Tanzania yakanusha ripoti kuhusu FDLR

Tanzania yakanusha ripoti kuhusu FDLR

rpg

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
3,620
Reaction score
1,478
Tanzania imekanusha vikali tuhuma kwamba imekuwa ikiwaruhusu viongozi wa kundi la waasi la FDLR kufanya mikutano nchini humo.

Hapo jana kulikuwa na taarifa ambazo zilitangazwa na vyombo mbali mbali vya habari duniani kuhusu ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja mataifa kuhusu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba iilituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Katika ripoti hiyo pia wanajeshi wa Burundi wanatuhumiwa kuwa walitekeleza unyanyasaji wa kingono.

Chanzo:
BBC
 
Ni jambo zuri kwa serikali kukanusa tuhuma hizo sababu zinatutia doa na majirani zetu
 
Kama wanaweza wakasema wana ushahidi, kwa nini wasiuweke ili tuuone badala ya kusikia maneno yao pekee.

By the way, hizi habari zinakuwa recycled kila baada ya muda ili kuipa pressure Tanzania ili ipambane na FDRL kama ishara ya kuonyesha haikisaidii kikundi hicho. Rwanda hawawezi kupambana na FDRL bila ridhaa ya Tanzania.

Tofauti ya Tanzania na Rwanda ni kuwa, Kagame amewekesha kwenye makampuni makubwa ya PR ili yamsaidie katika mission zake za ndani na nje ya nchi wakati Tanzania hata magazeti ya ndani yanapambana na serikali ya Tanzania. Kwa mtaji huo ndiyo maana Rwanda wanaweza hata kupenyeza habari zao kwenye media mbali mbali za kimataifa katika mlengo wa kutetea maslahi yao.
 
Kuna hata siku moja serikali ya Tz imeshawahi kuacha kukanusha?!!! Ndio kawaida yao leo nimemsikia msemaji wa serikali mwambene anahojiwa na bbc ni kujikanyaga tu, anahojiwa kuwa mbona UN wanaushahidi kuwa kiongozi wa FDR ikuja Tz, yeye anasema hawana taarifa hiyo, Mi nina uhakika hawa watu wanapokomalia kitu jua wanamanisha. Ni suala la muda tu. Mangapi yamekanushwa ila baadaye yakaja kudhihirika ni ukweli, scandal ya radar, ndege ya rais, meno ya tembo na escrow.
 
Mwambene kajibu sawa kwani hata kama alikuja aliripoti ukumbi wa habari maelezo? Mwambene wanamtafuta kwa sababu ya kulipiga biti gazeti la the east african lillokuwa chombo cha propaganda cha Rwanda kutukana Tanzania.Sasa hivi wanahonga BBC walete taarifa za siku nyingi .BBC huwa wanakuwa very current habari zao hii ni ya siku nyingi.Naona BBC hawajajifunza kilichowapata Rwanda wakafungiwa.

Mtandao wa wanyarwanda ulioko BBC wa akina Eric David Nampesya utaiponza BBC.
 
Mtiwe doa mara ngapi? Serikali yenyewe doa tayari!

Ni kweli serikali yetu haifanyi vizuri kiutendaji hilo liko wazi lakini katika suala hili pamoja na kutia doa, hizo bado ni taarifa hazina ushahidi ama haujawekwa wazi, Si kwamba naitetea serikali lakini nasukumwa kusema hivi kulingana na uzito wa suala lenyewe.

Suala la msingi tunatakiwa kudumisha uhusiano wetu na majirani zetu ili kuendelea kulinda Amani na mahusiano mema yenye kuleta tija kwa taifa
 
Kama wanaweza wakasema wana ushahidi, kwa nini wasiuweke ili tuuone badala ya kusikia maneno yao pekee.

By the way, hizi habari zinakuwa recycled kila baada ya muda ili kuipa pressure Tanzania ili ipambane na FDRL kama ishara ya kuonyesha haikisaidii kikundi hicho. Rwanda hawawezi kupambana na FDRL bila ridhaa ya Tanzania.

Tofauti ya Tanzania na Rwanda ni kuwa, Kagame amewekesha kwenye makampuni makubwa ya PR ili yamsaidie katika mission zake za ndani na nje ya nchi wakati Tanzania hata magazeti ya ndani yanapambana na serikali ya Tanzania. Kwa mtaji huo ndiyo maana Rwanda wanaweza hata kupenyeza habari zao kwenye media mbali mbali za kimataifa katika mlengo wa kutetea maslahi yao.

Kwa hiyo BBC na Reuters wanaweza kutumika na PR team ya Kagame ?

