Kweli tuna watz wagonjwa wewe mmoja wao, hii ni hoja na wala siyo shambulizi kwa serikali wala kwa mtu. Upo ugumu ktk utekelezaji wa sera ya viwanda, huku ukiwa huna mitaji, elimu na sera iliyo wazi kwa uwekezaji, wa ndani na huo wa nje. Hujui utauza wapi, hujui utashindana vipi, huwajui wanufaika muda utatuambia kama ni mapenzi basi wewe kwa ccm umekufa kuoza kila saa hila na matusiTusi lipo wapi!? Je wewe ni mmoja wa MANIFESTO ile!?
hii iikiendelikiendelea itakuwa ni kwa Mungu.Haiwezekani jana Kilimo kwanza,mara BRN...leo yamefukiwa ,yamefukiwa Tsnzania ya Magafuli viwanda na diabomba-! Tulikuwa na mradi wa Katiba umekufa!,Leo NSSF,na wameanza eti kwameankuwekeza viwanda,walifanya lini haya maandalizi?weledi wanao?!
Mkuu Allen Kilewella labda niweke senti moja kwa uchache. Kwanza, mleta mada kaleta mada nzuri tu inayotugusa kama Taifa na wananchi. Haya ndiyo mambo ya kujadili ingawa yanavurugwa makusudi
Mag3 alileta uzi 'kelele' zinavyotumika kuua hoja za msingi
Nikirudi kwenye mada, mletaji kasema nchi za viwanda ziliwekeza katika human capital
Hoja hii inaeleza kwanini ''viwanda'' tulivyokuwa navyo vichache vilikufa.
Hakuna postmortem wala utafiti wa kisayansi unaojibu hoja hiyo.
Ndipo tunakwenda katika hoja ya mleta mada nyingine
Research and Development: Hii inaeleza kwanini tunahitaji viwanda na kwasababu zipi, katika soko gani na tutawezaje kukabaliana na ushindani.
Pia inaeleza gharama za uzalishaji na jinsi ya kukabiliana na bidhaaza bei rahisi
Tatu, kuna suala la nishati.
Je tutaweza kuwa na nishati ya uhakika na nafuu itakayokidhi gharama za uendeshaji?
Kumbuka nishati ni factor kubwa katika kuamua gharama na uzalishaji
Ikiwa hatujaweza kusambaza gesi, kwa miaka 4 tutawezeshaje viwanda?
Nne, katika region integrations na globalization tutalindaje viwanda tarajiwa?
Kama tutafanya protectionism,tutaweza kumlinda consumer asiwe victim?
Hayo ni kwa uchache,yote yapo katika mwamvuli wa jambo muhimu tusilotaka kuliongelea ambalo ni Dira ya Taifa.
Dira na sera ni vitu viwili tofauti. Hapa tunaongelea vision na policy, na kwamba sera lazima zi reflect dira irrespective ya nani au chama gani kinakuwa madarakani
Wanatuambia wameandika sera ya viwanda ni kwa kutumia dira gani?
Tulikuwa na elimu kwa wote, ikaja kilimo kwanza na kuua sera ya elimu.
Ghafla kama walivyosema wachangiaji wengine BRN na sasa sera za viwanda.
Policy hizi zina reflect dira gani ya Taifa?
Pengine kushindwa kwa viwanda kutatokana na mambo mengi, kubwa ni siasa.
Tatizo letu ni kutokaa pamoja kama Taifa na kupanga kisha kuchagua tunataka nini.
Hatuna hamasa ya kujifunza kutokana na makosa yetu (retrospective) na tunaendesha mambo kisiasa kuliko utaalamu.
Tungerafuta kwanza, kwanini Tanganyika packers, Mutex, Mwatex, Mgololo, Kilimanjaro match box, Tanalec, General tyre, Moshi machine, Mangula Machine, Moro polyester, Morproco n.k. n.k. vilikufa tukipata jibu tuanzie hapo
Je, hatuna pamba ya kutosha, hatuna wavaaji wa kutosha, hatuna magari ya kutosha, hatuhitaji vipuri n.k.
