Tanzania yang’ara Mkutano wa Kupambana na Rushwa London

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Screen-Shot-2016-05-13-at-5.11.35-PM.png

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu Majaliwa katika kikao cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, ameelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne, ambavyo ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.

Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ofisi yake haijahusika na kuandaa mkutano wa wanadiaspora waishio Uingereza kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu maalum wamechaguliwa kushiriki mkutano huo.

Amesema mkutano huo umepangwa kufanyika kesho na uko wazi kwa Watanzania wote kushiriki ili waje kusikiliza nchi yao imefanya nini na kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi, watapatiwa fursa hiyo.

Source: Channel ten
 
JPM atakimbia na huo wa Japan maana nadhani hajiamini kutiririka kwa kithungu! Na yule Mlowola sijui anajiweza kupanda kwa podium na ku present issues za rushwa na kukaribisha maswali n majibu papo kw papo? Au ndio wataomba Mtume maswali wajibu kwa email! Kazi ipo! Ila tutafika tu! Nguvu kwa nguvu
 
Watz kama wewe sijui mkoje, JK alikuwa anasafiri SANA akawa vasco, Leo Tumempata JPM Yuko busy home mnasema hajiamini... Mimi nasema JPM usiende popote piga kazi humu humu Achana Na Hawa pimbi Na nyumbu wasio jua watakacho.
 
Sasa Imeng'ara wapi.Sheria ya kupambana na Rushwa inayowalazimisha TAKUKURU kupitia kwa DPP ndipo kesi ziende mahakamani inapaswa kubadilishwa

Kiitifaki Waziri Mkuu wa Uingereza ana uwezo gani wa kualika nchi nyingine kwenye mkutano utakaofanyika Japan?

Kama ni mwamvuli wa Commonwealth Malkia ndio hualika. Au nimefikiri reverse.
 
Sijaona ilipong'ara maana Issue za Stanbic,Masamaki,Wauza madawa,Wauza sukari wamekamatwa na washakuwa cleared bila hatia its mean Rushwa imetumika hapo.... huo ung'araji chai sana
 
Hayo mambo ya kupambana na rushwa tayari nishampa 100%. Bado hajanikosha kwenye eneo la kutoa uchumi hapa ulipo na kusonga mbele. So far, sijaona mkakati mahususi wa kufanikisha jambo hilo.
 
Sasa Imeng'ara wapi.Sheria ya kupambana na Rushwa inayowalazimisha TAKUKURU kupitia kwa DPP ndipo kesi ziende mahakamani inapaswa kubadilishwa

Kiitifaki Waziri Mkuu wa Uingereza ana uwezo gani wa kualika nchi nyingine kwenye mkutano utakaofanyika Japan?

Kama ni mwamvuli wa Commonwealth Malkia ndio hualika. Au nimefikiri reverse.
To be honest tunawashangaa sana. Kwa argument hizi chadema inabid mkae chini mjipange namna ya kuuhandle huu utawala wa magufuli. Tuliwaamin sana ila mnazidi kupoteza credibility. Chama kinakufa. Hamna anayejenga hoja tena. Mlichobaki mnapinga the obvious. Magufuli anafanya vizur kwa ujumla. Kwenye mabaya pingen kwenye mazur sifien. Lakin kwa style hii ya kupinga kila kitu trust me ata wale wana ukawa wachache waliobak ambao hawajamuelewa magufuli come 2020 watakua washamuela na mtaambulia aibu. Nakuakikishia uchaguz ukiitishwa any time from now to 2020 chadema haitapa hata 10% ya kura zote
 
JPM atakimbia na huo wa Japan maana nadhani hajiamini kutiririka kwa kithungu! Na yule Mlowola sijui anajiweza kupanda kwa podium na ku present issues za rushwa na kukaribisha maswali n majibu papo kw papo? Au ndio wataomba Mtume maswali wajibu kwa email! Kazi ipo! Ila tutafika tu! Nguvu kwa nguvu
Acha dharau lofa we. Kwani kuongea kiingereza ndio usomi? Nenda kwa machangudoa wa mitaa ya Ohio uone wanavyotiririka kimombo na wengi shule hakuna.
 
Now Tanzania tuna Rais Mzalendo wa ukweli. before tulikuwa na Marais watalii. tunajivunia kuwa na huyu JPM. wait hizi nchi za magharibi soon watatukubali + kutupigia saruti kudadakekii.... zao
 
Sasa mwenye PHD anashindwa kuongea changu asiye hata darasa moj anatiririka! Unasemaje hapo? Alikariri shule na kumez tu? Akienda midahalo mikubw ka unaofanyika sasa Rwanda ataongea nini aibu ajipange tunakosa mengi!
Acha dharau lofa we. Kwani kuongea kiingereza ndio usomi? Nenda kwa machangudoa wa mitaa ya Ohio uone wanavyotiririka kimombo na wengi shule hakuna.
 
Sasa Imeng'ara wapi.Sheria ya kupambana na Rushwa inayowalazimisha TAKUKURU kupitia kwa DPP ndipo kesi ziende mahakamani inapaswa kubadilishwa

Kiitifaki Waziri Mkuu wa Uingereza ana uwezo gani wa kualika nchi nyingine kwenye mkutano utakaofanyika Japan?

Kama ni mwamvuli wa Commonwealth Malkia ndio hualika. Au nimefikiri reverse.
Povu linakutoka,kwanini Juzi PM Wa UK alikua anampa taarifa malkia kuhusu mkutano,unajuaje amepewa maagizo na Malkia,wewe lini uliona nakusikia kwenye vyombo vya Habari malkia akialika watu!?
 
Hayo mambo ya kupambana na rushwa tayari nishampa 100%. Bado hajanikosha kwenye eneo la kutoa uchumi hapa ulipo na kusonga mbele. So far, sijaona mkakati mahususi wa kufanikisha jambo hilo.
Uchumi mikakati yake lazima ukomeshe ufisadi kwanza ili uweze kufanikiwa Bila hivyo wapambe watakula zote kbsaaa
 
Acha dharau lofa we. Kwani kuongea kiingereza ndio usomi? Nenda kwa machangudoa wa mitaa ya Ohio uone wanavyotiririka kimombo na wengi shule hakuna.
Safi nadhani ukichunguza sana elimu zetu ili ujulikane msomi uweze umombo!?kuna uhusiano gani utawala bora na lugha ya mwezako!?nadhani chadema inapoteza mwelekeo kwakua inawatu ambao daima awapendi ukweli
 
Back
Top Bottom