Halafu sijaona serikali ikitaka ushahidi au ikitaka kuombwa radhi na UN au BBC
 
Kwa hiyo BBC na Reuters wanaweza kutumika na PR team ya Kagame ?
Ni pesa zako tu .Chombo chochote cha habari duniani chaweza tumika kwa PR.Mfano Gazeti la the EAST AFRICAN lina sehemu inayohusu Rwanda tu ile sehemu ni maalumu kwa ajili ya PR ya Kagame na mara nyingi hulipiwa pesa nyingi.

Hilo la reuters na bbc sidhani kama ni rahisi vyombo hivyo kama taasisi kutumiwa kirahisi na Kagame sababu BBC IMEFUNGIWA rwanda.Anachoweza kuwa anafanya ni kuhonga au ku-influence waandishi wenye asili ya Rwanda wafanye PR kwa niaba yake au kwa kupitia marafiki zao au watu wa karibu walio katika vyombo hivyo kwa kutoa makala mbali mbali ambazo wahariri wa Reuters au BBC wanakuwa wako vipofu wanadhani ni makala za kawaida kumbe wanaifanyia PR rwanda free of charge na kuidhalilisha tanzania kupitia Rwanda ambako BBC walikofungiwa.

Ushauri wangu wa bure kwa REUTERS na BBC ni kuwa wawe na tahadhari katika kuifanyia kazi Rwanda againist Tanzania hasa kupitia waandishi wao.Wafanye screening ya waandishi wao na kama wako BBC kwa maslahi ya BBC au ya RWANDA.Wapitie makala zao zote waone kama wanafaa kuendelea kufanya kazi BBC au waende wakaanzishe kampuni zao za PR kwa ajili ya kagame.
 
Mwambene kajibu sawa kwani hata kama alikuja aliripoti ukumbi wa habari maelezo? Mwambene wanamtafuta kwa sababu ya kulipiga biti gazeti la the east african lillokuwa chombo cha propaganda cha Rwanda kutukana Tanzania.Sasa hivi wanahonga BBC walete taarifa za siku nyingi .BBC huwa wanakuwa very current habari zao hii ni ya siku nyingi.Naona BBC hawajajifunza kilichowapata Rwanda wakafungiwa.

Mtandao wa wanyarwanda ulioko BBC wa akina Eric David Nampesya utaiponza BBC.
Ndio tatizo la wa Tz, kwani unapokuwa msemaji wa serikali habari unapewa idara ya habari maelezo?!! Yeye anapojibu kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama havina ushahidi kuwa huyu kiongozi wa Fdr, alishawahi kutembelea Tz, Amezitoa wapi? Msichanganye habari ndio kawaida yetu mtu akitunyooshea kidole badala ya kutafakarj tunaanza kutafuta mchawi, sasa hawa watangazaji wa bbc wanaingi aje hapa? Wao ndio wameandaa hiyo report? HAbari ikiandikwa na vyombo vya habari vya kimataifa ndio serikali inakuja juu. BBC wakiwasifia kuwa jk ndiye rais bora afrika mnakubali kuwa ni sawa ila wakiwakosoa tu wanatumika!!!
 
sasa hawa watangazaji wa bbc wanaingi aje hapa? Wao ndio wameandaa hiyo report?

Wanahusika sana kwenye mtandao wa kuchafua Tanzania.Rwanda akiwa mjumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa anaitumia nafasi yake vibaya kwa hiyo kupenyeza uwongo wake kwa wajumbe wengine wa baraza hilo.Kisha umbeya huo unachapishwa kama taarifa ya UN.Halafui hiyo taarifa inachukuliwa na mtandao wa Wanyarwanda walioko vyombo vya habari kama mnyarwanda Erick David NAMPESYA wa BBC na kusambazwa kwenye vyombo vya habari wanavyofanyia kazi kama BBC n.k
 
nilidhani nampesya ni jina kibongo!!basi tunao wanyarwanda wengi sana wanaojifanya watanzania...mkuu time will tell,serikali hii ukiitetea sana utakuja kuumbuka in the end.,save the best for last.
 
Serikali yetu siiamini na haiaminiki. Wao wakati wote hukimbilia kukanusha hata bila ya kujitafiti. Miaka mitatu Tanzania ilituhumiwa kuruhusu meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania na kuwa zilisajiliwa Tanzania. Serikali ikakimbilia kukanusha, baada ya muda ikadhihirika ni kweli na kuwa meli hizo zilisajiliwa Zanzibar.

Wizi wa EPA Dr. Slaa alipotamka tu serikali ilikanusha lakini mwisho wa yote ikadhirika ni kweli.

