Tanzania yakubali kuipatia Kenya madaktari 500 kusaidia upungufu wa Madaktari

Daktari mwenye akili na mwenye kuona mbali hawezi kwenda huko kuhatarisha maisha yake na kusaliti wenzake.
Mgomo Kenya umeshaisha, plus kuna wabongo wanafanya kazi DRC, South Sudan sasa kwa nini unataka kuwatisha kwenda Kenya.
MSHAHARA WA DR KENYA NI MARA MBILI YA BONGO.
 
Wajue tu kuwa Kenya ukipasua kichwa badala ya goti watakudai fidia na kufungwa juu.


Na washawasha!
 
Magufuli ameshindwa kuajiri madaktari huo ndio ukweli Kenya has more dr and better trained than Tz
 
Kwa watu tunaoshughulika na masuala ya mahusiano, tuna mashaka makubwa sana na uamuzi huu. Usalama wa madaktari wetu upoje? Je madaktari wetu watapata ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha majukumu yao? Je, chama cha Madaktari Tz hakijiingizi katika mgogoro na chama cha Ke? Tusisahau kuwa madaktari wetu wanakwenda kuhudumu katika Jamii. Je wanajamii ambao ndugu zao wamekosa kazi na kuchukuliwa na madaktari kutoka Tz watawaacha salama madaktari Wetu? Je ukabila ulioko Ke hautawadhulu madaktari Wetu. Mimi nadhani jambo hilo linahitaji uchambuzi makini. Serikali inatakiwa ijiridhishe vya kutosha kabla ya kukubali ombi hilo.
 
Mmmh.. Kenya nagoifahamu mm. Tusishangae kusikia madaktari wakidhuriwa au kutekwa..labda kama watapewa ulinzi
 
arleady we failed as a state, kwa uhaba uhu unapeleka madoktar nje tena 500, n ujuha uhu. kenyata kashndwa kumalzana na madaktar kenya, chonde chonde usalama wa watoto hawa wa maskn man wakenya c wa2 wa spot spot
 
Sisi wametosha au haruna hela ya kuwaajiri
Haahahaaa,Sio kweli,sisi wenyewe tuna uhaba wa madaktari,halafu sisi ati tuwape madaktari,Ni madaktari au medical assistance?,wasaadizi wauguzi,sisi wenyewe tu upungufu mkubwa wa madaktari.
 
Kumbe sisi madokta wametosha ehh
Wanatosha sana. Tuna excess ya 3,000 doctors na vyuo vyetu vikuu vinafyatua 1,500 MDs yearly. Na hii itaongezeka zaidi pale vyuo vikuu vya UDOM na Mloganzila vitakapoanza kufyatua. Wastaafu hata kama ni mabingwa kiasi gani na bado wana nguvu za kufanya kazi hatuwapi mikataba kwa sababu tuna excess ya madaktari bingwa vile vile.

Huo ndiyo ukweli. Tanzania tumesonga mbele sana kwenye masuala ya elimu. Tuna maelfu ya maelfu ya wahitimu wa vyuo vikuu wako mitaani jobless, wakiwemo waalimu, wahasibu, wanasheria, madaktari, wahandisi na wana sanaa mbali mbali. So we can be a donor country in this field.
 
I just hope wote waliouponda uamuzi bila tutoa alternative siku madaktari wetu wakigoma tutakua na afya tele na hatuna ndugu alie mahututi hospital na inchi jirani zimegoma kutoa msaada kwakua tu wakati wao wanahitaji hatukuwasaidia...ni kweli ht sisi ma dr hawatutoshi ila kwa wenzetu ni state of emergence ikiisha watarudi...tuliokua na wagonjwa kipindi cha mgomo wa kina Dr Ulimboka watakua wanaelewa na maanisha nn...Amani na iwe kwenu
 
hii ni serikali uchwari mungu saidia.
muda si mrefu waziri au naibu wake watakuja kusema tanzania inaupungufu wa madaktari fulani.


ukiwa msemaji bila break, ajaribu kuweka akiba ya maneno.
 
Inashangaza, maana kwenye hospitali nyingi tuna upungufu wa madaktari!

