MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,878
- 5,881
uko sawa kabisa mkuu.kwanza wawekezaji wa ndani pamoja na viwanda vilivyoanzishwa waangaliwe suala la operation cost ni kubwa kutokana na kodi kubwa ambayo wanatozwa ..pia serikali iwape motisha kwa wawekezaji wa ndani wanaotaka export nje ya nchi hasa taxes reduction ya atleast 30% kama wanavyofanya nchi jirani mfano kwa sasa dangote kawekeza kiwanda cha cement tanzania ila ukija suala ya bei ya cement ya dangote ni cheap compare na twiga cement reason ikiwa anapata punguzo toka serikali ya nigeria kwenye uwekezaji huo....
Frankly, Tanzania ya viwanda ni ngumu sana kwa mfumo huu.
Unapoongelea rasilimali watu ujue unaongelea skilled and unskilled labour.
Mfumo wa elimu ni mbovu (umekufa) hivyo skilled competent labour ni ngumu kupatikana sasa na pia huko mbeleni. Hii inaongeza gharama kwa kiwanda kuajiri skilled labour na kulipa bei kubwa (wachache waliopo ni ghali au waajiri nje ya nchi kwa gharama zaidi). Ni ndoto kuwaza viwanda kama kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka.
Pili unskilled labour (vibarua) ni expensive. Nchi tunazoiga watu wanatumikishwa kwa ujira mdogo na tunaviona hivyo viwanda vyao tunavyotaka kuiga. Mfano, China, Indonesia, Vietnam etc. watu wanajiua kwa sababu ya kazi nyingi, ngumu, ujira mdogo na zero compliance to safety regulations. Huku, generally speaking, ni ngumu kupata vibarua wanaokubali mazingira hayo ya kazi.
Teknolojia pia ni tatizo. Teknolojia inaongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza gharama. Kwa sababu Serikali haijaweka kipaumbele katika R&D tunaona nchi haina ubunifu katika sekta ya teknolojia. Hivyo inabidi tu-import teknolojia na hii inaongeza gharama katika kiwanda pia.
Mikopo ya benki ipo katika riba kubwa inayomkimbiza mwekezaji. Mfano unataka kuagiza mashine kwa mkopo wa benki, utaona riba ni kubwa, pia kwa sababu mashine itahitaji repairs, spares nazo utaagiza nje kwa sababu hapa hamna. Hii inaongeza pia gharama.
Mfano mwingine ni gharama ya vitu kama umeme. Umeme pia ni tatizo. Gharama za umeme zipo juu. Unaweza ukaajiri watu kwa bei kubwa, ukanunua vifaa na mashine zako kwa bei kubwa na kwa mkopo na umeme usiwake kwa mwezi. Hiyo ni hasara!
Pia ili uwe na viwanda inabidi uwe na serikali rafiki na sekta binafsi na wakezaji (wa nje na ndani). Kwa miezi hii michache serikali imekua aggressive kiasi kwamba inatisha wawekezaji. Hapa hatujaongelea kodi kibao serikali hii inazotoza.
Hivyo kuendesha nchi kwa viwanda ni mfumo. Ni sera endelevu na huwezi kukurupuka na kuanza tu. Ni kuwa na sera bora katika elimu, ubunifu, sayansi na teknolojia, miundombinu n.k
nakubaliana na wewe. Tatizo letu sio sera ila wanaotekeleza hizo sera. Yawezekana JK alikuwa na maono mazuri ila wanayobeba hayo maono ni wezi,wafitini,mafisadi, wenye nia mbili na wabinafsi. Ili kuwapata hawa hakuna haja ya kutafuta maraika ni kufanya kinachofanyka sasa. Tunatumbua huku tunaplan na kuimpliment. Lakini taifa lazima liwe na Progression plan ya kuandaa kizazi adilifu kuliVusha katika stage mbalimbali linalopitia.Sera ya matokeo makubwa sasa(BRN) ILIMSHINDA MTANGULIZI WA JPM... KAMA INGEFAA JPM ANGEIHUISHA UPYA ILI IENDANE SAMBAMBA NA MFUMO WA VIWANDA... EMBU ANGALIA MALAYSIA TULIPOCOPY HIYO BRN WAO WAKO WAPI KIUCHUMI...WAKO MBALI ZAIDI YETU..SHIDA MOJA TZ SIASA NYINGI, KUBEBANA KWINGI NK
Kwanza tukiangalia sera ya viwanda vidogo na kati iko vizuri sana shida ni utekelezaji wake umekua shida.
Tuanze na SIDO imepewa mandate ya kusaidia wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati viweze kufanya primary and secondary processing. Mafunzo wanatoa kisha wanatekelezwa kwa maana mwenye wazo hasaidiwi vya kutosha kufikia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda hivyo.
