Tanzania Yapanda katika Viwango vya Fifa -October

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
676
34
Tanzania imepanda katika viwango vya soka vya Shirikisho la Dunia la Soka (FIFA) kwa mwezi wa Oktoba. Kwa mujibu wa tovuti ya Fifa Tanzania imepanda hadi nafasi ya 110 kutoka nafasi ya 117 mwezi wa September. Tanzania inategemewa kupambana na Sudan mwishoni mwa November katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani. Sudani iko nafasi ya 106 kwa miezi yote miwili September na Oktoba.

Katika Top 10 kwa Oktoba ni:

1. Spain
2. Italy
3. Germany
4. Brazil
5. NetherLand
6. Croatia
7. Argentina
8. Cech Republic
9. Russia
10. Portugal

Kazi kwa Maximo na vijana wake kututoa kimasomaso!!
 
Back
Top Bottom