Tanzania yaigomea Rwanda kutumia sehemu ya anga lake

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,065
2,362
Tunakumbuka hii ni mara ya pili Rwanda kuiomba Tanzania sehemu ya anga ili iweze kuitumia, taarifa ambazo zipo na kuongelewa na naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano amesema, hawataruhusu Rwanda kutumia sehemu ya anga lake kwa sababu wana mpango wa kusimika RADA nne, pamoja na hayo aliongelea athari za kuruhusu nchi kutumia anga la nchi nyingine, pia aliongelea hasara ambayo tunaipata kwa kuruhusu nchi jirani ya Kenya kumiliki sehemu ya nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Chanzo
 
Huo ndio mpango wa sasa, kwa maana ya anga letu lote kuwa chini ya rada zetu nne.

Enzi zile za awamu zilizopita sekta ya anga ilikuwa inajiendea tu. Ashukuriwe mungu huyu mkuu wa sasa anaheshimu sana professions za watu, mamlaka ya anga ipo chini ya wanaanga wenyewe.

Rwanda na kenya kwa sababu kwao sekta ya anga haikuwa chini ya wanasiasa, walikuwa wakifaidika na anga letu kwa miaka mingi.

Sasa ununuzi wa rada nne maana yake ni kwamba ile sehemu ya anga letu iliyokuwa ikitambuliwa kuwa ipo chini ya rwanda, itarudi kwenye umiliki wetu.

Pato la taifa litaongezeka sana, kwa sababu ya kodi za ukatishaji wa ndege za mataifa mengine katika anga letu.
 
Huo ndio mpango wa sasa, kwa maana ya anga letu lote kuwa chini ya rada zetu nne.

Enzi zile za awamu zilizopita sekta ya anga ilikuwa inajiendea tu. Ashukuriwe Mungu huyu mkuu wa sasa anaheshimu sana professions za watu, mamlaka ya anga ipo chini ya wanaanga wenyewe.

Rwanda na Kenya kwa sababu kwao sekta ya anga haikuwa chini ya wanasiasa, walikuwa wakifaidika na anga letu kwa miaka mingi.

Sasa ununuzi wa rada nne maana yake ni kwamba ile sehemu ya anga letu iliyokuwa ikitambuliwa kuwa ipo chini ya Rwanda, itarudi kwenye umiliki wetu.

Pato la taifa litaongezeka sana, kwa sababu ya kodi za ukatishaji wa ndege za mataifa mengine katika anga letu.

Nidai shilling 500 ya silver
 
sasa na nyie Azam mmeanza kua kama TBC mbona sauti haisikiki?? naona naibu waziri na mtangazaji wanahojiana hakisikiki kitu!!
 
Huo ndio mpango wa sasa, kwa maana ya anga letu lote kuwa chini ya rada zetu nne.

Enzi zile za awamu zilizopita sekta ya anga ilikuwa inajiendea tu. Ashukuriwe Mungu huyu mkuu wa sasa anaheshimu sana professions za watu, mamlaka ya anga ipo chini ya wanaanga wenyewe.

Rwanda na Kenya kwa sababu kwao sekta ya anga haikuwa chini ya wanasiasa, walikuwa wakifaidika na anga letu kwa miaka mingi.

Sasa ununuzi wa rada nne maana yake ni kwamba ile sehemu ya anga letu iliyokuwa ikitambuliwa kuwa ipo chini ya Rwanda, itarudi kwenye umiliki wetu.

Pato la taifa litaongezeka sana, kwa sababu ya kodi za ukatishaji wa ndege za mataifa mengine katika anga letu.
Mchango mzuri
 
Delegation (Kukasimisha) ya anga la nchi moja kwa nchi nyingine ni kitu cha kawaida kabisa. Kunaitwa kukasimisha kwa sababu first principal ya Chicago convention in haki ya kumiliki anga lako (Convention on International Civil Aviation (the Chicago Convention), each State has complete and exclusive sovereignty over the airspace above its territory). Hivyo huwa kunakuwa na sababu za kiutendaji ili kuhakikisha ufanisi kwa huduma za ndege (air traffic service) au usalama wa ndege. Kwa upande wa ufanisi, hili mara nyingi huzingatia wingi wa ndege na hata ukubwa wa anga lako ili kuwe na tija ya huduma hizi. Hapa nazungumzia kutokuwa na ulazima wa kuweka vifaa vya kuongozea ndege kwa nchi yenye anga dogo wakati jirani zao wanaweza kutoa huduma hiyo. Mfano halisi ni anga la juu la Rwanda na Burundi ambapo huduma hutolewa na Kituo chetu cha Dar es Salaam. Kwa kuangalia ukubwa wa eneo la anga la nchi hizi mbili isingekuwa busara kuwa na anga linalo jitegemea kwa kutilia maanani ukubwa wake. Uwezo wa ndege kubwa kukatisha anga la Burundi au Rwanda ni muda mfupi sana hivyo kutokuwa na umuhimu wa nchi tatu kutoa huduma hiyo kwa kukabidhiana. Nina maana Tanzania kuikabidhi Rwanda au Burudi ndege itakayokatisha anga hilo kisha Rwanda au Burundi kuikabidhi DRC ndege iliyokatisha anga lao. Itakuwa ni muda mfupi sana kutoka anga la Tanzania hadi kufika anga la DRC ukikatisha anga la Burundi au Rwanda. Huu utakuwa usumbufu kwa marubani. Swala la pili ni la usalama ambapo nchi moja inaweza kuwa na uwezo wa kutoa huduma na jirani yake hana uwezo huo hapo pia ukasimishaji wa anga unaweza kutokea. Somalia kwa sababu ya vita anga lake lilikasimishwa kwa Umoja wa Mataifa na huduma kutolewa kutoka Kenya. Sehemu ya Bahari ya Hindi ya anga la Tanzania ilikasimiwa kwa Kenya kwa kuangalia uwezo wa Kenya kutoa huduma kwa urahisi katika eneo hilo na pia kwa kuzingatia njia za ndege.