Jibu rahisi ni ndiyo kama ni hivyo tulifeli wapi na je sababu za kufeli tumezibaini na kuziondoa?
Mtanzania wa kawaida, ambaye anawakilisha kundi la walio wengi, hawezi kununua hata juice ya Azam. Ushindani wa masoko ya nje ni mkubwa mno; sidhani kama tutauweza kwa miongo kadhaa ijayo. Kundi la Watanzania walioweza kununua hata hizo juice linapungua kutokana na serikali kubana matumizi etc; halafu sijui wanadhani hizo bidhaa za Tanzania ya viwanda watamuuzia nani!
Ni kweli mkuu...wengi wananunua juice ya shilingi 100 inayowekwa kwenye chupa za maji zilizotumika. Kwa kweli tunahitaji mipango na mikakati madhubuti ili kufikia kuitwa Tz ya viwanda...Mtanzania wa kawaida, ambaye anawakilisha kundi la walio wengi, hawezi kununua hata juice ya Azam. Ushindani wa masoko ya nje ni mkubwa mno; sidhani kama tutauweza kwa miongo kadhaa ijayo. Kundi la Watanzania walioweza kununua hata hizo juice linapungua kutokana na serikali kubana matumizi etc; halafu sijui wanadhani hizo bidhaa za Tanzania ya viwanda watamuuzia nani!
I wish huyu jamaa angekuwa anafanyiwa consultation hata monthlyStimulus package muhimu, huwezi kuwa unabana matumizi, mishahara midogo halafu unataka muwekezaji aje hapa, wananchi masikini bidhaa hazitanunulika
hii ni moja ya setbacks ya hiyo dream ya Tanzania ya viwanda
Uwezo wa kununua utachochewa na ajira katika hivyo viwanda na ongezeko la uzalishaji mali hasa kwa vijana kuanzisha ajira binafsi kama kufuga samaki na nyuki ambvyo vitapelekwa viwandani kuchakatwa.Kitulo kuna hoja imetolewa kwamba kabla ya kuuza nje ni lazima kwanza kujenga uwezo wa watanzania kwenye kununua vitu vitakavyozalishwa nchini. Lakini inaonekana kama vile kuna mpango mahsusi wa kupunguza uwezo wa watanzania kwenye kununua.
nani?I wish huyu jamaa angekuwa anafanyiwa consultation hata monthly
Huyo uliosema kuwa anabana hadi mishahara.nani?
Hieanda walimanisha vowanda vya maneno matupu kama hapa kazi Tu!Binafsi ninapousikia huu usemi napatwa na kigugumizi ,kwa elimu yangu ndogo hii ya uchumi katika dunia ya utandawazi nina maswali mengi kushinda majibu kwa mfano
1.Viwanda vinavyotajwa kwenye makaratasi na mikutano mbalimbali ikitokea vikazalisha bidhaa tutauza wapi? (Market ya products at global level) Je tuta charge tarrifs na quotas kubwa bidhaa za ulaya na Mashariki ya mbali ili zetu ziuzike?
2.Swali la pili sambamba na swali lililopita ,hatuna technology, wala Reseach and deveopment centres ambazo ni nyumba ya innovations na technological capabilities so we depend totally on imported technology and machines. Tutawezaje kupambana katika soko na watu ambao wametuuzia technology? (assume machines tunazo however the fact hatuna) huu sio mpambano wa Tembo na sungura?
3.Swali la tatu historia inaonyesha nchi zote zilizoendelea kiviwanda waliwekeza kwenye rasilimali watu (human capital) tena kwa muda mrefu tu ,itawezekana vipi hii paper policy itekelezelezwe ndani ya miaka mi 5?
4.kwa wanaojua maana hasa ya Globalization is an attemp to make African countries to be primary producers wa raw materials hii ni moja ya objectives zao major political global powers hili halina ubishi utandawazi ni ubepari !hivyo basi kutangaza viwanda kwa nchi za ulaya na East Asia ni kutangaza vita ya masilahi tumejiandaa vipi kukabiliana na hili?tulijifunza kweli kwenye sera ya ISI pilicy ambayo tuli adopt soon after independence ikafa tukajaribu Export promotion industrialization ikafa kibudu ikafuata ujamaa policy then import liberalization na sasa SIDP?
