Tanzania ya viwanda: Another failure at first place

Nawe tushauri tujipangaje? Au tuambie ulivyojipanga ili tuige mfumo wako tupate maendeleo kwa pamoja. Sisi ni wajamaa.
 
Mhh umenitisha
 
na viwanda vikija je tutatoa wapi nishati kama cha dangote tu kimetutoa jasho kukipa umeme?
 
Tutaanza na viwanda vya matofali
 
Yaani mnatumia nguvu nyingi na muda Mwingi kujadili vitu ambavyo haviwezekani kufanyika Tanzania hata kwa miaka 70 ijayo...

Unaongeleaje habari za Viwanda wakati watoto wetu wanakaa chini madarasani,,,???

Hospitali hazina dawa,,,??
 
Yaani mnatumia nguvu nyingi na muda Mwingi kujadili vitu ambavyo haviwezekani kufanyika Tanzania hata kwa miaka 70 ijayo...

Unaongeleaje habari za Viwanda wakati watoto wetu wanakaa chini madarasani,,,???

Hospitali hazina dawa,,,??
Wewe ukiambiwa viwanda unaelewa nini? Au unajitoa ufahamu!?
 
ooohhhh!! ni ile ile,iliua mwatex,sunguratex,zzk mbeya,urafiki textile.........leo eti inaaminika kujenga viwanda!!!
 
Mkuu Allen Kilewella labda niweke senti moja kwa uchache. Kwanza, mleta mada kaleta mada nzuri tu inayotugusa kama Taifa na wananchi. Haya ndiyo mambo ya kujadili ingawa yanavurugwa makusudi

Mag3 alileta uzi 'kelele' zinavyotumika kuua hoja za msingi

Nikirudi kwenye mada, mletaji kasema nchi za viwanda ziliwekeza katika human capital

Hoja hii inaeleza kwanini ''viwanda'' tulivyokuwa navyo vichache vilikufa.

Hakuna postmortem wala utafiti wa kisayansi unaojibu hoja hiyo.
Ndipo tunakwenda katika hoja ya mleta mada nyingine

Research and Development: Hii inaeleza kwanini tunahitaji viwanda na kwasababu zipi, katika soko gani na tutawezaje kukabaliana na ushindani.

Pia inaeleza gharama za uzalishaji na jinsi ya kukabiliana na bidhaaza bei rahisi

Tatu, kuna suala la nishati.
Je tutaweza kuwa na nishati ya uhakika na nafuu itakayokidhi gharama za uendeshaji?

Kumbuka nishati ni factor kubwa katika kuamua gharama na uzalishaji
Ikiwa hatujaweza kusambaza gesi, kwa miaka 4 tutawezeshaje viwanda?

Nne, katika region integrations na globalization tutalindaje viwanda tarajiwa?
Kama tutafanya protectionism,tutaweza kumlinda consumer asiwe victim?

Hayo ni kwa uchache,yote yapo katika mwamvuli wa jambo muhimu tusilotaka kuliongelea ambalo ni Dira ya Taifa.

Dira na sera ni vitu viwili tofauti. Hapa tunaongelea vision na policy, na kwamba sera lazima zi reflect dira irrespective ya nani au chama gani kinakuwa madarakani

Wanatuambia wameandika sera ya viwanda ni kwa kutumia dira gani?
Tulikuwa na elimu kwa wote, ikaja kilimo kwanza na kuua sera ya elimu.

Ghafla kama walivyosema wachangiaji wengine BRN na sasa sera za viwanda.
Policy hizi zina reflect dira gani ya Taifa?

Pengine kushindwa kwa viwanda kutatokana na mambo mengi, kubwa ni siasa.

Tatizo letu ni kutokaa pamoja kama Taifa na kupanga kisha kuchagua tunataka nini.

Hatuna hamasa ya kujifunza kutokana na makosa yetu (retrospective) na tunaendesha mambo kisiasa kuliko utaalamu.

Tungerafuta kwanza, kwanini Tanganyika packers, Mutex, Mwatex, Mgololo, Kilimanjaro match box, Tanalec, General tyre, Moshi machine, Mangula Machine, Moro polyester, Morproco n.k. n.k. vilikufa tukipata jibu tuanzie hapo

Je, hatuna pamba ya kutosha, hatuna wavaaji wa kutosha, hatuna magari ya kutosha, hatuhitaji vipuri n.k.

Jibu rahisi ni ndiyo kama ni hivyo tulifeli wapi na je sababu za kufeli tumezibaini na kuziondoa?
 
Umeshaonyeshwa plan yake?
 
Kichwani umepigwa brush ukang'aa, very resourceful argument.
 
Katika mazingira haya ya nchi za Kiafrika nchi kama Tanzania ikiwa serious itahitaji miaka si chini ya 50 kuwa na uchumi wa viwanda.
Tunaposikia kuwa Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda tunaogopa na kuingia chini ya uvungu sababu Tanzania ya Magufuli sana sana itakuwa ya miaka 10 sasa huo uchumi wa viwanda unawezekanaje ndani ya muda mfupi kiasi hicho?
Hakuna uwekezaji au mapinduzi kwenye maeneo muhimu kama elimu, nishati wala utafiti, itawezekanaje?
Tungeweza hata kuanzisha utaratibu wa kuvutia watu wenye ujuzi kutoka nchi zingine wahamie Tanzania kwa mfumo wa green card na hapo tungewalenga kutoka mataifa kama Syria ambako wataalamu wake wanatangatanga huku na kule sababu ya vita. Tungewatoa hata Libya pia lakini serikali zetu hizi zina akili fupi sana hasa ukizingatia zinaweka mbele maslahi ya chama kuliko nchi.
Tanzania ina potential kubwa mno, tembea mikoani utaona lakini hakuna thinking.
Kingine kinachoharibu mambo ni huu utaratibu wa kuendesha kila kitu kutoka serikali kuu. Kwa nini kila anayekuja kuwekeza aende TIC Dar es Salaam wakati lengo lake ni kujikita Katavi? Kwa nini mikoa isiachwe huru kujiwekea mipango yake ya uwekezaji na kujitafutia wawekezaji duniani kama inavyopenda? Hii italeta ushindani na penye ushindani ndipo taifa hupiga hatua vinginevyo tumeshakwama na hatutoki hapa ng'o.
 


Kuna kasoftware kadogo kamuhimu sana kamekosekana pahala. Kangetupaisha sana
 
Nguruvi3 umetoa darsa kubwa sana kwa kuidadavua hoja iliyoletwa na mleta mada. Kuna jambo umeligusia ambalo najiuliza kama ni asili yetu (Nature) ama inatokana na makuzi yetu? Watu kwenye mada muhimu kama hii wanaichafua kwa kuleta maswali na majibu mepesi mepesi kwa kufauta ushabiki wao wa vyama vyao vya siasa, inakera!!
 

Muda umefika Tanzania inahitaji kutenga majimbo kutokana na potentials na kisha kuembrace INTEGRATED DEVELOPMENT PLANNING with focus to potentials available at localities. Hii mambo ya uchumi kupangwa na kuendeshwa na central gvt haina tija. Yenyewe ibaki kucoordinate mambo across regions
 

Mkuu achana na wanasiasa walishawaona wananchi wapumbavu wewe unasema viwanda Umeme bado changamoto viwanda nchi yoyote yenye viwanda ina umeme wa uhakika
 

Bavicha ndo walitaka kuprit pesa mpya kwa kuhisi wananchi wameficha pesa ndani jitafakari sio kila anaekosoa serikali Bavicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…