Swala la kuwa na rada au kutokuwa na rada siyo muhimu sana katika ukasimishaji wa anga kwani kuna njia za kutoa huduma bila kuwa na rada ambazo zinakubalika (Procedural control) hasa kwa anga lisilo na ndege nyingi kama katika nchi nyingi barani Afrika. Swala la rada ya kiraia kuhusishwa na ujasusi au usalama wa nchi ni siasa tu maana hii ni rada iliyo wazi (transparent) tofauti na rada ya kijeshi (ujasusi) ambayo msingi wake mkubwa ni kutokujulikana kwa huyo unayemwangalia. Hata hivyo kutokujua tofauti kati ya rada za kiraia na kijeshi kumeendelea kutumika katika kuharahisha manunuzi ya rada za kiraia kwa kuwandanganya wanasiasa kuwa zinaongeza usalama wa nchi au zinakusaidia kujihami dhidi ya jirani yako mwenye rada. Ukweli zinaongeza uhakika wa huduma ya air traffic services ukilinganisha na anga lisilo na rada. Na hii ni kweli unapokuwa na anga lenye ndege nyingi na huenda isiongeze tija yoyote kwa anga lenye ndege chache kama ilivyo katika nchi nyingi barani Afrika.

Kwa kumalizia, swala la Rwanda kuomba kukasimishwa sehemu ya anga la Tanzania ni kutaka kuwa na anga kubwa ili kupata uhalali wa kutoa air traffic services katika anga lake ambalo kwa sasa liko chini ya kituo cha Dar es Salaam kutokana na udogo wake. Itakuwa kichekesho kama Rwanda wataanza kutoa huduma hii katika kianga kidogo hivi ingawa kisheria na kwa principle za Chicago convetion kuhusu usafiri wa anga wana haki ya kufanya hivyo katika anga lao. Nafikiri Rwanda wamewekeza kuliko mahitaji halisi katika air traffic services hivyo kujikuta hawana jinsi bali kuwaomba watanzania wawafikirie. Tanzania wamekata! Nchi nyingine pekee yenye uwezo wa kukasimisha anga lake kwa Rwanda ni DRC ambao sidhani hata kama wanaweza kusikiliza maombi ya Rwanda achilia mbali Rwanda wenyewe kujaribu kufanya hivyo kutokana na mahusiano yao. hata hivyo tusisahau hali ya kidunia ambapo mataifa yaliyo katika umoja hasa wa kiuchumi yana jaribu kuwa na anga la pamoja ili kuwa na gharama za chini za uendeshaji na kuongeza tija kwa kupunguza mipaka katika anga zao. Labda EAC itakapo kuwa imekomaa Rwanda wanaweza kufikiriwa kama wadau katika hili. Kwa sasa ni ngumu sana kwa Rwanda kuweza kuwashawishi jirani zake hasa kwa kutilia maananni historia ya wanyarwanda inayowahusisha na tuhuma (zisizothibitishwa) za kujitanua.

Tunakumbuka hii ni mara ya pili Rwanda kuiomba Tanzania sehemu ya anga ili iweze kuitumia, taariba ambazo zipo na kuongelewa na naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano amesema, hawataruhusu Rwanda kutumia sehemu ya anga lake kwa sababu wana mpango wa kusimika RADA nne, pamoja na hayo aliongelea athari za kuruhusu nchi kutumia anga la nchi nyingene, pia aliongelea hasara ambayo tunaipata kwa kuruhusu nchi jirani ya Kenya kumiliki sehemu ya nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Eti waliomba anga ya Tanzania ili "KUITUMIA"
Acheni kuchonganisha Tanzania na Rwanda.

Nchi moja kucontrol anga za nchi nyingine ni jambo la kawaida sana especially kama nchi haina mitambo ya kucontrol airspace yake yenyewe.
 
Nilimsikia Naibu Waziri Mhandisi Edwin Ngonyani kupitia Azam Tv kuwa wamekataa, akasema japo ni marafiki zetu tena sana ila huwezi jua baadae itakuaje.
 
Back
Top Bottom