Ni kweli Madaktari kwene hospitali zetu hawatoshi LAKINI WAPO MTAANI HAWANA AJIRA! Serikali ya CCM imeshindwa kuwapa ajira haina fedha wafanye nini basi?Hata hao walio ajiriwa hawalipwi inavostahili!Kuna madai yao lukuki na hasajalipwa!!!
Acha waende huko kwa Uhuru Kenyatta akawape ajira!
  1. Angalizo: 1 Kenyan Shs is equivalent to 20 Tshs.
  2. Angalizo: Securty ya Kenya si mzuri sana.Al-Shaabab wako all over hasa notthern Kenya.
Doctors mtakaopata nafasi hizo chukuei tahadhari zote za kiuchumi na kiusalama.Mtakao bahatika all the best!
 
View attachment 482795
5c37841ad50a804e822edcf4c88cd1a9.jpg


Tanzania imekubali ombi la kuipatia Kenya madaktari 500 watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba hasa baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao leo tarehe 18 Machi, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Wizara ya Afya ya Kenya uliotumwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenya.

Kiongozi wa ujumbe huo ambaye ni Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Dkt. Cleopa Mailu amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa baada ya kutokea mgomo wa madaktari pamoja na uamuzi wa nchi hiyo kugatua madaraka katika sekta ya afya, imebainika kuwa nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa madaktari ambao hauwezi kumalizwa kwa kutegemea madaktari wanaosomeshwa nchini humo bali kupata madaktari kutoka nje ya nchi.

Mhe. Jack Ranguma amesema Kenya ipo tayari kuwalipa stahili zote madaktari 500 watakaopatiwa kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na mishahara na nyumba za kuishi.

Nae Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wizara yake ipo tayari kutoa madaktari hao haraka iwezekanavyo kwa kuwa Tanzania inao madaktari wengi wazuri ambao wamemaliza masomo yao na hawajapata ajira, na wengine wamemaliza mikataba yao ya kazi na bado wana uwezo wa kufanya kazi.

“Kwa hiyo nitoe wito kwa madaktari wote Tanzania ambao hawapo katika utumishi wa umma, hawapo katika hospitali teule na ambao hawapo katika hospitali za mashirika yasiyo ya kiserikali wanaolipwa na Serikali, waombe nafasi hizi.

Vigezo vikubwa ambavyo tutaviangalia ni kwanza awe amemaliza mafunzo ya vitendo (Internship) na pili awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika, kwa hiyo leo hii tutatoa tangazo na tumefurahi sana kwa sababu tunao madaktari wa kutosha ndani ya nchi na tunaweza kuwapeleka Kenya” amesema Mhe. Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli amesema Tanzania imekubali ombi hilo kwa kuwa Kenya ni ndugu, jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania na amemtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Ummy Mwalimu kuharakisha mchakato wa kuwapata madaktari hao ili wawahi kwenda Kenya kutekeleza jukumu hilo.

“Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tutawapatia madaktari hao 500 ili wakatoe huduma ya matibabu kwa ndugu zetu waliopo Kenya, na kwa kuwa mmenihakikishia kuwa madaktari wangu mtawalipa mishahara inavyotakiwa, mtawapa nyumba za kuishi, na mtahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri na salama mimi sina tatizo na naamini mambo yatakwenda vizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

18 Machi, 2017


MI NISINGEENDA AISEE, HUO UADI NI MKUBWA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
pale unapoona mzee wako anakupeleka yeye mwenyewe ili uwe sadaka nawe unamshangilia kuwa ni shujaa.!
Wamepelekwa watu DRC, Somalia, Sudan, Msumbiji, kutaja machache, tena kwenye mrindimo wa mabomu itakuwa wadaktari kwenda Uganda????? Ndio maana ya kuhakikishiwa nyumba na ulinzi
 
Mgogoro wa madaktari kenya umeshakwisha.nawashanga watu mnaolalamika mbona botswana wapo madaktari wengi wa tz hamsemi.acheni vijana wapate ajira.sisi sio kwamba wametosha hapana ila ajira ndiyo hakuna.kwa hiyo ni jambo jema tu kwa mh Rais kwa uamuzi huo.kuliko vijana wetu waendelee kuzurula mitaani.
 
Mie nasubiri tamko la chama cha madaktari-MAT juu ya hili la serikali,manake wiki moja ilopita wifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari cha huko Kenya kuhusu hili suala...
Walishasema hawako tayari kwenda huko.

Mtego huu.
 
Unprecedented move. Its a strong message to Drz and otherz that should they boycott we will do the same
 
Back
Top Bottom