Wakati huo huo SIDO wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali hao kwa riba kubwa lakini core busiiness ya shirika sio kutoa mikopo bali kusaidia viwanda vidogo na kati na kama ni mikopo ilibidi itolewe kwa wajasiriamali wenye mawazo yanayotekelezeka.
Nini kifanyike rais magufuli alifumue shirika la umma sido lirudi kwenye core business yake, waanzishe viwanda vidogo, kukuza viwanda vido ili viwe vya kati na vya kati viwe vikubwa. Sido iondokane na mambo mengine yote badala yake kusaidia SMEs tu.
Ukuaji wa viwanda vidogo ndio msingi wa kukua kwa viwanda vya kati na vikubwa.
Sehemu ya kwanza inayoweza kufanya transfomation ya uchumi wa tanzania ni agro processing. Angalia tu muhogo technolojia ya kusindika haizidi 3million lakini bado watu wengi hawajaingia. Shida kubwa mitaji na pale inapopatikana riba kubwa.
Ilipaswa kuwa na faida kubwa sana nchi hii kuongozwa na chama kimoja kama China,Singapore etc, badala yake pamekuwa hakuna leadership na continuity ya progressive plan. Nyerere aliondoka na yake, mwinyi, mkapa,jk. Tunawaheshimu kwa kulisimamia taifa ila pia nao walikuwa na mapungufu yao. Sasa jpm anapaswa kuweka basement ya uhakika kama sio walewale.Siaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasa. Tangu wameshika hatamu wameshindwa kupiga maarufuku hata toothpick na pamba za masikio kuagizwa kutoka nnje ,wakat pamba twalima wenyewe na miti ya kutengenezea toothpick tunayo.
Tatizo tulilonalo ni kukubali kuongozwa na wanasiasa. Nawaambia ukweli. Hatutatoka hapa tulipo kama hatutampata mtu ambaye yeye hafikilii siasa bali anafikiria nchi na maendeleo kwa ujumla. Yaani mtu ambaye kichwa chake hakitasema huyu ni ccm wala huyu ni chadema. Bali atajari uzoefu na ujuzi wa huyo mtu kumuweka kwenye sekta inayofaa. Yaani tumpate mtu ambaye yeye yupo tayar kukitoa sadaka chama chake cha siasa kwa sababu ya nchi hii. Na awe na maono sio mbwembwe wala ulaghai. Na pili awe tayari kushaurika. Hayo mambo mengine mnayoyasema ni simple tukimpata mtu wa hiviTunatoka katika KILIMO KWANZA japo bado hatujafanikiwa sana, Tunaelekea TANZANIA YA VIWANDA.
Hii ni kitu ninayoiunga mkono 100%. Ni aibu kuimport nguo za mitumba,stick,maziwa ya unga, vyuma,Furniture, na bidhaa kibao huku tuna rasilimali watu,chuma (madini,), makaa ya mawe, mazao ya kilimo na vitu vingi ya kututoa huko.
Unadhani Rais JPM afanye nini ili Mapinduzi ya Viwanda Tanzania yawe halisi. Je unaona spidi hii iko sawa?Watu wamjiandaa kufungua viwanda hata vidogo?Je watu wako tayari kununua bidhaa za ndani? Miundo mbinu na masoko yanaandaliwa kwa kasi inayotakiwa?
unaweza ongeza dhamani kwa taifa kwa kutoa suluisho au nini kifanyike ili mpando hii uwe halisi kwa kila mtanzania.
Ilipaswa kuwa na faida kubwa sana nchi hii kuongozwa na chama kimoja kama China,Singapore etc, badala yake pamekuwa hakuna leadership na continuity ya progressive plan. Nyerere aliondoka na yake, mwinyi, mkapa,jk. Tunawaheshimu kwa kulisimamia taifa ila pia nao walikuwa na mapungufu yao. Sasa jpm anapaswa kuweka basement ya uhakika kama sio walewale.
Yani wangetumia hayo mabilioni wanayoyakusanya Sasa kwan nguvu kununulia haya mashine hizi tukaliteka soko LA east Africa ingekuwa poa sana
Mfano: kipande kidogo tu cha gogo, kunitoa maelfu na malaki ya stick.
Angalia hapa chini mchakato mzima
Uko vizuriTatizo tulilonalo ni kukubali kuongozwa na wanasiasa. Nawaambia ukweli. Hatutatoka hapa tulipo kama hatutampata mtu ambaye yeye hafikilii siasa bali anafikiria nchi na maendeleo kwa ujumla. Yaani mtu ambaye kichwa chake hakitasema huyu ni ccm wala huyu ni chadema. Bali atajari uzoefu na ujuzi wa huyo mtu kumuweka kwenye sekta inayofaa. Yaani tumpate mtu ambaye yeye yupo tayar kukitoa sadaka chama chake cha siasa kwa sababu ya nchi hii. Na awe na maono sio mbwembwe wala ulaghai. Na pili awe tayari kushaurika. Hayo mambo mengine mnayoyasema ni simple tukimpata mtu wa hivi