Micheweni Pemba
JF-Expert Member
- Jul 13, 2010
- 351
- 179
Katika Gazeti la Nipashe toleo la Jumaane tarehe 27Juni 2016
kulichapishwa makala yanye kicha cha habari "Serikali yaingia hofu Uingereza kujitoa EU". Pamoja na mambo mengine, Mwandishi wa makala hiyo, Sanula Athanas, ameandika kuwa "SERIKALI imesema kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya (EU) huenda kukawa na athari kwa Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa nchi hiyo katika misaada inayotolewa na umoja huo nchini".
Akizungumza na Nipashe jana kuhusu athari za uamuzi huo kwa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile, alisema nchi huenda ikaathirika kimisaada na uwekezaji kutokana na uamuzi huo.
"Ni kweli kuna hofu ya athari zitakazotokana na uamuzi huo. Dunia nzima inalizungumzia suala hilo, lakini sisi bado hatujajua kitatokea nini maana Uingereza bado haijatoka (rasmi) kwenye Umoja wa Ulaya. Hofu iliyopo ni ikiwa uchumi wa Uingereza utashuka kwa maana hisa na thamani ya fedha yao kushuka katika soko la dunia, Tanzania tutaathirika kwa maana ya misaada inayotoka EU kwa sababu Uingereza anachangia."
Hata hivyo, mtendaji huyo wa serikali alisema athari za uamuzi huo zitatokea kwa Tanzania ikiwa uongozi mpya wa Uingereza utaona hakuna haja ya kuwekeza na kutoa misaada kwenye miradi iliyokuwa ikichangia wakati nchi hiyo ikiwa EU. Katika bajeti ya mwaka huu, EU ilipanga kuipa Tanzania Sh. trilioni 1.56, wakati Uingereza ilipanga kutoa msaada wa Sh. bilioni 622. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, katika bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 utakaoanza Ijumaa, serikali inatarajia kupata Sh. trilioni 3.6 za misaada ya wahisani.
"Wamejitoa kwa sababu zao wanazojua wenyewe, kuna hoja ya hili suala la wahamiaji, lakini uongozi mpya utakaoingia madarakani ndiyo utakaotupa mwanga kwamba sisi (Tanzania) tutaathirika vipi na uamuzi huo", alisema Dk. Likwelile.
Kwa upande wake, akizungumzia uamuzi huo katika mahojiano maalum na gazeti hili jana, Profesa Prosper Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, alisema Uingereza na Bara la Ulaya litaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na uamuzi uliofanywa na Waingereza. Aidha, mtaalamu huyo wa masuala ya uchumi alisema Tanzania itaathirika kibiashara, uwekezaji, misaada na utalii.
"Uamuzi huu utakuwa na athari kubwa kwa Uingereza yenyewe na Ulaya. Tanzania itaathirika pia kwa sababu inategemea EU na Uingereza. Uingereza imekuwa ikishirikiana na Tanzania kibiashara na uwekezaji. Ikiwa Uingereza itayumba kiuchumi, maana yake biashara na uwekezaji wa Tanzania utayumba pia, misaada pia itaathirika.
Sekta ya utalii pia itaathirika; watalii watapungua. Kwa kifupi tutaathirika kwa njia nyingi, nyingi tu. Na kwa sababu Uingereza ina mchango mkubwa wa uchumi kwenye Umoja wa Ulaya, umoja huo pia utaathirika na ukishaathirika, Tanzania nayo intaathirika kwa kukosa au kupata misaada kidogo kutoka umoja huo."
MAONI: Kwa kweli inashangaza sana kusikia viongozi wa serikali ya Tanzania wakielezea khofu zao zinazoashiria kuwa kujitoa kwa Uingereza kutoka Muungano wa Ulaya kutaiathiri vibaya Tanzania ki-misaada, ki-biashara na ki-uwekezaji. Kubwa linaloonekana zaidi hapa ni khofu ya kukosa misaada ya kuichumi na kimaendeleo tu; sio jambo jengine. Inashangaza sana.
Mimi nilidhani kuwa kujitoa kwa Uingereza kutoka Muungano wa Ulaya kutaifanya serikali ya Tanzania kutafakari kwa makini juu ya hali ya baadaye ya Muungano wa Tanzania. Nasema hivi kwa sababu, sababu zilizowapelekea wananchi wengi wa Uingereza kupiga kura ya maoni kuamua kujitoa kutoka Muungano wa Ulaya ndio sababu zilezile zinazowafanya Wazanzibari wengi tu kudai mamlaka kamili kwa Zanzibar kutokana na kero za Muungano zisizokwisha.
Kwa hivyo, lililo muhimu hapa sio kuzingatia uwezekano wa kukosa misaada au uwekezaji tu; kwani Uingereza, iwe ndani au nje ya Muungano wa Ulaya, bado ina mamlaka ya kutoa au kutokutoa misaada kwa Tanzania. Hii ni haki yake ya msingi kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo na uwezo wake kama nchi huru katika Jumuiya ya Kimataifa. Cha kujifunza hapa ni namna ambavyo serikali ya Tanzania itakavyoweza kujipanga ipasavyo kwa madhumuni ya kutatua kero za Muungano zinazoendelea kutawala mahusiano baina ya Tanganyika na Zanzibar tokea kuasisiwa kwa Muungano mnamo mwaka 1964 ili kilichofanyika Uingereza kisifanyike kwetu.
Kwa lugha nyepesi, ni vyema kutambua hapa kuwa wakati sasa umefika kwa serikali ya Tanzania kuzingatia kwa makini haja ya kuheshimu na kutekeleza maslahi mapana ya Wazanzibari ndani ya Muungano wetu kabla nao hawajachukua hatua za kutaka kujitoa.
Waswahili wanasema hivi: "Ukiona mwenzako ananyolewa, basi na wewe anza kujipaka maji".
Chanzo : Muhammad Yussuf