Tanzania ya VIWANDA: Tuko wapi, tunaenda wapi na kwa spidi Ipi?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mara baada ya tukio la Dangote na sintofahamu ambayo baadae lkamalizwa Vuguvugu la uhamasishaji viwanda kama limepoa. Waziri husika simuoni kwenye media akitoa miongozo uhamasishaji na mikakati ya muda mrefu na mfupi.

Katika Fani ya Kusimamia Miradi, kuna kitu kinaitwa Earned Value Management (EVM). Huu ni utaratibu unaokubalika duniani kuangalia kama uko mbele, nyuma au kwenye muda katika mradi wako mapema badala ya kusubiri mwisho ambapo utagundua umeingia gharama kubwa au mara mbili ambazo ungezizuia kama ungetumia mfumo huo mapema. Kwa kugundua hilo mikakati mikubwa kama hiyo huwekwa katika PHASE na kila Phase ina Muda wake, Ukubwa wake na Gharama zake, matokeo/output na ubora wake.

sisi wananchi kama wadau wa Viwanda tunaomba mchanganuo, au waziri atufahamishe tuko wapi, tunaenda wapi kwa mafanikio yapi katika phase hii.

Mimi ni mmoja wa watu wanaeamini katika tanzania ya viwanda inayowezekana kama kila changamoto ikifanyiwa kazi.
 
Back
Top Bottom