mbona bungeni alitumia lugha ya tofauti?huyu membe vp tena?ukisikia serikali imemeza moto ndo hii issue
Hakukuwa na njia mbadala hasa baada ya wenzetu kususia kikao kilichopangwa kufanyika Dar 10-14 mwezi wa tisa.
Maadhimio ya Mzuzu yalikuwa ni kama hatutaelewana/kufikia mwafaka, basi kwa pamoja tungetafuta msuluhishi (nchi yoyote ya jirani Afrika) kisha nae akishindwa ndipo twende UN.
Sasa wao wamesusa hasa baada ya ujumbe wetu makini ulioongozwa na Mh B. Membe na Prof A. Tibaijuka kuwamwagia vielelezo lukuki kiasi chakuwaacha midomo wazi.
Sasa naamini haki ya kila mmoja itaamuliwa na jicho la dunia.
Wamalawi hawataki suluhu kwenye suala la mpaka ndani ya ziwa Nyasa. Membe yuko sahihi, watanzania ni lazima tuwashitaki wamalawi ili tupate sababu ya kuwachakaza bila kuingiliwa na watu wa nje. Tanzania ikilipeleka suala hili kwenye mahakama ya kimataifa itashinda kesi. Ikishashinda kesi, au wamalawi wakakataa kuhudhuria kwenye ile mahakama, basi sasa sababu za kuingia vitani zinakuwa ziko wazi na tutakuwa tunapigana vita vya haki - Tutashinda tu.
Malawi hawataki kwenda kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya mipaka kwa sababu wanajua wakienda kule hoja yao ni chapati, itamezwa asubuhi tuu. Sasa wanajaribu kutumia nguvu ya wakoloni waliowatawala ili kuwabeba au kuwatisha watanzania.
Mkuu hatuwezi kushindwa. Kesi hii iko wazi mno ndo maana membe anakimbilia huko, wewe unafikiri yeye mjinga. Wote wanaozungumzia kesi hii wanasema Tanzania imesimamia kwenye sheria ya kimataifa, kwa maana kuwa ikiwa sheria ya kimataifa itatumika ushindi wa Tanzania uko wazi.mkuu unaongelea tu kushinda,vipi tukishindwa tuchukue uamuzi gani.?
nadhani hiyo ndio njia pekee iliyo salia,hatutawapiga maana uwezo tunao,ila tunataka mgogolo uishe kwa majadiriano
Wamalawi hawataki suluhu kwenye suala la mpaka ndani ya ziwa Nyasa. Membe yuko sahihi, watanzania ni lazima tuwashitaki wamalawi ili tupate sababu ya kuwachakaza bila kuingiliwa na watu wa nje. Tanzania ikilipeleka suala hili kwenye mahakama ya kimataifa itashinda kesi. Ikishashinda kesi, au wamalawi wakakataa kuhudhuria kwenye ile mahakama, basi sasa sababu za kuingia vitani zinakuwa ziko wazi na tutakuwa tunapigana vita vya haki - Tutashinda tu.
Sikuona sababu hasa ya Tanzania kufungua hiyo kesi, maana tutakuwa Kama tunatapatapa, Tanzania ndio tuliowazuia Malawi kutumia hicho kipande chetu, sasa wao ndio wangefungua hiyo kesi,
Ujinga mtupu hakuna sababu ya kuwashitaki wamalawi, Tanzania inatakiwa ku-develop kwa nguvu ukanda wa ziwa upande wetu na kuweka vitega uchumi vya kukata na shoka kama vile usafiri wa majini katika vijiji husika, uvuaji wa kisasa kwenye eneo letu na kuweka kituo cha manoari za kivita kwenye eneo letu then tuone huyo kimburu anayetaka kuleta chokochoko. Actions speaks louder.
Wakati umefika kuondoa mizoga ya CCM.