5.Ushirikishwaji wa nchi za kiafrica zingine katika kuunda efficient regional integration and cooperation kwa kuwa na common markets ,free trade areas na ku charge ushuru mkubwa bidhaa za nje ya ukanda ili viwanda vya nyumbani (infantry industry) vikue kama wanavyo propose "Prof viners pure theory of international trade " na kuongeza bargaining power as a regional bloc ukoje na tumehamasishaje?
Au Tanzania as a single countrypeke yake
itazuia soko lake kuuzwa bidhaa kutoka nje ya nchi kama ilivyotokea mwaka 1667 nchi za ulaya walipozuia marekani wasiingie bidhaa za chuma Europe?
6.Aliyetunga sera ya viwanda kupitia chama cha mapinduzi alizitambua changamoto hizo juu?Je kwakutumia tu utashi wa kawaida wa kujua kusoma na kuandika hii sera inatekelezeka ndani ya miaka mitano?????
7.Tukiangalia kwa undani safari ya sera ya technolojia na viwanda na Africa kiujumla zinafana fanana ila moja ya sababu ya kufeli hii sera at first place Tanzania ni kushindwa ku repair machine. kwakua in Africa hamna technological transfer na patent rights za technolojia ni kubwa mno kiasi kwamba wataalamu wengi wana link acquisation ya technolojia na heavy debt burden (mikopo mikubwa) na bado wana control technolojia zao hata baada ya kukukodishia inatia umasikini bara la Africa vipi baba Magufuli umejiandaa nalo vipi hili?
Mbaya zaidi hizi imported technology hatuwezi ku adapt katika mazingira yetu (indegeneous technology )
8.Swali lingine je watunga sera ya viwanda wanajua kuwa maendeleo ya Africa yanaendeshwa na sera za nchi za magharibi?unajua kwanini huu ni muongo wa sita tangua Africa ianze kupata uhuru imeshindwa kuwa na self reliant development (self sustained) licha ya kuwa ni kinara wa resources?
Maswali ni mengi mno,sera ya viwanda kwa sasa hivi ni ya chama hii maana yake nini ikitokea chama kingine kikachukua madaraka upo uwezekano wakaifutilia mbali muda huo lazima tutambue hamna Taifa limekua kiuchumi bila maendeleo ya sayansi ,Techolojia na viwanda katika share yake kwenye GDP,BOP, kutengeneza ajira,kuongeza kipato na kuboresha maisha ya raia wake katika level mbalimbali za kijamii .
Hii hoja inaibua mjadala pia, Je sera ya nchi ikoje katika kukuza maendeleo ya sayansi na Technolijia?Je ilifeli ndo maana ikaanzishwa political party initiation ya viwanda?Huku sio kuanzisha administrative bureaucracy?Yaani tumeanzisha kitu ambacho kilishakuwepo lakini hakukuwa na utekelezaji maana yake tulishafeli?
Wasalam
Hivyo viwanda vinatoka wapi na kwa Sera IPI...???Wewe ukiambiwa viwanda unaelewa nini? Au unajitoa ufahamu!?
Tatizo uwezo wako ni mdogo. Na mwisho wa siku utakuwa pungu wani. Nenda kwenye tovuti za Serikali mipango ukajifunze na kusoma dira ya maendeleo na Sera mbalimbali. La sivyo utabaki kuwa na kichwa kikubwa bila akili.Hivyo viwanda vinatoka wapi na kwa Sera IPI...???
Mtu wa kwanza kupelekwa Mahakamani ni Mtei na Mbowe.Kama mfumo wa haki ungekuwepo bongo, hii serikali ilitakiwa kufikishwa mahakamani na watu waka-resign maana kwenye kampeni watu waliambiwa kwamba serikali itajenga viwanda halafu baada ya kuanza kazi waziri anasema serikali haitajenga kiwanda na kazi ya serikali ni kupiga saundi ili wawekezaji waje! Kama ndivyo basi hakukuwa na haja ya kuwadanganya wapiga kura kwa sababu awamu zote zilipiga saundi ili kuvutia wawekezaji.