Tanzania yangu chini ya mkoloni CCM

Tanzania yangu chini ya mkoloni CCM

Zombi Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
1,076
Reaction score
2,161
Naishi Tanzania, lakini sihisi huru. Chini ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), najiona kama mtumwa katika nchi yangu mwenyewe.

Uhuru tuliourithi kutoka kwa kina Nyerere umebaki historia, kwani viongozi wa sasa wameugeuza kuwa fursa ya kujinufaisha wao na familia zao, huku mwananchi wa kawaida akizidi kunyonywa, kudhulumiwa na kupuuzwa.

Ninajuta sana kuona taifa hili likizama kwenye umasikini, rushwa, ukosefu wa haki, na uongozi wa kibabe. Viongozi wa sasa wamejisahau – wanajenga leo yao kwa tamaa, bila kujali kesho ya watoto wao.

Wanatunga sheria kwa faida ya muda mfupi, wakisahau kwamba maisha ni mzunguko, na kesho inaweza kuwageukia wao au kizazi chao.
 
Pole, komaa ndio ukubwa. Kwenye changamoto ndipo akili hufanyakazi zaidi. China walikumbwa na njaa miaka ya nyuma ndio maana wakaanza kula hadi nyoka na vitu vya ajabu ajabu.
 
Naichukia sana ccm inatutesa kwa kuwa ina kila kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom