Tanzania yailalamikia Ugiriki

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
[h=2]Tanzania yailalamikia Ugiriki[/h]

john%20haule%282%29.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule
Serikali kupitia Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imemwagiza Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela, kuiandikia barua serikali ya Ugiriki kuwa Tanzania imechukizwa na kitendo cha Watanzania waishio nchini humo kushambiliwa wiki iliyopita.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alisema wamemwagiza Msekela kuiandikia barua Ugiriki kuwa Tanzania haijapendezwa na kitendo kilichofanya na kikundi cha wafuasi wa chama cha Xris Avgi wakiongozwa na wabunge wao dhidi ya Watanzania waishio nchini humo



Haule alisema katika barua hiyo, wamemwagiza Balozi Msekela kuiandikia Serikali ya Ugiriki kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa Watanzania wanapatiwa ulinzi.

Alisema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa balozi Msekela kama ameshaiandika barua hiyo.

“Tumemwagiza Balozi Nsekela katika barua atakayoiandika kwa Serikali ya Ugiriki aiombe kupitia jeshi la Polisi la nchi kuhakikisha ulinzi katika makazi wanayoishi Watanzani unapatikana,” alisema Haule.

Hata hivyo, alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa chama cha Xris Avgi au Golden Down (Neo Nazi) hakihusiani na tukio lililotokea Dar es Salaam la kuuawa kwa raia mmoja wa Ugiriki.

Septemba mwaka huu, wafuasi wa chama hicho walivamia katika ofisi za jumuiya ya Watanzania waishio nchini humo na kuwajeruhi pamoja na kuharibu mali zao.
 
Back
Top Bottom