Tanzania yang'ara kwa amani duniani

Tanzania yang'ara kwa amani duniani

Iking'ara Afrika Mashariki ama duniani si ni kung'aa tu. La muhimu imeng'aa ama unataka tuwe tunanunua nyama kwenye mabucha ya Ulaya wakati nyama ni ile ile?
Kunga'ra duniani na kung'ra locally vitu tofauti kabisa...Tanzania inaweza kuwa na amani ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka, kwa dunia haipo

Hao wanaowasifia kwa amani si ndio waliwakosoa kwa mauaji ya watu juzi mkawapinga?
 
Hivi hizi tafiti zinafanyikiaga wapi na nani anafanya ?

Tango pori analishwa mtu hapa
 
Tanzania kuna nidhamu ya woga tu, Kwa amani haipo kabisa.
 
Point of correction

Tanzania inaongoza nchi zenye raia waoga.
 
Mmmm watu ndio kwanza wanahubiri tulinde amani, ukiona jambo ambalo watu au viongozi wanahubiri ujue kuna jambo, hakuna amani, kuna uvumilivu tu. Kuna siku watu watachoka
 
Inang'ara kwa amani Duniani au Afrika Mashariki?

Kunga'ra duniani na kung'ra locally vitu tofauti kabisa...Tanzania inaweza kuwa na amani ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka, ila kwa dunia haipo

Hao wanaowasifia kwa amani si ndio waliwakosoa kwa mauaji ya watu juzi mkawap
Kipimo cha amani nchini mwako wewe unakipimaje? Au unasubiri ripoti ya nje?

Kwangu mimi, amani ya nchi naipima kulingana na haki na uhuru wa kila mtu kwenye familia, majirani, jamii inayotuzunguka.

Kulingana na mila na desturi, kanuni na taratibu tulizojiwekea katika familia, kila mwanafamilia anatimiza wajibu wake. Ukiukwaji wa mwafamilia mmoja husababibisha kutokuwepo na amani katika familia.

Sina hofu ya kumtembelea jirani au kutembea/kufanya shughuli zangu mtaani au nje ya mtaa. Kama nimeajiriwa/nimejiajiri kila siku huenda kwenye shughuli hizo na kurudi nyumbani salama. Kama nyumbani hakuna amani kuna kanuni na taratibu za kurejesha amani.

Ukichukua mifano hiyo kwa upana wake, utapata kipimo cha amani katika nchi yetu. Tusikubali kuhadaiwa na wanasiasa ambao dhamira yao kuu ni madaraka ya kutawala, kwa maslahi binafsi. Km mara ngapi waliochaguliwa wanakuwa karibu na wapiga kura zaidi ya kuhudhuria vikao vyao vyenye malipo!!!
 
Tanzania ni ya 9 Afrika kwa amani na utulivu. Kungekuwa hakuna chadema tungalikuwa wa kwanza Afrika. Chadema na Zitto wametuharibia. Zamu ijayo hatutakubali tena watu hawa watuharibie amani yetu.
 
Hawa "wanaume" wakiwasifia mnafurahi ila wakiwapa ukweli wenu mnawaita mabeberu, wanyonyaji, waizi...
Na wakikosoa watu kama nyinyi huja mbio mkifurahi na vi screen shot vyenu mnapongezana ila wakisifia sasa povu jingiiiii kama hivi...tulishawazoea pingapinga kila kitu hata maendeleo.
 
What a greatest joke of the day.. Ni sawa na ukimya wa makaburini
 
Na wakikosoa watu kama nyinyi huja mbio mkifurahi na vi screen shot vyenu mnapongezana ila wakisifia sasa povu jingiiiii kama hivi...tulishawazoea pingapinga kila kitu hata maendeleo.
Kwa hiyo unaamini kwamba serikali ya magufuli ni kigeugeu?
 
habari mbaya sana kwa pingapinga na vibaraka Wa chadema wao wanataka kila siku habari za kuikosoa govt ili wapate political point za kuwadanyia mazuzu wao....
 
sio govt ..

Mbona unajichanganya mkuu? Umekula kweli?

Hoja ni hii... Serikali wakitetewa na "mabeberu" basi watawasia kweli ila wakiambiwa "ukweli mchungu" basi watawaita mabeberu hao hao majina kama wezi, wanyonyaji and the alike.

Sasa nikakuuliza je serikali ya magufuli ni kigeugeu??
 
Hongera pekee iende kwa vyama vya upinzani manake mengine yote yanayopoteza amani nchi zingine na Wapinzani wa Tanzania wanafanyiwa; lakini for the sake of amani yetu, wanaamua kutumia busara ili kutoivuruga nchi!

Maalim Seif amenyang'anywa ushindi mchana kweupe lakini badala ya kuwahamasisha wafuasi wa CUF kupigania ushindi wao; ndo kwanza akawahamasisha watulie!

Ni nani asiyejua hicho ni moja ya vyanzo vya uvurugikaji wa amani Africa?

Mbowe akaitisha UKUTA na watu wakahamasika! Lakini kwa kuchelea UKUTA ungevuruga amani; Mbowe aka-call off dakika za mwisho!!

Tanzania ni moja ya nchi chache sana Africa ambako, moja ya viongozi waandamizi nchini wanaponea chupuchupu kuuawa lakini bado viongozi wakuu wanawapoza wafuasi!!

Hongereni Vyama vya Upinzani na Wafuasi wenu manake pamoja na kwamba serikali imeoonesha dalili zote za kidhalimu na kupenda damu za raia wasio na hatia; nyie kwa busara zenu mmeepusha kutoa kafara ya damu za wanadamu kwa Mazimwi yala watu!

God bless Tanzania!
Pongezi kwa wananchi wanaokataa kudanganywa na wanasiasa wanaosaka kiki
 
Pongezi kwa wananchi wanaokataa kudanganywa na wanasiasa wanaosaka kiki
Kweli kabisa ndugu yangu... hoja yako naiunga mkono! Na pongezi zaidi hususani kwa wananchi wa MKIRU ambao, pamoja na ndugu na jamaa zao kupotea katika mazingira yakutatanisha huku ikihofiwa wameuawa na maafisa wa serikali lakini bado wananchi hao wameamua kuvuta subira!
 
Back
Top Bottom