Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,281
Wanabodi,
Nilikuwa nimelala , mara usingizi ukakatika, nikaanza kuwaza haya na yale na mara nikawakumbuka wahanga wa tetemeko la Bukoba!, poleni! .
Kiukweli nchi yetu ya Tanzania, ni nchi ya ajabu sana!. Tumepata janga kubwa la tetemeko la ardhi, tuaonyeshwa jinsi watu wanavyotaabika na wanavyoteseka, kwa kukosa makazi, watu wanalala nje baada ya kubomokewa na nyumba zao.
Watu mbalimbali ikiwemo jumuiya ya kimataifa wakaguswa na mateso ya binadamu wale, wakajikusanya na kujitoa kuchangia, huku nchi zenye kujua kitu kinachoitwa "disaster emergency rapid response" wakarespond immediately kwa kutoa fedha na misaada ya kibinaadamu kwa haraka sana ili kusaidia kuwapunguzia watu mateso binadamu wale!, kitu cha ajabu kibisa, misaada ile ikahifadhiwa ili kuja kutumika kukarabati Miundombinu ya umma baadaye!, tuwe wakweli, toka ndani ya nafsi zetu, is this fair?!.
Hao waliotuchangia kwa haraka, walichanga kutokana na kuguswa na uharibifu wa Miundombinu ya umma au kutokana na kuguswa na mateso ya binadamu wale, wakajitoa ili kusaidia humanitarian support ili binadamu wale wapunguziwe mateso, na sio kuchangia Miundombinu ya umma, ni haki kweli kuitumia misaada ya kibinaadamu, kukarabatia Miundombinu ya umma? !.
Kwa walioguswa na mateso na tabu za binaadamu wale na wakaahidi kusaidia kiasi hiki na kile, baada ya kugundua kumbe michango yao sio tena ya kubinaadamu kuwasaidia binadamu wale bali ni michango ya development kukarabati Miundombinu ya umma, kweli wataendelea kutoa kwa moyo ule ule, au watawajibika kutoa tuu hivyo hivyo kwa shingo upande kwa vile waliahidi kwa sababu ahadi ni deni?!.
Tukisema Tanzania ni moja za nchi za ajabu kabisa humu duniani, ni kukosa uzalendo kwa nchi yetu pale kitu kinapothaminishwa kuliko utu, ambapo kwenye janga kama lile la tetemeko lilihilohitaji a massive humanitarian support kupunguza mateso ya binadamu, lakini badala ya nchi yetu kuweka priority kwenye watu kwa Katha mini utu wa mtu na kuelekeza misaada hiyo iwe ni ya kibinaadamu kusaidia kupunguza mateso kwa watu, sisi priority yetu ni Miundombinu ya umma!, yaani hiyo Miundombinu umma ndio yenye umuhimu zaidi kuliko utu, kuliko ubinaadamu kiasi cha kufanya imepewa umuhimu wa kwanza, halafu misaada ya kibinaadamu watu kuambiwa "kila mtu kuubeba msalaba wake mwenyewe!" is this fair? !
Lengo la swali hili ni kuelimishana tuu kuhusu hiki kinachofanywa na serikali yetu kwanza kama ni fair, na pili if it is right, kwa sababu serikali yetu inaongozwa na binaadamu na sio na malaika, ili if it is not fair na it is not right, kuwepo watu ambao tuliona na tukasema ili utakapofikia muda wa karma to hit back, watu wasibaki wakijiuliza why, references zipo na tutakumbushana humu humu kama tutakuwepo.
Ni swali tuu! .
Paskali.