituo maalumu vilivyoundwa kwa ajili ya kuwezesha kusogeza huduma hii karibu zaidi na jamii (huduma mkoba). Natoa wito kwa Jamii nzima ya Watanzania kujitokeza kupata chanjo hii dhidi ya UVIKO -19 kwani jamii ikipata Chanjo itasaidia sana kupunguza milipuko ambayo inaweza kutokea mara kwa mara na ikijitanabaisha kwenye ugonjwa mkali unaohitaji matibabu ya muda mrefu ikiwemo kulazwa wodini na kufikia kufariki.

Ndugu Watanzania,

Ninachukua fursa hii kuwaagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi mnahimizwa kwenda kwenye vituo vya huduma za afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chanjo. Aidha, nawahimiza wananchi kuchukua hatua mbalimbali za kujikinga dhidi ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na uvaaji wa barakoa, kunawa mikono kwa maji na sabuni, kutumia vitakasa mikono (sanitizer) na nyinginezo ambazo wataalamu wa afya wamekuwa wakiendelea kuzisisitiza.

Ndugu Wanahabari,

Mwisho, Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wengine wote wenye nia ya kusaidia eneo hili kwa namna moja au nyingine kujitokeza na kufuata utaratibu wa mwongozo wa serikali kuhusu suala la kuwezesha msaada huo. Dunia ni yetu sote kila mmoja analo jukumu la kuilinda kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
 
Serikali ya Tanzania leo imepokea dozi 499,590 za chanjo ya ugonjwa wa Uviko-19 aina ya Pfizer kutoka serikali ya Marekani ikiwa ni msaada wa mpango wa Covax.

Chanjo hizo zimepokewa wakati tayari baadhi ya Watanzania wamepata chanjo ya Johnson &Johnson na Sinopharm.
Mleta mada beth , we ulishachanjwa?
 
Kuna kiongozi mmoja mkubwa wa wajinga na wapuuzi alishawahi kutuaminisha kwamba Corona haipo na kwamba tutashinda kwa nyungu na maombi?
Shetani yule sasa imebaki historia acha wananchi wachanjwe
Nati zake kadhaa kwenye ubongo wake zilikuwa zimelegea, mtu timamu hawezi fanya/sema aliyokuwa anayafanya/sema hadharani
 
Kuna kiongozi mmoja mkubwa wa wajinga na wapuuzi alishawahi kutuaminisha kwamba Corona haipo na kwamba tutashinda kwa nyungu na maombi?
Shetani yule sasa imebaki historia acha wananchi wachanjwe
Sadakta, tena yule kiongozi ni punguani wa mapunguani eti uliona wapi scientist anapinga science?
 
Nati zake kadhaa kwenye ubongo wake zilikuwa zimelegea, mtu timamu hawezi fanya/sema aliyokuwa anayafanya/sema hadharani
Wewe ndio mshenzi, huwezi kuwafanya wananchi kuwa majaribio ya chanjo ambazo hujui hata chemical components zake. Unabugia tu.

Wakileta machanjo ya marekani unabugia, wakileta machanjo ya china unabugia, ya Russia unabugia. Ati tunafuata sayansi! Mweeeh!!

Hizi nchi za kajamba nani za Afrika na hasa Tanzania bado hazijajitambua. Kuna vibaraka wengi mno ambao ni version mpya ya machifu mangungo.

Ukishalambishwa dollar na wazungu basi unabong'oa unawaachia wakufire wanavyotaka. Jifunze kujitegemea.

Huwezi kuwa shoga wa wazungu milele. BE INDEPENDENT and conscious.
 
Mabeberuwamekupa shingapi ya kudalalia machanjo?

Nyerere Mabeberu yakamshinda

Mzee Mwinyi Wahisani au wafadili

Mzee Mkapa Wadau wa maendeleo

Mzee Kikwete Wadau wa maendeleo

Lijinga MABEBERU
 
Mungu wangu hiv we ni mzima kiakili?
Vyeti feki vinakusumbua fanya kazi yondo sster
Mm sina vyeti feki mzee. Wala sijawahi felix mitihani wowote wa taaluma kwenye maisha yangu. Acha kupiga hoja kwa mungu!? Kwa hiyo wenye vyeti feki siyo raiya???
 
Anauwezo wa kukataa masada wa mzungu wewe? Miaka 60 ya uhuru wameshindwa hata kubadilisha maji ya bahari yawe yanafaa kwa matumizi yakawaida ya binadamu wewe unabaki kushabikia mashangingi na ma v8? Huku watu wakiishi bila.maji.
Hovyooo
Ati mabeberu
Wewee, jibidishe kufanya kazi na kujitegemea. Huwezi kuwa kibaraka wa wazungu siku zote. NI AIBU.

Do some manual works. Carpentry, plumbing, whatever. Earn a lawful living.

Acha haya mambo ya kuwabong'olea mabeberu.

Haiwezekani nchi iwe majaribio ya machanjo ya watu. Pfizer unabugia, moderna unabugia, sijui matakataka gani unabugia!!


Wanakupa shingap?
 
Back
Top Bottom