Tanzania yagoma kutia saini sera ya ardhi EAC

Tanzania yagoma kutia saini sera ya ardhi EAC

CULCULUS

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
316
Reaction score
619
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amegoma kusaini mikataba ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) unaohusu sera za ardhi, ulinzi na mambo ya nje. Sitta ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC unaofanyika Burundi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo wamelikataa ili lirejeshwe kwa wakuu wa nchi kwa uamuzi.

Hali hiyo ilifanya mkataba huo kusainiwa na nchi nne tu za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hivyo kuiacha nafasi ya saini ya Tanzania kubakia wazi.

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Stragomena-Tax Bamwenda alisema jambo hilo ni nyeti, lakini akaweka bayana kuwa ujumbe wa Tanzania utapaswa kutoa taarifa kwa baraza kufafanua msimamo wao.

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Lazaro Nyalandu aliweka wazi kwamba suala la ardhi halipaswi kuwa sehemu ya EAC. Alionya kwamba kuna mazingira yanayoashiria kuwa baadhi ya wajumbe wa nchi za jumuia hiyo wamekuwa wakiangalia ardhi ya Tanzania kwa jicho la husuda.

Mbunge huyo wa Singida Kaskazini alisema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo inawapa nafasi Watanzania kuchagua eneo la kwenda kuishi.Lakini akasisitiza kuwa ardhi hiyo lazima ibakie kwa ajili ya Watanzania na vizazi vijavyo.

Tanzania imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Jumuia kwa msimamo wake kuhusu ardhi hivyo kukwamisha juhudi za kuimarisha EAC

Source:
Tanzania yagoma kutia saini sera ya ardhi EAC
 
photo+3-IMG_1745.jpg


Huyu akiweka msimamo wa kutia saidini Kikwete atachangamkia kwa sana tu.
 
naunga mkono kwa dhati maamuzi ya serikali ya tz kwa msimamo wao huo,
kwa kutolifanya suala la ardhi kuwa sehemu ya muungano wa shirikisho hilo.😛oa
 
Hawa watu wanataka ku-share kitu ambacho wenyewe hawana. Wacha tulaumiwe, ardhi yetu watuachie, hata ikibidi tuondoke EAC.
 
waTanzania mmoja mmoja au kwa vikundi hatuna umiliki wa kisheria wa ardhi yetu kwa matumizi mbali mbali hasa makazi na mashamba...mlolongo wa umiliki ni mrefu sana na wa gharama kubwa! Sidhani kama ni muda muafaka wa kufungua milango ya ardhi kwa EAC wakati sisi wenyewe bado hatujawa na umilikiwa kisheria wa ardhi yetu!
 
....Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Lazaro Nyalandu aliweka wazi kwamba suala la ardhi halipaswi kuwa sehemu ya EAC. Alionya kwamba kuna mazingira yanayoashiria kuwa baadhi ya wajumbe wa nchi za jumuia hiyo wamekuwa wakiangalia ardhi ya Tanzania kwa jicho la husuda....
Nyalandu amehamia lini wizara ya afrika mashariki? Au ni mimi naanza kupoteza kumbukumbu!
 
Kwa kweli naunga mkono uamuzi wa serikali yangu,yaani hata wasikubali,mimi ni mmoja wa wa2 niopinga wageni kumiliki ardhi na si mzungu tu hata mkenya sitaki,jamani hivi na ardhi tukishare watz tunabaki na nini?
 
Embu naombeni tuletewe hiyo document tuisome na sisi wananchi
 
ardhi isiwe sehemu ya makubaliano yoyote ya JAM...... ndiyo maana hata Tanganyika na Zanzibar zilipoungana...... ardhi haikuwa sehemu ya muungano..... ikizingatia sisi na wazenj ni damu damu...... sasa sembuse nyang'au...... pambaf@;#;';😡
 
waTanzania mmoja mmoja au kwa vikundi hatuna umiliki wa kisheria wa ardhi yetu kwa matumizi mbali mbali hasa makazi na mashamba...mlolongo wa umiliki ni mrefu sana na wa gharama kubwa! Sidhani kama ni muda muafaka wa kufungua milango ya ardhi kwa EAC wakati sisi wenyewe bado hatujawa na umilikiwa kisheria wa ardhi yetu!

Sawasawa kabisa, tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye sekta ya ardhi kabla ya kutia saini hayo makubaliano.
 
Back
Top Bottom