Wizi kupitia ununuzi wa Radar, serikali ilikanusha baadaye ikadhihirika ni kweli.

Wizi kupitia Escrow Tegeta Account ulipotamkwa tu na Kafulila serikali ilikanusha kwa nguvu zote, mwisho wa yote kila mmoja anajua.

Serikali ya namna hiyo, inaweza kuaminiwa na yeyote katika kauli zake? Wenzetu hawa huwa hawaropoki kama hawa akina Rweyemamu au akina Lukuvi, ukiona wanatamka kitu wamekifanyia kazi. Na wakisema wana ushahidi usidhani wanatishia, ni kweli watakuwa na ushahidi.

Wanahusika sana kwenye mtandao wa kuchafua Tanzania.Rwanda akiwa mjumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa anaitumia nafasi yake vibaya kwa hiyo kupenyeza uwongo wake kwa wajumbe wengine wa baraza hilo.Kisha umbeya huo unachapishwa kama taarifa ya UN.Halafui hiyo taarifa inachukuliwa na mtandao wa Wanyarwanda walioko vyombo vya habari kama mnyarwanda Erick David NAMPESYA wa BBC na kusambazwa kwenye vyombo vya habari wanavyofanyia kazi kama BBC n.k
 
Mwambene kajibu sawa kwani hata kama alikuja aliripoti ukumbi wa habari maelezo? Mwambene wanamtafuta kwa sababu ya kulipiga biti gazeti la the east african lillokuwa chombo cha propaganda cha Rwanda kutukana Tanzania.Sasa hivi wanahonga BBC walete taarifa za siku nyingi .BBC huwa wanakuwa very current habari zao hii ni ya siku nyingi.Naona BBC hawajajifunza kilichowapata Rwanda wakafungiwa.

Mtandao wa wanyarwanda ulioko BBC wa akina Eric David Nampesya utaiponza BBC.
Hata mie nimeishangaa BBC imeanza kutumiwa kama toilet paper. Hii habari tulishaijadili sana hapa JF, na tukahoji kama iwapo kuna mtu FDLR yuko Dar na anatuma pesa kwa mtu aliyepo Kampala ili azipeleke DRC, ni kwanini report inaituhumu TZ pekee na si Uganda pia? Na kuonesha kwamba report inaandikwa purposely inaweka transfer ya hela ndogo kuliko hata mshahara wangu kutoka Dar kwenda kampala kama ushahidi wa TZ kuwasaidia FDLR, hii ni dharau. Mbona report hailalamiki kuwa TZ ina wahamiaji haramu kutoka nchi kibao na hawashughulikiwi? au UN inasupport uhamiaji haramu! Hawa BBC wanakuja na report outdated na kuireport kama vile ni mpya.
Lakini hao wanaowekeza kwenye propaganda hizo wanatwanga maji kwenye kinu, hapa TZ panaitwa "Mtakuja" Wenye shida wote wanakimbilia hapa na propaganda za Aggressors huwa tumezizoea na hizi za sasa ni cha mtoto sana, tumeshawahi kuitwa taifa la kigaidi lakini baadae hao hao waliotuita wakabadili lugha.
Tanzania ilishatoa ushauri wa jinsi ya kutatua tatizo la DRC, lakini watu wakaangalia maslahi binafsi na kupinga vikali ikiwa ni pamoja na kutishia kutupiga. Sasa hivi wanaona mambo yanadoda wanaanza kutafuta mchawi.
 
Naona umekuwa too biased. Mengi uliyoongelea hapa ni hisia na hakuna uthibitisho wowote. Kwa nini usifikirie kuwa tuhuma dhidi ya Tanzania zinaweza kuwa ni za kweli?

Serikali yetu haiaminiki na inafanya kazi kama kikundi kisichokuwa na kiongozi. Kuna uwezekano, mimi naamini, viongozi wa hilo kundi kukutanikia Tanzania kwa mikutano bila hata ya mfumo mzima wa serikali kuwa na ufahamu. Unafahamu kuwa intelijensia yetu ile ya zamani haipo tena?

Pia ufahamu kuwa Kagame aliwahi kutamka kuwa angemtwanga Kikwete, je huwezi kufikiria pia kuwepo uwezekano wa serikali yetu kuwa na ukaribu na wapinzani wa Kagame ili kama vita ikitokea kuwa na advantage ya kuwatumia pia wapinzania wa Kagame. Kwenye usalama huwezi kukaa ukajibweteka wakati jirani yako amekwishakutisha kukutwanga.

Back
Top Bottom